Habari za Punde

Bado Kunahitajika Nguvu ya Pamoja ili Kuisimamia Serikali ya Umoja wa Kitaifa - Dkt.Mzuri Issa.



Na.Mwanajuma Juma.                                                                                                                                   

MKURUGENZI wa Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania 'TAMWA Zanzibar' Dkt. Mzuri Issa amesema bado kunahitajika nguvu ya pamoja ili kuisimamisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Akizungumza katika mafunzo ya Waandishi wa habari juu ya umuhimu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa alisema waandishi wa habari ni lazima wachukuwe jukumu lao katika kuhakikisha lengo la kuanzishwa kwake linafanikiwa.

Alisema kwenye Taifa Ustawi na Umoja wa wananchi ni nguvu kubwa katika kuhakikisha maendeleo yanaatikana.

Hivyo kama waandishi wa habari wanawajibu mkubwa wa kuacha ushabiki wa siasa bali wajuwe kwamba wao ndio wanaopaswa kupaza sauti zao ili jamii izidi kujenga matumaini na Serikali hiyo.

Mapema akitoa mada juu ya umuhimu wa Serikali umoja wa Kitaifa Mkufunzi wa Waandishi kutoka Internews Ali Haji Mwadini alisema pamoja na waandishi kufanyakazi katika mazingira magumu  lakini bado wanajukumu la kuifahamisha jamii hasa wa vijijini kuhusu Serikali hiyo.

Hata hivyo alisema kuwa kufa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya 2010 kulichangiwa sana na waandishi wa habari ambao hawakuweza kutimiza majukumu yao katika kuihamaisiha jamii juu ya uwepo wake.

Hivyo alisema ili wasirejee nyuma ni wajibu wao sasa kutumia kalamu zao kwa kuandika mara kwa mara SUK, ambayo wananchi wanaonekana wana matumaini makubwa na serikali hiyo.

Wakichangia mada hiyo baadhi ya waandishi wa habari walisema kufa kwa Serikali hiyo 2010 kulitokana na waandishi kuwa na woga, kuingiza utashi wa kisiasa pamoja na kutokujiamini juu ya kuandika habari ambazo zinahusiana na SUK.

Hata hivyo walisema pamoja na uwepo wa Serikali hiyo lakini bado wanawoga kwa kuingiza mambo ya nyuma na wengi wao kudhani kwamba ndani ya Serikali hiyo kuna chama cha siasa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.