Habari za Punde

WAZIRI WAMALIASILI NA UTALII DKT. HAMISI KIGWANGALLA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI DKT.DONALD WRIGHT WAKUTANA KUZUNGUMZIA UTALII.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright kuelezea mafanikio ya Tanzania katika Uhifadhi wa Maliasili na utayari wa Tanzania kupokea Watalii kutoka  mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani wakati huu wa janga la Corona. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) walipokutana kwa  mazungumzo mafupi yaliyojikita katika kuimarisha ushirikiano na uendelezaji wa shughuli za uhifadhi baina ya Tanzania na Marekani leo  jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia) na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo mafupi yaliyolenga kukuza Utalii hasa wakati huu wa janga la Corona na kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani katika shughuli za uhifadhi.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla kuhusu mchango wa Taifa la Marekani katika shughuli za Uhifadhi nchini Tanzania na namna nchi yake itakavyoendelea kusaidia shughuli za uhifadhi katika eneo la Mafunzo, Teknolojia na Vitendea kazi  walipokutana kwa  mazungumzo jijini Dar es salaam.
PICHA/Aron Msigwa – WMU.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.