Habari za Punde

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA MAJENGO MAPYA YA SHULE YA SEKONDARI IHUNGO MKOANI KAGERA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya kufungua Majengo ya mapya ya madarasa ya Shule ya Sekondari ya wavulana ya Ihungo iliyopo Bukoba mkoani Kagera. Kushoto ni Balozi wa Uingereza hapa nchini David Concar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Majengo Mapya ya Shule hiyo ya Ihungo Sekondari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo, Balozi wa Uingereza hapa nchini David Concar, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akikata utepe kufungua Majengo mapya ya madarasa ya Shule ya Sekondari Ihungo ambayo iliathiriwa vibaya na tetemeko la Ardhi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua madarasa ya Shule ya Sekondari ya Ihungo ambayo ilijengwa upya mara baada ya tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016 mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.