Pemba 12.03.2021

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein
Ali Mwinyi, amewataka wananchi watakaokabidhiwa nyumba za vijiji za maafa
zilizojengwa Tumbe Kisiwani Pemba na Nungwi kwa Unguja, kuhakikisha nyumba hizo
wanazitunza ili zisipoteze haiba yake.
Rais Dk.
Mwinyi alisema nyumba hizo hivi karibuni zinatarajiwa kuzinduliwa kwa upande wa
Unguja ikiwa ni pamoja na Pemba, ili wananchi waliokusudiwa waweza kuzitumia.
Aliyaeleza
hayo leo mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua nyumba hizo 15 ambazo
zitakaliwa na familia 30, zilizoko katika kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati waziara yake ya siku moja Kisiwani Pemba.
Aidha,
Rais Mwinyi aliwashukuru wananchi wa Shehia ya Tumbe kuonyesha kuwa wapo tayari
kwa ushirikiano na Serikali yao, huku akisema kwamba changamoto zilizopo katika
nyumba hizo zinashuhulikiwa ili kumailizika kwa wakati.
“Tumeambiwa
kama suala la maji ni changamoto kwa sasa, ila hivi karibuni litamalizika,
fedha za fidia nazo zinashuhulikiwa ndani ya wiki hii zinamalishwa na
changamoto ya idadi ndogo ya watu wanaohitaji kuwepo hapa nayo inashuhulikiwa”alisema.
Katika
hatua nyengien Dk.Mwinyi aliwashukuru wafadhili waliojenga nyumba hizo,
Emirates Red Creasent ya Falme za Kiarabu kwa kazi kubwa walioifanya,
kuhakikisha nyumba hizo wameziwekea na huduma za kijamii ikiwemo, kituo cha
afya cha kisasa, skuli, msikiti na maduka.
Akizungumzia
suala la Amani na Utulivu, Dk. Mwinyi aliwataka wananchi wa Unguja na Pemba,
kuendelea kudumisha amani iliyopo, Umoja na mshikamano, kwani lengo la serikali
ya Umoja wa Kitaifa ni kuwaunganisha watu, kwa kuachana na mifarakano
iliokuweopo.
“Tumefanya
hivi ili kuwaweka wananchi katika hali ya amani, utulivu na usalama ili waweze
kupata maendeleo yaliokuwa bora kutka kwa viongozi wao”alisema.
Hata
hivyo, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa hatua iliyobaki hivi sasa ni serikali
kupeleka maendeleo kutokana na kuwepo kwa amani, umoja na mshikamano, huku
akitambua kuwa kuna huduma nyingi za kijamii zinazohitajika, ikiwemo afya,
maji, elimu barabara na hususan za vijijini, kwani aliwaahidi wananchi wakati
wakampeni kwamba atahakikisha kuwa huduma hizo zinapatikana.
Kwa upande
wa akinamama aliwahidi kuwa Serikali itawapatia mikopo kutoka mabenki, hivyo
wanapaswa kujipanga vyema katika vikundi vyao, kwa kuwapatia mafunzo, mitaji na
masoko, kitu watakachopewa kitakuwa na tija nao.
Nae
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la
Wawakilishi Dk. Khalid Salum Mohamed, alisema kuwa nyumba hizo 15 zinazochukua
familia 30 kwa wakati mmoja, pia kuna hospitali ya kisasa, soko, maduka 15,
msikiti unaochukua watu 350 pamoja na skuli yenye vyumba tisa.
Dk.
Khalid alisema chanzo cha ujenzi wa nyumba hizo ni athari zilizotokea mwaka
2017 za mvua kubwa ya masika, ambayo karibu familia 6500 unguja na Pemba
ziliathiria, lakini watu wa Mwezi Mwekundu walikuja na kushirikiana na serikali
kujenga nyumba za kuwasaidia waathirika hao.
Alieleza
kuwa waathirika ni wengi lakini ilionekana familia 385 ambao nyumba zao
ingebidi vivynje kutokana kuwepo katika maeneo hatarishi, Pemba nzima imeoneka
kuna familia 41 nyumba hizo na hao wapate makaazi hapa.
Aidha,
alisema kuwa mradi kama huo upo huko Nungwi kwa upande wa Unguja, na kueleza
kuwa kwa mujibu wa mkataba serikali imelazimika kutengeneza barabara, Kupeleka umeme
na maji ambapo kwa upande wa maji tayari visima vitatu wameshachimbwa ila hawakufanikiwa
kutokana na uhaba wa maji, lakini hivi sasa wanachimba chengine na kwenda hadi mita
90 na wanatarajia kuyakuta maji.
Kwa
upande wa fidia, Waziri huyo alisema tayari wameshalipa TZS Milioni 16 na TZS Milioni
11 wanatarajia kuzimaliza ndani ya wiki inayofuata, kati ya milioni 27
walizokua wakidaiwa kwa ajili ya fidia.
Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi alifika Mtaa
wa Mpendae Mjini Unguja kwenda kutoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu Dk. Idrissa
Ahmada Khamis aliyefariki dunia hapo jana na kuzikwa leo huko kijijini kwao
Kinduni Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rajab Mkasaba,
Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment