STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 11.02.2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi mpya wa Kamishna wa Bodi ya
Mapato (ZRB), pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar
(PBZ).
Kwa upande wa Bodi ya
Mapato (ZRB), alieteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi hiyo ni Salum Yussuf Ali, uteuzi
ambao umeanza tarehe 10 Februari,2021.
Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi
amemteua Muhsin Salim Masoud kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Watu wa
Zanzibar (PBZ) kuanzia tarehe 10 Februari, 2021.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi
Zena Ahmed Said, Kamishna wa Bodi ya Mapato (ZRB) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki
ya Watu wa Zanzibar (PBZ) waliotenguliwa watapangiwa kazi nyengine kadri
itakavyoamuliwa.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
Good Job
ReplyDelete