Habari za Punde

Dkt. Hussein Mwinyi Ajitokeza Kuchukua Fomu ya Kugombea Kuteuliwa Urais wa Zanzibar Kupitia CCM Ikiwa Mwanachama wa Tano wa CCM Kuchukua Fomu leo.b\A

Katibu wa Idara ya Oganizeshi ya CCM Zanzibar Ndg. Galoso Nyimbo akimkabidhi Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Mhe. Hussein Mwinyi , hafla hiyo imefanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar  leo mchana. Akiwa Mwanachama wa Tano wa CCM kuchukuwa Fomu ya Kuwania kuteuliwa na CCM kupeperusha Bendera ya CCM katika uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Octoba 2020.
Mgombea nafasi ya Urasi wa Zanzibar Mhe. Dkt.Hussein Mwinyi akiwaonesha Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar. baada ya kukabidhi kwa utaratibu mwengini wa kutafuta wadhamini


Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akiwa na Maofisa wa CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar wakimuongoza kuelekea katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Afisi hiyo.
Mwanachama wa CCM Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi , akizungumza na waandishi wa  habari baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea nafasi hiyo kupitia CCM. 


WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk.Hussein Mwinyi amechukua fomu ya kugombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dk.Mwinyi ambaye ni mtoto wa pili wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi amechukua fomu hiyo leo Juni 17,mwaka 2020 katika ofisi za CCM Zanzibar huku akiomba radhi kwa waandishi wa habari baada ya kueleza kuwa hajajiandaa kuzungumza na vyombo vya habari kwasababu lengo lake ilikua ni kuchukua fomu ya kugombea urais tu.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo Dk.Mwinyi amesema kuwa "Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima na afya njema.Nimekuja kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar.Pili nakishukuru Chama changu kwa demokrasi ya hali ya juu ndani ya chama inayomhusu kila mwanachama kugombea nafasi anayoitaka, hivyo nashukukuru kwa hilo.

"Niombe radhi leo sikuja kuzungumza na waandishi, nimekuja kuchukua fomu na tayari nimeshaichukua.Hivyo narudi kwenda kuangalia matakwa yanayotakiwa kwenye fomu hii ili niweze kuijaza na hatimaye nirudishe kabla ya muda kwisha.Mazungumzo yatakuwepo wakati mwingine, wakati muafaka, wala sina la kuzungumza maana hata yaliyoko kwenye fomu sijayajua, hivyo mtaniwia radhi, sitakuwa na mengi zaidi ya hayo,"amesema Dk.Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.