Habari za Punde

Yacouba Songe Aingarisha Yanga Ligi Kuu Bara Kwa Ushindi wa Bao 1-0

 

Wachezaji wa Timu ya Yanga wakishangilia ushindi wakati wa Mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kuifunga Timu ya Biashara United kwa bao 1-0.


Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuichapa Biashara United bao 1-0 baada ya hivi karibu kuambulia matokeo mabaya katika ligi kuu Vodacom inayoendelea.

Bao la Yanga limewekwa kambani  na mshambuliaji Yacouba Sogne dakika ya 59 akimalizia krosi ya Adeyum Salehe

Katika mchezo huo Yanga ilikuwa na ingizo jipya la beki Dickson Job ambaye amechukua nafasi ya Lamine Moro huku ikiwa mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Yanga dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar.

Kwa Matokeo hayo Yanga wanaendelea kuongoza Ligi kwa kufikisha Pointi 54 kwa michezo 25 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na Pointi 49 kwa mechi 21

Mahasimu wako Simba Sc kesho itashuka dimbani kuumana na Mwadui Fc Mjini Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.