Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi Ajumuika na Waumini wa Kiislam Katika Sala ya Ijumaa na Dua Maalum ya Kuiombea Nchi Amani Iliofanyika Masjid Mwitani Wete Pemba leo 18-12-2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislam baada ya kumalizika kwa Dua ya kuiombea Nchi Amani na kumuombea dua, iliofanyika katika Masjid Mwitani Wete Pemba leo baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa
 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana kama nchi haina amani, umoja na mshikanao.

Alhaj Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo huko Masjid Mwintani uliopo Mtemani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pembawakati akitoashukurani katika dua maalum iliyotayarishwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ikiwa ni kwa ajili ya kuiombea nchi pamoja na viongozi wa Serikali ambapo tayari kwa upande wa Unguja Ofisi hiyo imeshaandaa dua kama hiyo.

Alhaj Dk. Hussein Mwinyi alitoa shukurani kwa viongozi wote waliohusika katika maandalizi ya dua hiyo na kuwashukuru Waumini na wananchi waliohudhuria dua hiyo maalum.

Alieza haja ya kuendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuijaalia nchi kuwa na amani na kuhakikisha amani hiyo inadumishwa.

Alisema kuwa dhima kubwa ni kuhakikisha amani inadumishwa na kusisitiza kwamba umoja wa kitaifa nao unadumishwa kwa kuunganishwa watu kama kitabu cha Mwenyezi Mungu kilivyosisitiza.

Aliongeza kuwa haposiku za nyuma mifarakano ilikuwa mikubwa kwa sababu tu ya itikadi za kisiasa na kusisitiza kwamba wakati wa mambo hayo umeshapita na tayari kwa upande wao viongozi wameshaanza kufanya kwa vitendo kwa kukubaliana kwa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Alieleza kuwa bado wako wengi ambao hawajakubaliana na dhana hiyo na kusisitiza haja ya kuendelea kuwaelimisha juu ya umuhimu wa wananchi kuwa wamoja.

Alieleza kuwa katika kuleta maendeleo yanayokusudiwa kuletwa ni lazima kuwepo kwa umoja, amani na mshikamano.

Alisema kuwa suala muhimu ni kuwepo kwa amani nchini sambamba na kuwaunganisha wananchi na kuwashukuru wananchi kwa utulivu waliouonesha pamoja na kuipokea Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikiwa ni sababu ya kuleta umoja kutoka ngazi ya kisiasa mpaka kwenye familia.

Alhaj Dk. Hussein Mwinyi alisema kuwa ukurasa mpyaumefunguliwa wa amani na maridhiano na kumuomba MwenyeziMungu aendelee kuidumisha amani hiyo pamoja na kuyatekeleza yale yote yaliyoahidiwa na viongozi.

Aliwataka wananchi kuendelea kuwaombea dua viongozi wao, kuliombea dua Taifa lao sambamba na kudumisha amani na mshikamano na kusisitiza kwamba  iwapo yakifanywa hayo maendeleo makubwa yatapatikana kwani MwenyeziMungu amesisitiza hilo.

Aidha, alitumiafursa hiyo kuwashukuru viongozi wa dini kwa kuiombea dua nchi pamoja na kuidumisha amani iliyopo na kuweza kuhubiri amani hiyo na kuwataka wale wote waliokuwa hawajakubali umuhimu wa umoja waendelee kuwaelimisha pole pole kwnai watafahamu umhimu wa umoja, mshikamano na kuondoa chuki.

Alimshukuru Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabih pamoja na viongozi wote kwa kushiriki dua hiyo.

Dua hiyo maalum iliongozwa na Sheikh Ahmada Hussein Bakari na Sheikh Jamal Mohammed Abeid alitia fatha ya dua hiyo huku mufti akisoma dua maalum ya kufundia dua hiyo.

Mapema akisoma hotuba ya Ijumaa Sheikh Said Abdallah Nassor kutoka Masjid Rahman ya Gombani Chake Chake Pemba alieleza jinsi ya dini ya Kiislamu inavyosisitiza amani, umoja na mshikamano.

Alidha alieleza jinsi Mwenyezi Mungu anavyotaka watu wawe kitu kimoja na wala wasifarakane kwani pale watakapofarakana hapatakuwa na maendeleo yanayokusudiwa kuwepo.

Akitumia aya za Quran pamoja na hadithi za Bwana Mtume Muhammad (S.A.W), alieleza jinsi ya suala la umoja katika maisha ya mwanaadamu na kutumia fursa hiyo kumpongeza Rais Alhaj Dk. Hussein Mwinyi kwa kulisimamia vyema suala hilo kwa kushirikiana na viongozi wenziwe.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.