Habari za Punde

Matembezi ya Tamasha la Utalii wa Baskeli Kivutio Kwa Wageni Mkoa wa Kusini Unguja. Kuutangaza Utalii wa Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud wa kwanza (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa mwakakogwa Mzee Mwita wakati wakiwa katika ziara ya Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya vitu vya asili kutoka Makunduchi,ukiwemo Msikiti Kichaka hutembelea na Wageni wanaoifika Kijiji cha Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya michezo ya Asali Mkoa ya Kusini Unguja wa kupigana magomba, wakati wa maadhimisho ya Mwaka Kongwa hufanyika kila mwaka Kijiji cha Makunduchi Unguja.
Baadhi ya vyakula vya Asili ya Kusuni Unguja moja ya Maonesho ya Tamasha la Utalii wa Matembezi ya Baskeli kutangaza Utalii wa Ndani Zanzibar Mkoa wa Kusini Unguja.
Mmoja wa Washiriki wa Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja Kudrat Mussa kutoka Tanzania Bara akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha hilo na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Kiboje Wilaya ya kati.
Fundi Mkuu wa Baskeli katika msafara wa Tamasha la Utalii wa Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja Juma Lukodwa akikabidhiwa Cheti cha ushiriki wa Tamasha hilo na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Kiboje Wilaya ya kati.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akimkabidhi Cheti cha ushiriki wa Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli  Vuai Ali Maneno kutoka Vilabu vya Baskeli Zanzibar hafla iliyofanyika Kiboje Mkoa wa Kusini Unguja .
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akiwakabidhi Baraza la Vijana la Wilaya ya kati Baskeli na Vifaa vya kazi huko Kiboje Wilaya ya kati katika Ufungaji wa Tamasha la Utalii wa ndani kwa kutumia Baskeli Mkoa wa Kusini Unguja.
Baraza la Vijana kutoka Wilaya ya Kusini Unguja wakikabidhiwa Baskeli na Vifaa vya kazi na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud hafla iliyofanyika Kiboje Wilaya ya kati.
                      Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.