Habari za Punde

Semina elekezi kwa Walimu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha pili




Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Omar Ali Omar (Bhai) alipokuwa akizingumza na Walimu katika semina elekezi kwa Walimu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha pili, katika ukumbi wa Skuli ya Mahonda


 Baadhi ya Walimu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha pili, katika ukumbi wa Skuli ya Mahonda walioshiriki kwenye Semina elekezi

 Baadhi ya Walimu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha pili, katika ukumbi wa Skuli ya Mahonda walioshiriki kwenye Semina elekezi

Na Maulid Yussuf WEMA

ZANZIBAR

Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Omar Ali Omar (Bhai) amesema sula la  kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya mitihani ni wajibu wa kila msimamizi wa mitihani ili kuleta ufanisi wa kazi zao.



Amesema hayo wakati alipofungua semina elekezi kwa Walimu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha pili, katika ukumbi wa Skuli ya Mahonda Sekondari Mkoa wa kaskazini Unguja amesema kupewa dhamana ya kusimamia mitihani inahitaji kujali haki na sheria na usawa kwa watoto ili waweze kufikia malengo yao.


Amewataka Walimu hao kuhakikisha wanatunza siri katika kipindi chote kwani  utunzaji wa siri ni suala lilolosisitizwa tokea  wakati wa kujaza mkataba wa kuingia katika dhamana  ya kuwa Mtumishi wa umma hivyo utunzaji siri ni jambo la lazima kwa kila mtumishi.


Pia amewasisiza kuwa waadilifu kwa dhamana wanayokabidhiwa kwa kufuata taarabu na miongozo ya sheria inavyowaongooza kwa kutambua kuwa dhamana waliyopewa ni kubwa katika na muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Hata hivyo amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanatumia taaluma zao kwa kuwaondoa hofu Wanafunzi wakati wa kufanya mitihani ili nao watumie muda wao kwa kujibu maswali kwa umakini.


Aidha amewataka wazazi na walezi nao kutumia nafasi zao  kwa kuwanasihi watoto wao  kuepukana na vitendo vyote vinavopelekea  kufanya utanganyifu katika kipindi chote  mitihani yao ili waweze kufaulu vizuri na kufikia mlengo ya Serikali katika kupata wataalamu Wazuri wa baadae.

Kwa upande wao Walimu wanaotarajiwa kusimamia mitihani hiyo wamesema mafunzo hayo yamewasaidia sana na pia wameahidi kuwa watafuata maagizo na masharti yote ya  usimamizi wa mitihani ya ili kuifikia malengo ya Taifa ya kuwa na wataalamu wa fani mbalimbali.

Pia wamewashauri wazazi wote wa Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Taifa kuwatoa hofu watoto wao na kuwanasihi  kuachanana na vitendo vya udanganyifu.

Katika semina hiyo Hakimu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja bwana Nyange Makame Ali ametumia fursa hiyo  kuwaapisha kiapo cha uaminifu   Walimu na  Wasimamizi wote wa mtihani wa Taifa kwa wilaya ya kaskazini B Unguja.


Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha zaidi  ya walimu 120  kwa Wilaya ya kaskazini B Unguja ambapo mitihani ya kidato cha pili inatarajiwa kufanyika  tarehe 22 mwezi huu hapa Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.