Habari za Punde

SERIKALI IMEFANIKIWA KUDHIBITI CORONA -WAZIRI UMMY


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akikata utepe wakati wa uzinduzi wa makabidhiano ya vifaa vya Kunawia Mikono kudhibiti ugonjwa wa Covid 19 Mkoa wa Tanga kulia ni Country Director Water Mission Benjamini Filskov.
SERIKALI imesema kuwa imefanikiwa kudhibiti na kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya virusi vya corona huku ikiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ili kuutokomeza kabisa.


Hayo yalisemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake ya kushtukiza kwenye kwenye Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga ambapo aliweza kuzungumza pia na wahudumu wa Afya na kupokea msaada wa vifaa vya kunawia maji kudhibiti Ugonjwa wa Covid 19 vilivyotolewa na Shirika la Water Mission Tanzania

Mwalimu alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na wananchi wake na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa imeweza kuudhibiti ugonjwa huo huku ikiendelea na juhudi za kuumaliza kabisa.

"Kwa kiasi kikubwa tumeweza kuidhibiti corona na sasa tunaelekea kuumaliza kabisa, tuachane na kusikiliza baadhi ya vyombo vya habari vya wenzetu wanaotaka kututisha kuhusu ugonjwa huu" Alisema.

"Lakini pia ndugu zangu waandishi wa habari mnaona hali halisi hapa tumefika hakuna mgonjwa hata mmoja wa corona, hivyo muwajulishe wananchi habari hizi kwamba ugonjwa tumeudhibiti na hatuna kituo chenye wagonjwa wa corona ndani ya mkoa wetu" Alisisitiza Mwalimu.

Aidha alifafanua kwamba wananchi wote wanaokwenda kupata huduma za kijamii ni lazima waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya corona kwa kufuata maagizo ya serikali na wataalamu wa afya.

Awali alipofika katika kituo hicho cha afya alikuta hali ya msongamano wa wagonjwa katika eneo la kusubiria huduma ya kuonana na daktari.

Mwalimu alisema kuwa kutokana na msongamano huo kuna asilimia kubwa ya kupatikana maambukizi ya corona kwa wagonjwa hao ambao pamoja na kuvaa barakowa lakini walikaa kwa kubanana sana jambo ambalo limempa wasiwasi.

"Wagonjwa wamefuata tiba hapa lakini kuna wasiwasi watu wakaondoka na corona, mnatakiwa muendelee kujikinga, nimeona pale nje mnanawa kwa maji tiririka na sabuni, barakowa mmevaa lakini kwa mlivyokaa kwa msongamano mnaweza kuambukizana" alisema.

Hata hivyo waziri alimuagiza Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Ngamiani Angelina Mashaka pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kupata eneo la kuongeza sehemu ya kukaa wagonjwa wanaofuata tiba ili kuepusha msongamano.

Vile vile alimtaka Mashaka kuendelea kuwakumbusha wagonjwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya corona wanapofika kupata tiba kwa kuzingatia tahadhari zote zinazotakiwa.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Ngamiani Angelina Mashaka 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya kunawia mikono kudhibiti ugonjwa wa Covid 19 hayo kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Msaidizi wa Afya Mazingira Wizara ya Afya Salvata Silayo na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwa kwenye kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga wakati aliopokwenda kukabidhi vifaa hivyo kulia ni 
Mwakilishi wa Mkurugenzi Msaidizi wa Afya Mazingira Wizara ya Afya Salvata Silayo 
Country Director Water Mission Benjamini Filskov kushoto akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Jonathan Budenu.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Country Director Water Mission Benjamini Filskov .
Sehemu ya vifaa ambavyo vimetolewa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.