Habari za Punde

Vyakula na Vinywaji Visivyo na Kilevi Vimeshuka Bei kufikia 4.9 August 2020 ukilinganisha 6.7 July 2020.

Mtakwimu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Salma Saleh Aliy akiwasilisha Mfumko wa bei Agosti 2020 mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani  huko katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini.
(Picha na Mwashungi Tahir  Habari Maelezo)
Mwashungi Tahir     Maelezo Zanzibar.   3-9-2020.
Kasi ya mfumko wa bei kwa mwaka uliomalizia August 2020 umeshuka kufikia 2.4 ukilinganisha na 3.6 kwa mwezi wa July 2020.
Akizungumza na waandishi wa habari Mtakwimu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Salma Saleh Aliy huko katika ukumbi za  Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali iliopo Mazizini  wakati alipokuwa akiwasilisha mfumko wa bei.
Amesema chakula na vinywaji visivyo na kilevi vimeshuka kwa kufikia 4.9 August 2020 ukilinganisha 6.7 July 2020.
Aidha amesema miongoni mwa vyakula vilivyoshuka ni pamoja na mchele wa mbeya , wa pembe , unga wa sembe, ndizi mbichi samaki ,mafuta ya taa , saruji .
Kwa upande wake Meneja wa Idara ya Uchumi Tawi la Zanzibar (BOT) Moto Ngwinganele amesema hali iliyosababisha  mfumko wa bei kushuka ni chakula kuwepo chakula cha  kutosha  na kutarajia  kuongezeka zaidi.
Pia amesema kwa upande wa mafuta ya taa, disel na Petrol  yameshuka kutokana na kushuka katika soko la dunia  kwa kuwepo   maradhi ya corona.
Vile vile amesema kwamba malengo ya Serikali ni kuona wananchi wanaendelea kupata bidhaa kwa bei nafuu ili waweze kujikwamua kimaisha  na kumudu kununua  bidhaa  ambazo zimeshuka katika masoko yote.
Nao wananchi wamesema wanashukuru Serikali kutokana na kupungua kwa bei na kuweza kumudu kununua chakula.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.