Habari za Punde

Waziri Bashungwa ameibuka mshindi wa kura za maoni 587 sawa na 86.5% kati ya wagombea 34.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akifurahi na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Karagwe mara baada ya kutangazwa  mshindi wa kura 587 kati ya kura 679 ambazo ni sawa na asilimia 86.5 kati ya wagombea 34 waliojitokeza kugombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika jimbo la karagwe. (Picha na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara)
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu mara baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi jimbo la Karagwe Mkoani Kagera.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akiweka kura yake kwenye sanduku la kukusanya kura za maoni  katika mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi jimbo la Karagwe mkoani Kagera.
Jennifer Bashungwa (Mama Alaska) Mke wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa, {aliyeshika karatasi} akihesabu kura alizopata mme wake mara baada ya wajumbe kumaliza kupiga kura katika mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi jimbo la Karagwe mkoani Kagera.
 Wagombea 34 wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi wakisikiliza maelekezo ya uchaguzi wakati wa kura za maoni katika mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi jimbo la Karagwe mkoani Kagera.

Na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara.

Bashungwa ametangazwa kuwa mshindi baada ya kupata kura 587 kati ya kura 679 ambazo ni sawa na asilimia 86.5 kati ya wagombea 34 waliojitokeza kugombea ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi katika jimbo la karagwe.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Karagwe Merry Kananda ametangaza matokeo ya wagombea wote 34,  kura zilizopigwa ni 679 na hakuna kura iliyoharibika na matokeo ni kama ifuatavyo; Adrian Katesigwa 5, Ajuna Jefta 0, Alex Nkuba 0, Athanase Albert 0, Boniface Kazoba 2, Charles Gabikwa 1, Elivis Bikombo 2, Elipidius Kalamu 2, Ester Kakulima 0, Erasmus Ereneus 1, Faustine           Kisheny 3, Getrudius Kazingo 0, Girson Ntinmba 0, Gordian Kikompolisi 0, Ibrahim Bushagama 0, Iman Masenge 1, Innocent Bashungwa 587, Joachim Stewart 1, Joseph Kaham 48, Lameck Byamukama 6, Mjaibu Mutabazi 0, Moris Mulilo 1, Nicholaus Batalingaya 1, Njunwa Kebile 1, Noanatus Bakatagula 2, Octavius Kashorobwa 0, Onesphoa Kabalyenda 0, Robinson Mutafungwa 5, Sadock Peter 0, Sima Rwakilomba 0, Sparon Kinyina 1, Stevene Revelian 0, Straton Mushongi 2, Vedasto Gotifridi 7.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kura za maoni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi jimbo la Karagwe, Waziri wa Viwanda mna Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ameanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu pia amewashukuru wajumbe wa mkujano mkuu jimbo la Karagwe
“ Mwenyezi Mungu amenigusa kupitia wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya karagwe, wakati naomba kura nimesema tumepita pamoja kwenye milima na mabonde na nikawaomba mnivushe katika bonde la leo na mmenivusha kwelikweli”

Ameendelea kwa kuwaahidi kuendelea wathamini, kuwaheshimu na kuchapa kazi kuliko kipindi cha miaka mitano inayoisha maana ushindi waliompa unaendana na kiu ya maendeleo ya wananchi walioowawakirisha katika mkutano huo na ameendelea kuwaomba wajumbe na wananchi wote wa wilaya ya Karagwe waendelee kumuombea ili apitishwe kwenye vikao vinavyofata ili aweze kuipeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.