Habari za Punde

Hotuba ya Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, katika hafla ya kumuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharrif Hamad - Ikulu Zanzibar 08 Disemba, 2020

 

HOTUBA YA  MHESHIMIWA DK. HUSSEIN ALI MWINYI, RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, KATIKA HAFLA YA KUMUAPISHA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS MHESHIMIWA SEIF SHARIF HAMAD -  IKULU ZANZIBAR

08 DISEMBA, 2020

Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad;

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,

Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla;

Makamu wa Pili wa Rais,

Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid;

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,

Mheshimiwa Omar Othman Makungu;

Jaji Mkuu wa Zanzibar,

Mheshimiwa Dk. Mwinyi Talib Haji;

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,

Waheshimiwa Mawaziri wa Wizara mbalimbali za SMZ,

Dk. Abdulhamid Yahya Mzee;

KatibuwaBaraza la MapinduzinaKatibuMkuuKiongozi,

Mheshimiwa Idrisa Kitwana Mustafa;

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,

Mheshimiwa Dk. Abdalla Juma Saadalla Mabodi;

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,

Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe;

Kiongoziwa Chama cha ACT Wazalendo,

Waheshimiwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Mliohudhuria,

Ndugu Viongozi wa Dini,

Ndugu Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,

Ndugu Viongozi Wote wa Chama na Serikali,

Ndugu Waandishi wa Habari,

Wageni waalikwa,

Mabibi na Mabwana,

Assalam Aeikum,

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

Awali ya yote, namshkuru Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Aradhikwa kutujaalia afya njema na kuweza kukutana hapa Ikulu, kwa ajili ya hafla  hii muhimu ya  kumuapisha Mheshimiwa Maalim Seif  Sharif Hamad, ambae  juzi nilimteua kuwa  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane. Nakushukuru Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad Makamu wa Kwanza wa Rais,  kwa kukubali uteuzi wangu. Ridhaa yako imeniwezesha kutimiza matakwa ya Katiba ya Zanzibar ya  Mwaka 1984 katika Ibara ya 39 - (1), nakuuu:Kutakuwa na Makamu Wawili wa Rais ambao watajulikana kama Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamu wa Pili wa Rais.

Hatua hii muhimu imekamilisha uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane ninayoiongoza.

Nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad kwa kupendekezwa na Chama chake cha ACT Wazalendo ili ateuliwe kushika nafasi ya Makamo wa Kwanza wa Rais. Kupendekezwa kwa jina lake, na kuteuliwa kwake ni ushahidi usio na shaka wa imani kubwa ambayo wanachama na viongozi wa ACT wamewekeza juu yake. Nami kwa kuheshimu na kutambua uzito wa imani hiyo kwake, na imani yangu kwake, nikamteua bila kigugumizi chochote, kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

 Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

Tarehe 2 Novemba, 2020 niliapa katika Uwanja wa Amaan,kuwa Rais wa Awamu ya Nane wa Zanzibar. Katika kiapo changu kile, pamoja na mambo mengine, niliapa kuilinda na kuingoza nchi yetu kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Katiba yetu, Kifungu cha 9 (3) inaelekeza (nanukuu), “Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa wa umoja wa kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia”.Aidha, Kifungu 39 (3) kinanitaka, kumteua Makamo wa Kwanza wa Rais kutoka Chama kilichopata nafasi ya pili katika uchaguzi, na chenye idadi ya kura zaidi ya asilimia 10.

Hapana shaka kuwa uteuzi huu nilioufanya umezingatia na kutimiza matakwa ya Katiba yetu. Mbali na kuwa nitakwa la Katiba, binafsi, mimi ni muumini wa umoja wa kitaifa, mshikamano, udugu na maridhiano. Na amini kwa dhati ya moyo wangu kuwa maridhiano ni njia nzuri ya kujenga umoja wa kijamii na ustawi wa nchi na wananchi wake. Ni jambo linalowaleta watu pamoja, linaloileta nchi pamoja, linalotuhakikishia amani na mshikamano wa kudumu.

Kutokana na ukweli huo, nilielezea katika hotuba yangu ya kufunga Kampeni zangu pale Kibanda maiti na pia katika siku ya Kufungua Baraza la Wawakilishi juu ya dhamira yangu na utayari wangu wa kuyaendelezamaridhianonakuundaSerikaliyaUmojawaKitaifa.

Nilitumiafursahizopiakufafanuamatumainiyangukuwa, kizazi cha leo cha Wazanzibariambaoasilimia 93 wamezaliwabaadayaMapinduzinaMuungano, kinayodhimayakipekeeyakufungaukurasawauhasamanachuki, nakufunguaukurasampyawaupendonamaridhiano. Matamanioyangu, bilashakanayawengiwanayoitakiamema Zanzibar yetu,nikuondoshwakwamajerahanamadondayahistoriayetuya Zanzibar, ambayoyameendeleakuwamtihanikwetumarakwamarakatikachaguzizetu.

 

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

Katikakuyaendelezanakuyastawishamaridhiano, ukowajibuwaviongozi, ukowajibuwavyamavyasiasanaukowajibuwawananchinajamiikwaujumla. Mimi, naahidi, nitajitahidikwakadriyauwezowangukuyajenganakuyadumishamaridhianokwamaslahimapanayanchiyetu. Yale yaliyondaniyamamlakanauwezowangu, nitayatekelezabilakigugumiziwalaajizi.

