JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
NA MATUMIZI KWA MWAKA
2021/22
Kwa upande wa wafanyabiashara, nawahimiza kulipa kodi stahiki kwa Serikali. Si haki wala si uungwana kwa wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi. Kufanya hivyo kutaifanya Serikali yetu ishindwe kutoa huduma muhimu kwa wananchi. Hospitali zetu zitakosa dawa na kusababisha vifo, Watumishi watakosa mishahara na haki zao Stahiki na wanafunzi watakosa elimu bure ambayo ni zawadi tuliyowapa.”
I.
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa
Spika, naomba
kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kukubali kupitisha
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2021/22. Hotuba hii
inawasilisha bajeti ya kwanza ya Kipindi cha Kwanza cha Serikali ya Awamu ya
Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Serikali katika Bunge lako Tukufu yanawasilishwa kwa mujibu wa Ibara ya 137 ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na
Kifungu cha 23 (3) cha Sheria ya Bajeti, Sura 439 pamoja na Kifungu cha 124 (4)
cha Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Juni 2020.
2.
Mheshimiwa Spika, pamoja
na hotuba hii ninawasilisha vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina Bajeti ya
Serikali. Kitabu cha Kwanza ni Makadirio ya Mapato; Kitabu cha Pili ni
Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala wa
Serikali; Kitabu cha Tatu ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Sekretarieti
za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na Kitabu cha Nne ni Makadirio ya
Matumizi ya Maendeleo kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali,
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, Muswada wa Sheria
ya Fedha wa mwaka 2021 pamoja na Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Serikali wa
mwaka 2021 nayo ni sehemu ya bajeti hii.
3.
Mheshimiwa Spika, awali
ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na
kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha Bajeti ya Serikali
kwa mwaka 2021/22. Aidha, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuijalia nchi
yetu amani, umoja na mshikamano na kutupatia kiongozi mwadilifu, thabiti na
imara chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
4.
Mheshimiwa Spika, huu ni
Mkutano wa kwanza wa Bunge la Bajeti baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani uliofanyika Oktoba 2020, ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipata
ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza nchi yetu. Ushindi mkubwa na wa kishindo
uliopatikana kwa CCM umedhihirisha siyo tu imani kubwa ya wananchi kwa Chama
Cha Mapinduzi, bali pia ni matarajio na kiu kubwa waliyonayo ya maendeleo kwa
Taifa letu.
5.
Mheshimiwa Spika,
itakumbukwa kuwa tarehe 17 Machi, 2021 Taifa letu lilipata msiba mkubwa wa
kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli. Naomba kutoa pole kwa Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge lako Tukufu, Wanafamilia
hususan Mama Janeth Magufuli na Watanzania wote kwa msiba huo mzito. Hayati
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ataendelea kukumbukwa kwa uongozi wake shupavu
wenye uthubutu na uzalendo wa hali ya juu ulioleta mabadiliko chanya ya
kiuchumi na kijamii kwa nchi yetu. Mwenyezi Mungu aipumzishe Roho yake mahali
pema peponi. Amina! Aidha, napenda kuchukua fursa hii kutoa pole kwa Watanzania
kwa kuondokewa na Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mhandisi Balozi John
William Herbert Kijazi, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Mwenyezi Mungu azilaze
roho za marehemu hao mahali pema peponi. Amina!
6.
Mheshimiwa Spika, kipekee nitumie fursa hii kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza mwanamke katika
historia ya nchi yetu. Mheshimiwa
Spika naomba Niweke Ufunguo, Katika Hotuba yangu popote nitakapo tumia
neno “MAMA YETU” Nitakuwa namaanisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Katika muda mfupi
wa uongozi wake, MAMA YETU ameonesha dhahiri kuwa ni kiongozi
makini, shupavu, mchapa kazi, mwadilifu, msikivu na aliye na dira thabiti ya
kuendelea kuiletea nchi yetu maendeleo makubwa. Aidha, ninampongeza “MAMA YETU” kwa kupata kura zote za ndio za
wajumbe 1,862 wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.
Wana CCM na watanzania kwa ujumla wana imani kubwa sana kwake katika kukiongoza
Chama kwa kuzingatia misingi ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi hasa ukizingatia
uzoefu wake wa miaka 20 ya uongozi ndani ya chama. Hongera sana Mheshimiwa Rais
na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi. Ninawaomba watanzania wote kila mmoja kwa
imani yake tuendelee kumuombea Mheshimiwa Rais ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi ili Mwenyezi Mungu aendelee kumjalia afya njema, hekima na
busara katika kutekeleza majukumu yake na “KAZI IENDELEE”.
7.
Mheshimiwa Spika, hotuba
hii inawasilisha Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye
Dira na Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita ya “Kudumisha
mazuri ya Awamu zilizopita, Kuyaendeleza mema yaliyopo na Kuleta mengine mapya.
Hivyo, makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22 yameandaliwa kwa
kuzingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ikiwemo: Mpango wa Tatu wa Maendeleo
wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 ambao umeandaliwa kwa kuzingatia
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025;
Dira ya Maendeleo ya Afrika Mashariki 2050; Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063;
Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030; Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo; na
makubaliano mengine ya kikanda na kimataifa ambayo Tanzania imeyaridhia. Aidha,
Bajeti imezingatia kikamilifu maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Hotuba
ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati akilihutubia Bunge hili tarehe 22 Aprili 2021.
8.
Mheshimiwa Spika, naomba
kurejea baadhi ya maeneo yaliyobainishwa katika Hotuba ya Mheshimiwa Rais
ambayo yamezingatiwa katika bajeti hii kama
ifuatavyo: Kudumisha Tunu za Taifa yaani Amani, Umoja na Mshikamano ambavyo
ni msingi mkuu wa maendeleo wa Taifa letu; kuendelea kutekeleza
kikamilifu Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini kwa kufanya marekebisho ya Sera, Sheria na kanuni
mbalimbali ili kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi na kuongeza fursa za ajira;
kufanya maboresho ya mfumo wa utozaji na ukusanyaji wa kodi ili kurahisisha ulipaji
wa kodi na kuongeza wigo wa walipa kodi; na kuendelea kuimarisha uendeshaji wa
mashirika ya umma ili yaweze kujiendesha kwa faida na kutoa gawio na mchango
stahiki kwa Serikali.
9.
Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ni kuongeza tija ya mazao ya kilimo, mifugo
na uvuvi kwa kuboresha upatikanaji wa mitaji kwa wakulima wadogo na wawekezaji
kwa kushirikisha taasisi za fedha, ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo pamoja
na benki nyingine; kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, uongezaji wa thamani ya
mazao na upatikanaji wa masoko; kukuza sekta ya viwanda hususan vinavyotumia
malighafi zinazopatikana kwa wingi hapa nchini na vyenye kuajiri watu wengi;
kuendelea kuziba mianya ya utoroshaji wa madini na kuhamasisha ujenzi wa
viwanda vya uchenjuaji na uchakataji wa madini nchini ili kuongeza mchango wa
sekta ya madini katika Pato la Taifa; kuimarisha miundombinu ya usafiri, usafirishaji na nishati ikiwemo ujenzi wa barabara na madaraja, reli, usafiri wa majini na angani, upanuzi wa bandari pamoja na uzalishaji na usafirishaji
wa umeme; kuendelea kuimarisha na
kuboresha huduma za jamii, hususan afya, elimu na maji; na kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine, jumuiya za
kikanda na mashirika ya kimataifa.
II.
TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA
MWAKA 2020/21
Mwenendo
wa Mapato
10. Mheshimiwa Spika, katika
bajeti ya mwaka 2020/21, Serikali ilipanga kukusanya jumla ya shilingi trilioni
34.88 kutoka katika vyanzo vyote vya ndani na nje. Hadi Aprili, 2021 shilingi trilioni 24.53 zimekusanywa sawa
na asilimia 86.1 ya lengo la kipindi hicho. Mchanganuo ni kama ifuatavyo:
(i)
Mapato yaliyokusanywa kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yalifikia shilingi
trilioni 14.54, sawa na asilimia 86.9;
(ii) Mapato yasiyo ya Kodi yalifikia shilingi trilioni 1.80,
sawa na asilimia 78.5 ya lengo;
(iii) Mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani vya Mamlaka za
Serikali za Mitaa yalifikia shilingi bilioni 607.4 sawa na asilimia 88.5 ya
lengo;
(iv) Misaada na mikopo nafuu iliyopokelewa ilikuwa shilingi
trilioni 1.89 sawa na asilimia 70.4 ya lengo;
(v)
Mikopo ya ndani ikijumuisha mikopo ya kulipa dhamana za Serikali
zilizoiva ilifikia shilingi
trilioni 3.99, sawa na asilimia 95.7 ya lengo; na
(vi) Mikopo ya nje
yenye masharti ya kibiashara ilifikia
shilingi trilioni 1.68 sawa na asilimia 88.1 ya
lengo.
11. Mheshimiwa Spika, mlipuko
wa UVIKO-19 umesababisha kutofikiwa kwa baadhi ya malengo ya makusanyo ya mapato ya ndani hususan kwa
sekta za utalii, usafiri wa anga na uingizaji wa bidhaa kutoka nje. Aidha,
baadhi ya mashirika na taasisi zimeathiriwa na UVIKO-19 na hivyo kupungua kwa michango
na gawio kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Mathalani, mapato ya Shirika la Hifadhi
za Taifa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania yameathiriwa kufuatia kuporomoka kwa shughuli za utalii
kulikosababishwa na kusambaa kwa UVIKO-19 katika nchi zinazoleta watalii wengi
nchini.
12. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha lengo la mapato ya ndani linafikiwa, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali
za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kama ilivyoainishwa ndani ya
Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji na Kufanya Biashara Nchini (Blueprint) kwa lengo la kuchochea ukuaji
wa uchumi. Aidha, Serikali imeendelea kusimamia na kufuatilia utekelezaji
sahihi wa sheria, kanuni na taratibu za kodi; kuboresha mifumo ya TEHAMA
ikiwemo Electronic Fiscal Device Management
System (EFDMS). Vilevile, Serikali imeendelea kufuatilia kwa karibu utendaji wa taasisi za
Serikali pamoja na kuendelea kuhamasisha utalii wa ndani.
13. Mheshimiwa Spika, misaada na
mikopo nafuu iliyopokelewa hadi Aprili 2021 ni shilingi trilion 1.89
ikilinganishwa na shilingi trilion 1.82 mwaka 2019/20. Pamoja na athari za
mlipuko wa UVIKO -19, misaada na mikopo nafuu iliongezeka kwa asilimia 3.84 ikilinganishwa
na kiasi kilichopokelewa katika kipindi kama hicho mwaka 2019/20. Serikali
itaendelea kuimarisha ushirikiano na Washirika wa Maendeleo ili kuwezesha
upatikanaji wa misaada na mikopo nafuu katika kuchangia bajeti ya Serikali.
14. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara, Serikali ipo
katika hatua za mwisho za majadiliano na baadhi ya Taasisi za Fedha za
Kimataifa ili kuhakikisha kiasi kilichopangwa kukopwa kinapatikana. Vilevile,
Serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma kwa lengo la kuongeza ushiriki wa
wawekezaji kwenye soko la ndani la fedha ili kuhakikisha kiasi kilichopangwa
kukopwa kinapatikana kwa wakati.
Mwenendo
wa Matumizi
15. Mheshimiwa
Spika, makadirio ya
matumizi kwa mwaka 2020/21 yalikuwa shilingi trilioni 34.88 ambapo shilingi
trilioni 22.10 ni matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 12.78 ni matumizi ya
maendeleo. Katika kipindi cha Julai 2020 hadi Aprili 2021, jumla ya shilingi
trilioni 24.74 zimetolewa sawa na asilimia 86.8 ya lengo. Kati ya kiasi hicho,
shilingi trilioni 17.42 zilikuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambazo
zinajumuisha shilingi trilioni 6.09 kwa ajili ya mishahara, shilingi trilioni
4.49 Matumizi Mengineyo na shilingi trilioni 6.84 kugharamia deni la Serikali.
16. Mheshimiwa
Spika, hadi Aprili
2021, jumla ya shilingi trilioni 7.32 sawa na asilimia 74.1 ya lengo zimetolewa
kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo shilingi trilioni 6.24
ni fedha za ndani sawa na asilimia 79.7 ya lengo na shilingi trilioni 1.08 ni
fedha za nje sawa na asilimia 52.8 ya lengo.
17. Mheshimiwa Spika,
katika utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa kipindi cha Julai 2020 hadi Aprili
2021, Serikali iliendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia maeneo ya
vipaumbele yaliyoainishwa kwenye bajeti kama ifuatavyo:
(i)
Ulipaji wa deni la Serikali kwa wakati
shilingi trilioni 6.84;
(ii) Ulipaji
wa mishahara ya watumishi kwa wakati shilingi trilioni 6.09;
(iii) Miradi
ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme ikiwemo mradi wa kufua umeme wa
maji wa Julius Nyerere; na mradi wa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) shilingi trilioni 1.02;
(iv) Ujenzi
na ukarabati wa Reli ikiwemo ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa shilingi
trilioni 1.49;
(v) Ujenzi
wa barabara, madaraja, na viwanja vya ndege shilingi trilioni 1.15;
(vi) Ulipaji
wa madeni yaliyohakikiwa ya Watumishi, Wazabuni na Watoa Huduma, Wakandarasi na
Washauri Elekezi shilingi bilioni 965.1;
(vii) Mikopo
ya wanafunzi wa elimu ya juu, elimumsingi bila ada, uimarishaji wa vyuo vya
VETA, kukuza ujuzi kwa vijana na ujenzi wa miundombinu ya elimu shilingi bilioni
406.6;
(viii) Ununuzi
wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu
ya afya shilingi bilioni 265.8; na
(ix) Miradi
ya maji mijini na vijijini shilingi bilioni 207.5.
Tathmini ya Uhimilivu wa Deni la
Serikali
18. Mheshimiwa Spika, Tathmini ya Uhimilivu wa Deni la Serikali ilifanyika Novemba, 2020 kwa
mujibu wa Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada SURA 134. Tathmini hiyo ilionesha
kuwa viashiria vya deni la Serikali viko ndani ya wigo unaokubalika kimataifa
katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu. Katika Tathmini hiyo,
viashiria vinaonesha kuwa: uwiano wa thamani ya sasa ya deni la Serikali kwa
Pato la Taifa ni asilimia 27.9 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 70; uwiano
wa thamani ya sasa ya deni la nje kwa Pato la Taifa ni asilimia 17.3
ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55; na uwiano wa thamani ya sasa ya deni la
nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 113.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 240.
19. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa
viashiria vinavyopima uwezo wa nchi kulipa deni, matokeo yalibainisha kuwa,
uwiano wa ulipaji wa deni la nje kwa mapato ya ndani ni asilimia 13.7
ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 23 na uwiano wa ulipaji wa deni la nje kwa
mapato yatokanayo na mauzo ya nje ni asilimia 14.0 ikilinganishwa na ukomo wa
asilimia 21. Kwa kuzingatia viashiria hivyo, Tanzania ina uwezo wa kuendelea
kukopa kutoka ndani na nje ya nchi ili kugharamia miradi ya maendeleo na pia
ina uwezo wa kulipa mikopo inayoiva kwa wakati.
Mwenendo wa Sekta ya Fedha
20.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka unaoishia Aprili 2021,
viwango vya riba za mikopo ya benki kwa ujumla vilipungua na kufikia asilimia
16.58 kutoka wastani wa asilimia 16.91 Aprili 2020. Riba za mikopo za kipindi
cha mwaka mmoja zilipungua na kufikia wastani wa asilimia 16.05 kutoka asilimia
16.37 Aprili 2020. Aidha, riba za amana ziliongezeka na kufikia asilimia 6.95
kutoka asilimia 6.69 Aprili 2020. Riba za amana za mwaka mmoja ziliongezeka na
kufikia asilimia 8.77 ikilinganishwa na asilimia 8.01 Aprili 2020. Hali hii
inafanya tofauti kati ya riba za mkopo na amana kwa mwaka mmoja (interest rate
spread) kupungua na kufikia asilimia 7.28 kutoka asilimia 8.36 Aprili 2020.
Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa sekta ya benki ili kuongeza kasi ya
kushuka kwa viwango vya riba za mikopo.
21. Mheshimiwa Spika, sekta ya benki imeendelea kuimarika ambapo uwiano wa mali inayoweza
kubadilishwa kwa muda mfupi kuwa fedha taslimu (Liquid Assets to Demand
Liabilities) ulikuwa ni asilimia 29.63 Machi 2021, ikiwa ni zaidi ya uwiano
wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20. Uwiano wa mikopo chechefu
umepungua na kufikia asilimia 9.36 Machi 2021 ikilinganishwa na asilimia 10.50
Machi 2020. Aidha, ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi ulifikia asilimia 4.8
Aprili 2021. Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi unaenda sanjari na utekelezaji
wa sera ya fedha inayolenga kuongeza ukwasi kwenye uchumi na utekelezaji wa
mpango wa Serikali wa kuboresha mazingira ya biashara nchini.
Athari za UVIKO - 19
22.
Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudi za kukabiliana na athari za
ugonjwa wa virusi vya korona (UVIKO-19), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliunda Kamati Maalum ya Wataalamu
kuchambua athari za ugonjwa huo na kushauri namna bora zaidi ya kukabiliana
nao. Kamati ilikamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa tarehe 17 Mei 2021
ambapo, pamoja na mambo mengine, Kamati ilibaini kuwa Tanzania kama zilivyo
nchi nyingine duniani imeathirika kiuchumi na kijamii kutokana na UVIKO-19 hasa
katika sekta muhimu zikiwemo afya, utalii, biashara, usafirishaji, sanaa na
burudani, ambazo zimesababisha kushuka kwa mapato yatokanayo na mauzo ya huduma
nje, akiba ya fedha za kigeni na kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi. Serikali
inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha shughuli za uchumi
zilizoathirika zinarejea katika hali ya kawaida kama ilivyokuwa kabla ya
mlipuko wa UVIKO-19.
23. Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 3 Mei 2021, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, alizungumza na Bi. Kristalina Georgieva - Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa nia ya kuimarisha mahusiano
katika masuala ya kiuchumi na kijamii likiwemo suala la mikakati ya kukabiliana
na athari za UVIKO-19. Kufuatia mazungumzo hayo, Wizara ya Fedha na Mipango
imeanza majadiliano na IMF ya mkopo wa dharura (Rapid Credit Facility - RCF)
wa dola za Marekani milioni 571. Mkopo huu ni wa masharti nafuu kwa ajili ya
kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazotokana na UVIKO-19.
III.
SERA ZA BAJETI KWA
MWAKA 2021/22
Shabaha za Uchumi Jumla
24. Mheshimiwa Spika, makadirio ya
mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2021/22, yameandaliwa kwa kuzingatia
misingi (assumptions) pamoja na shabaha mahsusi za uchumi jumla. Malengo na shabaha za uchumi jumla ni kama
ifuatavyo:
(i)
Kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato Halisi la Taifa kufikia asilimia 5.6 mwaka
2021 na kuendelea kukua kwa wastani wa asilimia 6.2 ifikapo mwaka 2023;
(ii) Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha
kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja kati ya wastani wa asilimia 3.0 – 5.0
kwa mwaka 2021/22;
(iii) Mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri)
kufikia asilimia 15.9 ya Pato la Taifa mwaka 2021/22;
(iv) Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.5 ya Pato la Taifa
mwaka 2021/22 kutoka matarajio ya asilimia 12.9 mwaka 2020/21;
(v)
Kuhakikisha kuwa nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) haizidi asilimia
3.0 kuendana na makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(vi) Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi
mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua
miezi minne (4.0); na
(vii) Kuhakikisha kuwa viashiria vya ustawi wa jamii
vinaimarika.
Sera na Mikakati ya Kuongeza Mapato
25. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Serikali itaendelea kuweka vipaumbele zaidi katika
ukusanyaji wa mapato ya ndani. Masuala muhimu ya kuzingatia ni pamoja na
kuimarisha na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuendelea kutekeleza
hatua zifuatazo:
(i)
Kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa kuweka mazingira
rafiki kwa mlipakodi kwa lengo la kuvutia uwekezaji, ukuaji wa biashara ndogo
na za kati ili kupanua wigo wa kodi;
(ii) Kuendelea kutekeleza mpango wa kuboresha mazingira ya
biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwianisha na kufuta au
kupunguza viwango vya kodi, tozo na ada kero;
(iii) Kuimarisha usimamizi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani
yakijumuisha mapato ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa kuhimiza matumizi
sahihi ya mifumo ya TEHAMA;
(iv) Kuendelea kuboresha Mfumo wa Serikali wa Kieletroniki wa
ukusanyaji wa mapato (GePG) na kuhakikisha taasisi zote za Serikali zinatumia
mfumo huo;
(v)
Kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji katika taasisi na Mashirika ya Umma ili
kuhakikisha kuwa gawio na michango stahiki inawasilishwa kwa wakati;
(vi) Kuimarisha usimamizi wa sheria za kodi ili kutatua
changamoto za ukwepaji kodi na kupunguza upotevu wa mapato;
(vii) Kuhamisha jukumu la uwekaji vinasaba kwenye mafuta ya
petroli kutoka kwa mkandarasi binafsi kwenda Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
ili kuhakiki ubora wa mafuta yanayoingizwa nchini na kudhibiti ukwepaji kodi
kutokana na uchakachuaji unaofanywa kwenye mafuta yanayopita hapa nchini; na
(viii) Kutoa kipaumbele katika utekelezaji wa mikakati na miradi
ya kuongeza mapato.
26.
Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizo za kuimarisha ukusanyaji
wa mapato ya ndani, Serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kuhamasisha ushiriki wa wawekezaji kwenye soko la ndani la fedha na kuorodhesha Hatifungani za Serikali katika Soko la
Hisa la Dar es Salaam. Aidha, Serikali itaendelea kutekeleza masuala
yaliyoainishwa katika Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (Development Cooperation Framework - DCF) ili kuwezesha upatikanaji wa misaada na mikopo ya masharti nafuu na
kukopa kwa utaratibu wa udhamini kutoka taasisi za udhamini wa mikopo (Export Credit Agencies
-ECA), ambayo masharti
yake yana unafuu.
Sera za Matumizi
27. Mheshimiwa Spika, Sera
za Matumizi katika mwaka 2020/21 zitajumuisha
yafuatayo:
(i)
Kuelekeza fedha kwenye maeneo ya
kipaumbele yatakayochochea ukuaji wa uchumi na kuhakikisha kuwa miradi
inayoendelea inapewa kipaumbele kabla ya miradi mipya;
(ii) Kuhakikisha
kuwa nakisi ya bajeti haizidi asilimia 3.0 ya Pato la Taifa kuendana na vigezo
vya Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(iii) Kudhibiti
uzalishaji na ulimbikizaji wa madeni;
(iv) Kuendeleza
nidhamu ya matumizi ya fedha za umma; na
(v)
Kuongeza matumizi ya TEHAMA katika
shughuli za Serikali ili kuongeza ufanisi ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa
wataalamu wa ndani kwenye eneo la usalama wa mifumo (systems security).
28. Mheshimiwa Spika, ili
kuendelea kuimarisha usimamizi wa fedha za umma kwa taasisi zinazotoza ada,
Serikali inaweka utaratibu mpya na endelevu wa kusimamia mapato na matumizi ya
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na
Wakala wa Meli Tanzania (TASAC). Hivyo, kuanzia mwaka 2021/22, mapato
yataendelea kukusanywa na taasisi hizo kupitia mfumo wa GePG na kuingizwa
kwenye akaunti za makusanyo (holding account) zilizopo Benki Kuu. Aidha,
taasisi hizi zitapatiwa fedha kulingana na bajeti iliyoidhinishwa na fedha
kutolewa kwenye akaunti ya makusanyo baada ya kupata ridhaa ya Mlipaji Mkuu wa
Serikali. Vilevile, Serikali itafanya ufuatiliaji wa matumizi ya taasisi hizi
kila robo mwaka.
29. Mheshimiwa Spika, Serikali inakusudia utaratibu wa utoaji fedha kwa
Taasisi za Uhifadhi (TANAPA, NCAA, TAWA) ili kuongeza ufanisi katika
utekelezaji wa majukumu yake. Katika kutekeleza azma hii Serikali itatoa fedha
za matumizi mengineyo kwa miezi miwili unapoanza mwaka wa fedha na kuendelea
kutoa kwa mwezi mmoja mmoja kila mwezi. Hatua hii itaziwezesha taasisi hizi
kuwa na akiba ya fedha za kukidhi mahitaji ya mwezi unaofuata kwa kipindi chote
cha mwaka.
Maeneo ya Kipaumbele kwa Mwaka
2021/22
30. Mheshimiwa Spika, Bajeti
ya Serikali kwa mwaka 2021/22 ni ya kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa
Maendeleo ya Watu”. Bajeti hii
itajielekeza katika utekelezaji wa vipaumbele vilivyoainishwa katika maeneo matano (5) ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22. Maeneo hayo ni: Kuchochea
uchumi shindani na shirikishi; kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na
utoaji huduma ili kuongeza thamani ya mazao ya kilimo; kukuza uwekezaji na
biashara; kuchochea maendeleo ya watu; na kuendeleza rasilimali watu.
31. Mheshimiwa Spika, ili kuwa na
uchumi shindani na shirikishi, Serikali itajielekeza katika kugharamia miradi
ambayo itajikita katika: Kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda na
kimataifa; kusimamia utulivu wa viashiria vya uchumi jumla; kuimarisha mazingira
ya biashara na uwekezaji; kuchochea uvumbuzi na uhawilishaji wa teknolojia
kutoka nje; na kuendeleza miundombinu na huduma za reli, barabara za kufungua
fursa za kiuchumi, kuunganisha nchi jirani, kupunguza msongamano mijini na
barabara za vijijini, madaraja, usafiri wa majini na angani, mageuzi ya TEHAMA
pamoja na kutekeleza mradi wa Tanzania ya Kidijitali, nishati, bandari na
viwanja vya ndege. Eneo hili limetengewa jumla ya shilingi trilioni 7.44
ikijumuisha shilingi trilioni 3.13 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
kielelezo.
32. Mheshimiwa Spika, miradi mingine ya
kielelezo itakayotekelezwa ni: Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL);
Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga ikijumuisha ujenzi wa reli ya
kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Mtwara hadi Mbamba
Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga; Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima
(Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Mradi wa Kuchakata Gesi Asilia kuwa Kimiminika
(LNG) – Lindi; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji - Ruhudji MW 358; Mradi wa Kufua
Umeme wa Maji - Rumakali MW 222; Uchimbaji wa madini ya Nickel; Ujenzi wa
Madaraja Makubwa na Barabara za Juu za Daraja la Kigongo - Busisi (Mwanza),
Tanzanite (Dar es Salaam) na Interchange ya Kamata (Dar es Salaam); Bandari ya
Uvuvi (Mbegani) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi; Kiwanda cha Sukari Mkulazi;
Utafutaji wa mafuta katika vitalu vya Eyasi Wembere na Mnazi Bay North;
Mradi wa Magadi Soda – Engaruka; Kuongeza Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na
Maalumu (Ujuzi wa Kati na Wabobezi) kwa Maendeleo ya Viwanda na Ustawi wa
Jamii; na kuendeleza Kanda Maalumu za Kiuchumi.
33. Mheshimiwa Spika, katika eneo la
kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma, msukumo utawekwa
kwenye miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo
na uvuvi. Katika eneo hili, kipaumbele ni pamoja na: Kujenga na kukarabati
miundombinu ya umwagiliaji na uhifadhi wa mazao ya kilimo; kuimarisha vituo vya
utafiti na huduma za ugani; kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na
uvuvi; kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi; kuboresha
huduma za uhimilishaji mifugo; na kujenga machinjio ya kisasa na minada ya
mifugo.
34. Mheshimiwa Spika, Serikali itaweka mkazo kwenye ujenzi wa viwanda vya
kuongeza thamani ya madini pamoja na kuzalisha bidhaa zitakazotumia malighafi
na rasilimali zinazopatikana nchini. Aidha, Bajeti hii itajielekeza katika
kugharamia miradi na programu inayolenga kuboresha huduma za utalii, fedha na
bima pamoja na kuendeleza viwanda vya uzalishaji wa dawa muhimu na vifaa tiba.
Jumla ya shilingi trilioni 1.38 zimetengwa kugharamia utekelezaji wa miradi
katika eneo hili.
35. Mheshimiwa Spika, katika eneo la
kukuza uwekezaji na biashara, Serikali itagharamia programu zitakazoimarisha
masoko ya ndani na kutumia fursa za masoko ya kikanda na kimataifa katika
kukuza biashara. Masoko yanayolengwa ni yale yatakayotoa fursa kwa bidhaa
zinazozalishwa nchini, ikiwemo bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, mifugo,
uvuvi na misitu. Vilevile, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya
biashara na uwekezaji ikiwemo kuendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Biashara
na Uwekezaji (Blueprint). Eneo hili limetengewa jumla ya shilingi
bilioni 31.6.
36.
Mheshimiwa Spika, ili kuchochea maendeleo ya watu, miradi itakayotekelezwa
italenga kuboresha maisha ya watu kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za jamii
ikiwemo elimu na mafunzo kwa ujumla, afya na ustawi wa jamii, huduma za maji na
usafi wa mazingira na kinga ya jamii ikijumuisha Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini kupitia TASAF. Aidha, Serikali itaendelea kupanga, kupima na
kumilikisha ardhi mijini na vijijini, kusimamia na kuendeleza rasilimali za
maji; na kuendelea na utekelezaji wa programu za kulinda mazingira na kuhimili
mabadiliko ya tabianchi. Jumla ya shilingi trilioni 4.43 zimetengwa.
37.
Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuendeleza rasilimali watu, Serikali
itagharamia programu inayolenga kuendeleza maarifa na ujuzi wa rasimali watu
katika ngazi zote za elimu ikiwemo kuweka mazingira wezeshi kwa vijana
kujiajiri. Aidha, Serikali itaendelea kuboresha viwango vya utoaji wa elimu ya
ufundi na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na ujuzi adimu kwa lengo la kuongeza
tija na ushindani wa wananchi katika kutumia rasimali zilizopo nchini ili
kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Jumla ya shilingi bilioni 50.5
zimetengwa.
38. Mheshimiwa Spika, hotuba yangu
niliyowasilisha leo asubuhi ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2020 na Mpango
wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 imeainisha kwa kina maeneo ya kipaumbele
ambayo Serikali itayatekeleza kupitia Bajeti ya mwaka 2021/22.
39. Mheshimiwa Spika, pamoja na miradi ya kielelezo, Serikali itatekeleza miradi
mingine ya uboreshaji wa miundombinu ambayo itagharamiwa na mikopo yenye
masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia. Miradi hiyo ni Mradi wa Kuendeleza Jiji
la Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) wa kukabiliana na mafuriko kwenye
Bonde la Mto Msimbazi utakaogharimu dola za Marekani milioni 120. Mradi huu
utahusisha ujenzi wa daraja katika eneo la Jangwani, na upanuzi na ujenzi wa
kingo za mto Msimbazi. Mradi wa pili unahusisha uboreshaji wa barabara za kukuza
fursa shirikishi za kijamii na kiuchumi ambapo Benki ya Dunia itatoa dola za
Marekani milioni 300 na mchango wa Serikali ni dola za Marekani milioni 50.
Mradi huu unalenga kuboresha barabara za vijijini katika maeneo yenye tija
kubwa ya uzalishaji wa mazao ya kilimo.
40. Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Serikali imeanza mazungumzo na Benki ya Dunia
kupitia dirisha la International Development Association (IDA) kwa ajili
ya mradi wa uboreshaji miundombinu katika Majiji na Miji 45. Utekelezaji wa
mradi huu utaanza katika mzunguko wa 20 (IDA 20) unaotegemewa kuanza Julai 2022
na utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 500. Mradi utahusisha ujenzi
wa miundombinu ya msingi ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa
lengo la kukuza uchumi wa miji husika.
Maeneo Mengine Muhimu
Maandalizi ya
Sensa ya Watu na Makazi Mwaka 2022
41.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajiandaa kufanya Sensa ya
Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu SURA 351. Kama mojawapo ya maandalizi ya utekelezaji wa Sensa ya
Mwaka 2022 Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa upande wa Tanzania Bara na Ofisi ya
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar imekamilisha kuandaa Kitabu cha Mkakati wa
Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka, 2022. Kitabu hiki kinaainisha namna ya usimamizi na
utekelezaji wa zoezi zima la Sensa, gharama ya kufanya Sensa pamoja na muundo
wa Sensa utakavyokuwa katika ngazi zote za kiutawala.
42. Mheshimiwa
Spika, jumla ya
shilingi bilioni 328.2 zinatarajiwa kutumika kugharamia sensa ya mwaka 2022. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Sensa nchini, Sensa
ya Mwaka 2022 itatumia teknolojia ya vishikwambi (tablets)
katika utengaji wa maeneo ya kijiografia na ukusanyaji wa takwimu uwandani.
Matumizi ya teknolojia hii yana manufaa makubwa, hasa katika kupunguza gharama
na muda wa kukusanya na kuchakata takwimu, hali inayowezesha kutoa matokeo ya
Sensa ndani ya muda mfupi.
43. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ni jukumu la kila mtu, natoa
wito kwa kamati zote za Sensa, Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote, Waheshimiwa
Wabunge pamoja na wananchi wote kwa
ujumla kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika maandalizi ya Sensa na
wajitokeze wote siku ya kuhesabu watu. Lengo ni kuhakikisha Watu waliolala
nchini usiku wa kuamkia siku ya Sensa (usiku wa sensa) wanahesabiwa na
kuchukuliwa taarifa zao za kiuchumi, kijamii, mazingira na makazi wanayoishi na
mengine mengi kwa ajili ya kupanga mipango endelevu ya maendeleo ya wananchi.
Maslahi ya Wafanyakazi
44. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa watumishi wa umma na wa sekta
binafsi katika kukuza Pato la Taifa. Kwa kutambua hilo, Serikali itachukua
hatua mbalimbali za kuboresha maslahi ya wafanyakazi kama ifuatavyo:
(i)
Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira (PAYE)
kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8. Hatua hii ni mwendelezo wa juhudi za
Serikali za kupunguza mzigo wa kodi kwa wafanyakazi, ambapo kiwango hicho kimepunguzwa
kutoka asilimia 11 mwaka 2015/16 hadi asilimia 8 itakayoanza kutekezwa mwaka
2021/22;
(ii) Kufuta tozo ya asilimia 6 iliyokuwa ikitozwa kwa ajili ya
kulinda thamani ya mkopo wa elimu ya juu (Value Retention Fee) kwa wanufaika;
na
(iii) Kutenga jumla ya shilingi bilioni 449 kwa ajili ya
kuwapandisha vyeo watumishi 92,619.
Maslahi ya Madiwani,
Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata
46. Mheshimiwa Spika, napendekeza kuanzia
mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za Waheshimiwa
Madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa Halmashauri zote zenye uwezo
mdogo kimapato. Halmashauri 16 zenye uwezo mkubwa wa kimapato (Daraja A)
zitaendelea kutumia mapato yake ya ndani kulipa posho za Madiwani kupitia kwenye
akaunti zao.
47. Mheshimiwa Spika, Maafisa Tarafa ni viunganishi muhimu wa ngazi za kata na Wilaya zetu ambapo
wengi wao hufanya kazi nzuri sana ya kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya
Serikali katika maeneo yao. Kwa kutambua umuhimu wao, Serikali ya CCM
iliwapatia pikipiki viongozi hawa ili waweze kufanya kazi zao vizuri. Hata
hivyo, wengi wao wanashindwa kugharamia ununuzi wa mafuta na matengenezo ya
vitendea kazi hivi na kulazimika kuwachangisha wananchi na hata wengine kuomba
msaada kwa wadau mbalimbali. Hali hii inapunguza sana ufanisi katika Tarafa
zetu. Kupitia hotuba hii, napenda niwajulishe Maafisa Tarafa wote nchini kuwa
MAMA YETU amesikia kilio chenu. Hivyo, napendekeza
kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho ya shilingi 100,000/= kwa
mwezi kwa kila Afisa Tarafa ili waweze kumudu gharama za mafuta na matengenezo
ya pikipiki.
48. Mheshimiwa Spika, Watendaji Kata ndio wasimamizi wa kazi za sekta zote na
ni watendaji wakuu kwenye kata. Wengi wao wanafanya kazi katika mazingira
magumu ili kufanikisha shughuli za maendeleo katika kata zetu ikiwemo kusimamia
ukusanyaji wa mapato na masuala ya usalama. Idadi kubwa ya watendaji hawa
hutumia mishahara yao kufanya kazi mbalimbali ikiwemo ufutiliaji wa mapato ya
Serikali kwa kukodi pikipiki ili kufanikisha shughuli zilizopo. Kwa ujumla wanafanya kazi nzuri sana ya kusimamia
shughuli za maendeleo kwenye kata zetu. Jambo hili limeongelewa kwa hisia kali
sana na Mheshimiwa Rose Busiga, Mbunge wa Viti Maalum (Geita), ambaye ni
mtendaji wa kata mstaafu na kuungwa mkono na wabunge wengi hapa bungeni.
Waheshimiwa wabunge, MAMA YETU amesikia kilio hiki na kutuelekeza kulitafutia
ufumbuzi suala hili. Hivyo, napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali kuanza
kulipa posho ya shilingi 100,000/= kwa mwezi kwa kila Mtendaji Kata kupitia
mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyokuwa yakitumika kulipa madiwani.
Madeni ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
49. Mheshimiwa Spika, wastaafu wetu walilitumikia Taifa hili kwa uzalendo,
uadilifu na bidii kubwa sana. Hatuwezi kuhesabu mafanikio ya nchi yetu bila
kutaja mchango wa wazee hawa. Kumekuwepo na changamoto za muda mrefu za ulipaji
wa mafao yao kutokana na ufanisi mdogo wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika
kuhudumia wastaafu wetu. Hali hiyo kwenye mifuko yetu imechangiwa, pamoja na
mambo mengine, na uwepo wa madeni ambayo mifuko inaidai Serikali na hivyo
kusababisha wastaafu wetu kukosa au kusubiri kwa muda mrefu ili kulipwa mafao
yao. Jambo hili pia limejadiliwa kwa hisia kali na Waheshimiwa Wabunge hapa
bungeni. Wazee wetu hawa hupata shida sana, ambapo baadhi yao hufadhiliwa
malazi kwa kulala misikitini na makanisani na wengine hutegemea wahisani
kuhudumia familia zao kinyume na mchango walioutoa katika ujenzi wa nchi hii.
MAMA YETU amesikia kilio cha wazee hawa na kutuelekeza Wizara ya Fedha na
Mipango kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kukamilisha zoezi la kitaalamu ili
kujua hali halisi ya madeni na namna bora ya kulipa madeni hayo.
50. Mheshimiwa Spika, napendekeza kulipa madeni yanayodaiwa na mifuko kwa
kutenga fedha kwenye bajeti na kutumia utaratibu wa kutoa hatifungani maalum
isiyo taslimu (Non-cash Special Bond) zitakazoiva kwa nyakati tofauti
kuanzia miaka miwili hadi 25. Utaratibu wa hatifungani una faida mbalimbali
zikiwemo: kuipa Serikali nafasi ya kibajeti ya kuendelea kutekeleza miradi
mingine ya maendeleo; kuiwezesha Serikali kuyatambua madeni hayo kwenye
kanzidata ya madeni; na kuzuia madeni hayo kuendelea kuongezeka kulingana na
tathmini ya thamani ya madai (actuarial valuation). Aidha, utaratibu huo
utaboresha mizania ya hesabu na mtiririko wa mapato yanayotokana na riba ya
hatifungani hizo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Hatua hii inakwenda kumaliza
kabisa tatizo hilo la wazee wetu kudai haki yao kwa damu na machozi yaliyodumu
kwa muda mrefu.
52.
Mheshimiwa Spika, katika jeshi la polisi kwa askari wapiganaji, kuna
utaratibu wa wapiganaji kufanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi kwa miaka 12
kabla hawajapata ajira za kudumu. Jambo hili huwasababishia wapatapo mkataba wa
kudumu wawe wamechelewa kwa miaka 12 ikilinganishwa na mtumishi mwingine aliyeingia
pamoja kazini katika idara nyingine. Jambo hili linamadhara hasi katika itifaki
ya utumishi na mafao ya mpiganaji anapostaafu. Hiki kimekuwa kilio cha muda
mrefu cha askari wa Jeshi la Polisi. Kutokana na changamoto hiyo, MAMA YETU
amesikia kilio cha askari hao na alituelekeza tukae na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi ili kutafuta suluhisho la jambo hili. Napendekeza kuanzia mwaka 2021/22
askari wa Jeshi la Polisi wataingia mkataba wa kipindi cha miaka 6 na kuingia
katika ajira ya kudumu.
