Na.Mwashungi Tahir Maelezo 3-11-2020.
UMOJA wa vyama vya siasa visivyo rasmin vimeipongeza Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar kwa kufanya uchaguzi huru na wa haki kuwafanya Wazanzibar kutumia Demokrasia yao ya kumchagua Dkt Hussein Ali Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar.
Ameyasema hayo Katibu wa vyama vya siasa visivyo rasmin Ameir Hassan Ameir wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale ulioko Kikwajuni.
Amesema kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeendesha uchaguzi huo kwa njia ya uhuru na amani hadi kutangazwa Dr Hussein Ali Mwinyi kuwa Rais wa awamu ya nane kwa kupata kura nyingi kwa asilimia 76 ambapo umoja huo umeridhika na maamuzi hayo.
Aidha Katibu huyo amesema uchaguzi umemalizika iliobakia wananchi kuendelea na pirika zao za maisha na kumpa mashirikiano kiongozi huyo aliyeingia madarakani.
“Uchaguzi umemalizika kilichobaki wazanzibar tushirikiane na kiongozi wetu huyu ili tuendeleze maisha yetu”, alisema katibu wa umoja huo.
Vile vile umoja huo umoja huo umewataka viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi walioteuliwa wakiwemo wakilishi, wabunge na madiwani kufanya kazi zao na kuwa na mashirikiano kwa wananchi wote ili tuijenge Nchi.
Hata hivyo umoja huo umefarijika na hotuba ya Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi aliyeitoa mara baada ya kuapishwa kwa kusema kuwa atashirikiana na vyama vya siasa katika kuijenga Zanzibar.
Pia wamewataka wananchi wasipoteze muda wa kukaa vijiweni na kuwa na mategemeo ya kwamba uchaguzi utarejewa na kauli hiyo waifute kwani uchaguzi tayari umemalizika.
No comments:
Post a Comment