Kwakuanzia, nimetekelezamaelekezoyaKatibakwakuwafikiawenzetuwa ACT nakuwakaribishakuundaSerikali. Aidha, kwamamlakaniliyonayokwenyeKifungu cha 66 cha Katibaya Zanzibar, nimewateuajanatarehe 7 Desemba, 2020, MheshimiwaNassor Ahmed MazruinaMheshimiwa Omar Said ShaabankuwaWawakilishikutokamiongonimwanafasi 10 nilizopewazakuteuaWajumbewaBaraza la Wawakilishi. Aidha, nitashauriananaMheshimiwaMakamowa Kwanza waRaisjuuyakujazanafasizilizobakikatikaBaraza la Mawazirinanamna bora yakuendeshaSerikaliyetuyaUmojawaKitaifa.

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

Maridhianoyakweliyanajengwakwa mambo makuumatatu:Kwanza nidhamira. Pandezotembilizilizotofautiananilazimakuwanaudhatikatikakufanikishanakuendelezamaelewanobainayao. Maridhianoyaukwelihayawezikupatikananakuwaendelevuiwapowahusikanawadauwotehawanadhamirayakweliyakufikia,kufanikishanakuendelezamaridhianohayo.

Pili, kuvumiliana, kustahamiliananakusahauyaliyopita. Waswahiliwalisema, “Yaliyopitasindweletugangeyajayo”.Maridhianoyoyoteyakijamiihayawezikudumuiwapokilasikututakuwatunakumbushanakwa mambo ambayoyamepita. Ujasiriwamaridhianonikusahauyaliyopitanakutotoneshavidondakwanividondavikitoneshwakilamarahaviwezikupona.

Na tatu,kujengautamaduniwakuaminiana. Maridhianoyoyotehayawezikudumuiwapopandembilizitakuwahaziaminianinakilawakatikutafutasababuyakutupianalawamanakutoanakasoro.

Ndugu Viongozi na Wageni Waalikwa,

Nafahamu kwamba uamuzi wa Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, umezingatia ushauri na maoni  kutoka kwa viongozi na wananchama wa chama Chake. Maamuzi haya yamefanyika kwa kufuata taratibu za Chama cha ACT – Wazalendo na baada ya kufanyika vikao mbali mbali. Kwa hivyo nachukua fursa hii, kutoa shukurani kwa viongozi na wafuasi wa Chama hicho kwa mchango wao katika kufikia kufanyika maridhiano na wakaweza kushirikiana na Chama cha Mapinduzi katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Awamu ya Nane.

Ndugu Viongozi na Ndugu Wananchi,

Kwa upande wangu, maamuzi haya yamefikiwa kwa kuzingatia mawazo, maeleke  na busara kutoka viongozi wa Chama Changu, CCM na siyo maamuzi ya peke yangu. Natoa shukurani kwa viongozi wenzangu wa CCM kwa mawazo yao na maelekezo yao hadi tukaweza kufikia katika hatua hii tunayoishudia hivi sasa. Mafanikio hayo ni kielelezo cha  ukomavu wa CCM katika kuendesha siasa bora hapa nchini.

Ndugu Viongozi na Ndugu Wananchi,

Sisi viongozi kila wakati  hatuna budi kuzingatia na tufahamu kwamba  maslahi ya wananchi ndio jambo la msingi. Tafauti zetu, kama ndogo au kubwa, zisiwe kikwazo cha maendeleo ya wananchi  na nchi yetu kwa jumla.  Katiba ya Zanzibar imeeleza kwamba  ‘Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe’,  Bila ya shaka tumeweza kufikia hatua hiyo kwa sababu tunauelewa ukweli huo wa kikatiba. Nasaha zangu kwa wananchi, ni kwamba sote tuwe kitu kimoja na tuunge mkono juhudi hizi zenye lengo la kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.

Ndugu Viongozi na Ndugu Wananchi

Nimaliziekwakusemakuwa, pamojanamimikuahidikutekelezayaleyaliyondaniyauwezowangu, mafanikioyamaridhianoyetuyatategemeasanautayariwavyamavyetunautayariwawananchiwetukuzipakisogotofautizetunakuyatazamamatumainiyaliyombeleyetu. Mimi naMheshimiwaMaalimSeiftumeonyeshautayarihuo. Ninyinanyiridhianeni, kilammojakwanafasiyake. Tuijenge Zanzibar mpya. Zanzibar yenyemshikamano, Zanzibar yenyemaelewanona Zanzibar yenyeneematupu. Mimi ninayomatumainimakubwasanajuuyahukotuendako.

NakushukurutenaMheshimiwaMakamuwa KwanzaRais, MaalimSeif Sharif HamadkwakuheshimunakutimizamatakwayaKatibanakwamoyowakowamaridhiano. Nakishukuru Chama chakokwaushirikianoambaokimekupa. Nakishukuru Chama changu cha Mapinduzinakwanamnayakipekee, MwenyekitiwangunaRaiswaJamhuriyaMuunganowa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Joseph MagufulinaMakamuMwenyekitiwa CCM naRaisMstaafuwa Zanzibar, MheshimiwaDkt. Ali Mohamed Sheinkwabarakazaonakuungamkonohatuahii. Bilakuwasahau, wananchiwa Zanzibar kwakuungananasikatikahatuanyinginemuhimuyakuijenga Zanzibar Mpya.

 

                                                MunguIbariki, Zanzibar,

MunguIbariki, Tanzania.

Ahsantenisanakwakunisikiliza!

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.