BAADHI ya wananchi Kisiwani Pemba, wakinunua na
wengine kuangalia nguo kwa ajili ya maandalizi ya skukuu ya Eid el Hajj katika
maeneo ya mji wa Chake Chake.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WANANCHI wakiwa katika moja ya mabanda ya kuuzia
nguo kutoka kwa wafanyabishara wadogo wadogo wa soko la jumapili, mbele ya
Hoteli ya Chake Chake.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
BIASHARA ya Mikungu, Vungu, na viotezo imekuwa kwa
kasi katika kuelekea skukuu ya Eid el Hajj katika maeneo mbali mbali ya Chake
Chake, pichani akinamama wakichagua bdhaa hizo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
VIATU vya Kimasai vimekuwa vikipendwa na wananchi
wengi, ikiwa ni moja ya utamaduni waviatu hivyo kuvaliwa na kanzu muda wa
asubuhi wakati wa kwenda Msikitini kusali sala ya Eid, pichani mwananchi
akiangalia viatu hivyo.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
IKIWA skukuu ya Eid el Hajj imefika, wananchi mbali
mbali wakichagua viatu kwa ajili ya maandalizi ya skukuu hiyo, katika eneo la
jua kali mjini Chake Chake.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
BIASHARA ya mayai imeonekana kuwa juu katika kipindi
hiki cha kuelekea skukuu ya Eid el Hajj, ambapo treya mmoja inauzwa kati ya
shilingi elfu 15,000/= hadi 14,000?=, pichani mmoja ya wauzaji wa mai hayo
akimtilia mteja wake.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
BIDHAA ya Samli,Siagi, Tomato Pest na viungo vya
kupikia vyakula, vimekuwa ni kitu muhimu katika kuelekea skukuu pichani mmoja
ya wafanya biashara akiwauzia wateja wake Tomato Pest kama alivyo kutwa katika
eneo la mji ya Chake Chake.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment