Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa kwanza kulia) akiwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe.Regine Hess ( wa pili kushoto) wakimsikiliza ....Mratibu wa wa Frankfurt Zoological Society Jack Ryan wakati akitoa maelezo katika Viongozi wakati walipotembea Karakana iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inayoendeshwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi la Frunkfurt Zoological Society iliyofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess wakati wakitembelea miradi mbalimbali iliyopo ndani na nje ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inayofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe.Regine Hess wakimsikiliza Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi wa Kanda Maghraibi, Martin Looiboko wakati wakitembelea miradi mbalimbali iliyopo ndani na nje ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inayofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regina Hess mara baada yaembelea miradi mbalimbali iliyopo ndani na nje ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inayofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi akimsikiliz Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess kabla ya kuanza kutembelea miradi mbalimbali iliyopo ndani na nje ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inayofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani
Na.lusungu helela
Serikali ya Ujerumani inatarajia kutoa kiasi cha Yuro Milioni 20 sawa na Shilingi Bilioni 56 za Kitanzania zitakazotumika kwa ajili ya miradi ya mikubwa ya shughuli za Uhifadhi nchini.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti liliyopo wilaya ya Serengeti mkoani Mara Waziri wa Maliasili na utalii,,Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania amesema miradi mbalimbalii inayofadhiliwa na Ujerumani iliyopo ndani na nje ya Hifadhi ina umuhimu mkubwa katika Uhifadhi
Amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuangalia mradi wa Ikolojia ya Serengeti pamoja na mradi wa Ikolojia ya Mwl.Nyerere ( Selous)
Dkt. Ndumbaro amesema msaada huo ni muendelezo wa ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani katika masuala ya Uhifadhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 60
Amesema msaada huo wa fedha h utalinufaisha Shirika la Hifadhi za Taifa ( TANAPA) Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) pamoja na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi la Frankfurt Zoological Society ( FZS)
Aidha, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema mbali ya fedha hizo kutumika katika masuala ya Uhifadhi, Serikali ya Ujerumani imejipanga pia kuzinufaisha Jamii zinazoishi kuzunguka Hifadhi.
Amesema nchi ya Ujerumani ni miongoni mwa Wadau wakubwa wa Uhifadhi nchini ambao wamekuwa wakisaidia masuala mengi katika Uhifadhi ikiwemo tafiti mbalimbali pamoja na vita dhidi ya Ujangili
" Tunaishukuru sana Serikali ya Ujerumani kwa msaada wao kama Wizara na Serikali ya Tanzania kwa ujumla tunasema asante sana " alisema Dkt.Ndumbaro
Amefafanua kuwa mradi huo utadumu kwa muda wa miaka mitatu na unatarajia kuanza hivi mapema mara baada ya bajeti kupitishwa.
katika hatua nyingine, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema katika Azimio la Arusha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusemam kuwa shughuli za Uhifadhi zinahitaji ushirikiano wa Wadau kwa ajili ya kutoa fedha pamoja na utalaamu.
Kwa upande wake, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess amesema msaada huo utasaidia Hifadhi hizo katika kipindi hiki cha mlipuko waa Ugonjwa wa Kovid ambapo idadi ya watalii imepungua.
Ameongeza kuwa Serikali ya Ujerumani imetoa fedha hizo kwa ajili ya kusaidia Hifadhi hizo ikiwa ni kuenzi misingi ya ushirikiano iliyowekwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
No comments:
Post a Comment