Habari za Punde

DK.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo Julai 4,mwaka 2020 ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar. 

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar kuanzia Majira ya Saa 8:00 Asubuhi. 

Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Taarifa ya mapendekezo ya Wana CCM waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Kikao hicho ni maalum kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108 na 109  (1), (7). 

Aidha Chama Cha Mapinduzi kinaeleza kuwa Kikao hicho ni miongoni mwa Vikao Vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa Mujibu wa Kanuni na Miongozo ya CCM. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.