Afisa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akiwafanyia Usajili Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi Zanzibat kutoka Chama cha ACT-Wazalendo Jimbo la Kojani Mhe. Hassan Hamad Omar na Mwakilishi Mteule wa Jimbo la Wingwi Mhe.Kombo Mwinyi Shehe na Mwakilushe Mteule wa Jimbo la Mtambile Mhe. Habibu Ali Mohammed, walipofika katika Ofisi za Baraza kwa ajili ya kufanya usajili na kuriupoti leo kwa hatua nyengine za uapishaji.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ndugu
Raya Issa Msellem akizungumza na Wawakilishi wateule kutoka chama cha ACT
wazalendo Jimbo la Kojani Mhe.Hassan Hamad Omar, Jimbo la Mtambile Mhe. Habibu Ali Muhamed na Jimbo
la Wingwi Mhe. Kombo Mwinyi Shehe mara
baada ya kusajiliwa.
Msimamizi wa Maktaba ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar ndugu Haji Khatibu Haji akiwafahamisha Wawakilishi wateule kutoka
chama cha ACT wazalendo jinsi wanavyoweza kupata huduma katika maktaba hiyo kwa
ajili ya shughuli zao.
Afisa uhusiano wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar ndugu Himidi Choko akiwapa maelezo Wawakilishi wateule kutoka chama
cha ACT wazalendo kuhusu mambo mbali mbali yanayowahusu ukaaji wa wajumbe ndani
ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
Chukwani.
Picha na Masoud Hamad -BLW -Zanzibar.
No comments:
Post a Comment