Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi wakuu wa Serikali na Wabunge wa Bunge la 11 wakiwa wamesimama wakati ukipingwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo Jijini Dodoma.
WABUNGE wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wamesimama
wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya uvunjaji wa Bunge la 11,uliofanyika
16-6-2020 Jijini Dodoma
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania la 11, wakati wa hafla ya uvunjaji rasmin wa Bunge hilo, hafla hiyo
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bunge Jijini Dodoma 16-6-2020,( kulia
kwa Rais) waliokaa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mhe. Samia Sululu,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Mhe; Balozi Seif Ali Iddi na Spika
wa Baraza la Wawakilishi. Mhe. Zuberi Ali Maulid
VIONGOZI
wa Wakuu wa Serikali kutoka Kushoto Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi.Mhe Zuberi
Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson, wakifuatilia hutuba ya Rais
wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli wakati wa hafla ya uvunjaji wa Bunge la 11.
WABUNGE wa Bunge la 11 wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kulivunja
Bunge hilo Jijini Dodoma
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli
akitoka katika ukumbi wa mkutano wa Bunge la 11, baada ya kumaliza hutuba yake
ya kulivunja Bunge hilo akiongozana na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali
Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, wakitoka katika ukumbi wa mkutano wa Bunge la 11 baada ya
kuvunjwa rasman, wakiongozwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dk. Tulia Ackson
No comments:
Post a Comment