Habari za Punde

Madalali na Waendesha Minada Wasiofuata Sheria Kukiona cha Moto.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akifafanua kuhusu matumizi ya Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License) baada ya kuuzindua, ambapo amewataka madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni ili wafanye biashara yao ya udalali kwa mujibu wa Sheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akifafanua kuhusu matumizi ya Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License) baada ya kuuzindua, ambapo amewataka madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni ili wafanye biashara yao ya udalali kwa mujibu wa Sheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizungumza na wawakilishi wa madalali pamoja na wahakiki mali wa mikoa Tanzania Bara kabla ya kuzindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni.
Mwenyekiti wa Madalali wa Mahakama Tanzania Bara Bi. Mwamvua Kigulu (kushoto) akizungumza jambo kwa niaba ya madalali wa mahakama wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni.
Mwenyekiti wa Madalali Binafsi Tanzania Bara Bw. Phidel Katundu (kulia) akizungumza jambo kwa niaba ya madalali binafsi wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia  mfumo huo kuwasilisha maombi yao ya leseni.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akimkabidhi leseni ya udalali iliyotolewa kwa njia ya Kieletroniki Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono Bi. Scholastika Kevela, mara baada ya kuzinduliwa kwa Mfumo wa  Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal- Auctioneers License), Jijini Dar es salaam. 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa nne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbalimbali wa Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya Madalili na Wahakiki mali kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara mara baada ya kuzindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji Leseni za Udalalli na Uendeshaji wa Minada ya Hadhara Tanzania Bara (GAMIS Portal-Auctioneers License), Jijini Dar es Salaam, ambapo madadali wote wanatakiwa kuanza kuutumia mfumo huo  kuwasilisha maombi yao ya leseni.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James mewaonya madadali na waendesha minada Tanzania Bara kuacha mara moja kufanya biashara hiyo bilaa kujisajili kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Bw. James ametoa onyo hilo Jijini Dar es Salaam wakati akizundua Mfumo Mpya wa Kieletroniki wa utoaji leseni za udalali na uendeshaji wa minada ya hadhara Tanzania Bara ambapo watoa huduma hiyo kuanza sasa wanatakiwa kujisajili kupitia mfumo huo kwa njia ya mtandao wa Internet ama kupitia simu zao za kiganjani.

‘’Napenda kuwafikishia taarifa hii wananchi wote, hasa Madalali na waendesha minada, kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa wote watakaojuhusisha na shughuli za udalali na uendeshaji wa minada bila kuwa na leseni halali’’ alisema Bw. James.

Aliziagiza Taasisi zote za Serikali kufanya kazi na Madalali na waendesha minada ambao wanatambulika kisheria na kwa kufanya hivyo watakuwa wameisaidia Serikali kujipatia mapato yatakayotokana na ada ya leseni itakayolipwa na wafanyabiashara ya udali na waendesha minada.

“Mfumo huu utapunguza changamoto zilizokuwepo hapo awali ambazo zilikuwa zinatumia mlolongo mrefu wa kupata leseni kwa kuwa mfumo huo  umeunganishwa na Mfumo wa Malipo wa GePG ambapo mwombaji ataweza kulipia ada ya leseni kwa kutumia benki, mawakala au simu za kiganjani na hivyo kurahisisha na kuboresha ulipaji, kupunguza gharama za ulipaji na kuongeza uwazi na udhibiti wa Fedha za Umma.

Bw. James aliutangazia Umma kuwa kuanzia  tarehe 24 Februari, 2020 maombi yote ya leseni za Udalali na Uendeshaji wa Minada Tanzania Bara yawasilishwe kupitia Mfumo wa Utoaji wa Leseni za Udalali na Uendeshaji Minada ambao unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango (www.mof.go.tz);

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. Chotto Sendo, amesema biashara ya udalali na uendeshaji wa minada hapa nchini imekuwa ikikua kwa kasi na hivyo kutengeneza ajira, kuongeza kipato pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Bw. Chotto aliongeza kuwa leseni za Udalali na uendeshaji wa minada Tanzania Bara zinatolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa mujibu wa sheria ya waendesha minada ya Mwaka 1928 iliyorejewa Mwaka 2002, na Wizara imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kutatua changamoto zinazowakabili wadau hawa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Wakizungumza kwa niaba ya madalali, Mwenyekiti wa Chama cha Mdalali wa Mahakama Bi. Mwamvua Kigulu na Mwenyekiti wa madalali Binafsi Bw. Phidel Katundu, wameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kubuni mfumo huo utakao wapunguzia gharama ya kufuata huduma ya usajili jijini Dodoma.

Wameiomba Serikali kudhibiti madalali wasio na leseni au wale wasiosajiliwa kwa kuwa wanaikosesha Serikali mapato pamoja na kuchafua taswira ya biashara ya udalali nchini.

Wamemwomba Katibu Mkuu Bw. Doto James kupitia upya Sheria ya Udalali ya Mwaka 1928 ambayo wamesema imepitwa na wakati na inakwaza shughuli za udalali nchini ikiwemo urasimu wa ufanyakazi kazi zao kutoka kwa mamlaka za Serikali Kuu hasa makatibu Tawala wa Wilaya ambao wanataka kupata vibali kutoka kwao kabla ya kutekeleza kazi zao za udalali katika maeneo husika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.