Habari za Punde

Mamia ya Wananchi na Viongozi Zanzibar Washiriki Maziko ya Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Marehemu Mkusa Sepetu Yaliofanyika Kijiji Kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi"A" Unguja leo 16-2-2020.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika kisomo cha hitma kumuombea  Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Mkusa Sepetu, kabla ya Sala ya Maiti, iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mbuzini Wilaya ya Magharibi "A" Unguja (kushoto kwa Rais) Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othma Ngwali na (kulia kwa Rais)Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said.  
Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe,.Dkt, Amani Karume akishiriki katika kisomo cha hitma kumuombea Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Mkusa Sepetu iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mbuzi (kushoto ) Sheikh Fadhil Soraga na (kulia) Katibu wa Mufti Mkuu Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume 
Baadhi ya Waheshimiwa wakishiriki katika kisomo cha hitma ya kumuombea Marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Jaji Mkusa Sepetu kabla ya kuusalia mwili wa marehemu katika Msiki wa Ijumaa Mbuzini Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo.
Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalib Ali Mfaume akihitimisha kisoma cha hitma ya marehemu Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar Jaji Mkusa Sepetu iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mbuzini Wilaya ya Magharibi "A" Unguja.kulia Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Khamis Juma Maalim, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwaliu, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Mhe. Zuberi Ali Maulid, wakiitikia dua. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.