Kurahisisha Kasi ya Utekelezaji wa Miradi
53.
Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi na ufanisi katika
utekelezaji wa bajeti ya Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango itafanya
mabadiliko katika Kanuni ya 21 ya Sheria ya Bajeti, SURA 439 ili kuondoa
changamoto iliyopo ya fedha ambazo hazijatumika hadi tarehe 30 Juni kila mwaka
kurejeshwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali. Mabadiliko hayo yatatoa fursa kwa Maafisa Masuuli kuwasilisha taarifa ya fedha kuvuka mwaka hadi tarehe 30 Juni kwa
Mlipaji Mkuu wa Serikali badala ya siku 15 kabla ya mwaka wa fedha kumalizika.
Fedha hizo zitawekwa kwenye Akaunti ya Amana kwa ajili ya utekelezaji wa
shughuli ambazo hazijakamilika wakati wa utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya
mwaka wa fedha husika. Kwa msingi huo, kuanzia sasa hakutakuwa na fedha zenye
miadi zitakazorejeshwa Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ifikapo tarehe 30 Juni
ya kila mwaka wa fedha isipokuwa pale ambapo Maafisa Masuuli wamekiuka masharti
ya Sheria ya Bajeti, SURA 439 na Sheria ya Fedha za Umma, SURA 348.
Kodi ya Majengo
54. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na changamoto kubwa katika ukusanyaji wa kodi ya majengo, hali
iliyosababisha Serikali kubadili njia za ukusanyaji mara kwa mara. Kabla ya
mwaka 2017/18, Serikali za Mitaa zilikuwa na jukumu la kukusanya mapato hayo
lakini hazikufanya vizuri. Kuanzia mwaka 2017/18, Serikali ilitumia Mamlaka ya
Mapato kukusanya kodi hiyo, ambapo pia haikufanya vizuri. Ukusanyaji wa kodi
hii kwa kutumia Serikali za Mitaa au TRA umekuwa ukitumia njia za kizamani
ambazo zinahusisha watu kusafiri, kupanga foleni na kukusanya fedha taslimu (cash).
Utaratibu huu unatumia gharama kubwa, muda na ni hatarishi kwa mapato. Katika
kuhakikisha kodi hii inafikia malengo, Serikali imeandaa utaratibu mzuri wa
kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi ya majengo.
Tozo ya Wajasiliamali
55. Mheshimiwa Spika, wafanyabiashara na watoa huduma wadogo nchini
wameendelea kutambulika kupitia vitambulisho vya wajasiriamali. Tangu kuanza
kwa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara na watoa huduma wadogo
nchini, jumla ya vitambulisho 2,335,711 vimegawiwa ambavyo vimewezesha
kukusanya jumla ya shilingi bilioni 46.71. Lengo ni kuendelea kuwatambua
wafanyabiashara wadogo na kuwawekea mazingira rafiki ya ufanyaji biashara.
Katika mwaka 2020/21, Serikali imefanya maboresho ya vitambulisho hivyo kwa
kuweka picha na jina la mjasiriamali ili kuongeza udhibiti na kufungua fursa
kwa wajasiriamali kuweza kutumia vitambulisho hivyo kupata huduma za kibenki na
bima ya afya. Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea na uratibu wa kugawa
vitambulisho hivi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo ndiyo
yenye mfumo wa kusajili wafanyabiashara hao, kuchapisha vitambulisho na
kuwapatia Halmashauri husika kwa ajili ya kugawa.
IV. MABORESHO YA
MFUMO WA KODI, ADA NA TOZO MBALIMBALI
56.
Mheshimiwa
Spika, napenda sasa
kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu mapendekezo ya kufanya marekebisho
ya mfumo wa kodi, ikiwemo baadhi ya viwango
vya kodi, tozo na ada zinazotozwa
chini ya Sheria mbalimbali na kurekebisha taratibu za ukusanyaji na usimamiaji
wa mapato ya Serikali. Marekebisho haya yamezingatia dhamira ya Serikali ya
kurejesha ukuaji wa uchumi katika hali ya kawaida baada ya athari zilizotokana
na UVIKO-19 sambamba na kuendelea kuwa na mfumo wa kodi ambao ni tulivu na wa
kutabirika ili kuvutia uwekezaji kutoka ndani na nje. Vile vile, marekebisho
yanalenga kuchochea kasi ya ukuaji wa
uchumi hususan katika sekta ya
kilimo na viwanda, kuongeza kipato
kwa waajiriwa na kuongeza mapato ya Serikali. Aidha, Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha
Mazingira ya Kufanya Biashara (BluePrint) kwa kuwianisha tozo na ada mbalimbali
zinazotozwa na Wizara na Mamlaka za Udhibiti kwa lengo la kupunguza na
kurahisisha ulipaji wake au kuzifuta baadhi ya tozo na ada hizi. Marekebisho
yanayopendekezwa yanahusu Sheria zifuatazo:
(a)
Sheria ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani, SURA 148;
(b) Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;
(c) Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;
(d) Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004;
(e) Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438;
(f) Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa,
SURA 290;
(g) Sheria ya Kodi ya Majengo, SURA 289;
(h) Sheria ya Ardhi, SURA 113;
(i) Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189;
(j) Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Stadi, SURA 82;
(k) Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, SURA
41;
(l) Sheria ya Ukaguzi wa Umma, SURA 418;
(m) Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada,
SURA 134
(n) Sheria ya Usajili wa Magari, SURA 124;
(o) Sheria ya Usalama Barabarani, SURA
168;
(p) Sheria ya Raia wa Kigeni (Uratibu wa
Ajira) Na. 1 ya mwaka 2015;
(q) Marekebisho ya Ada na Tozo mbalimbali
zinazotozwa na Wizara, Mikoa Wakala, Mamlaka za Udhibiti na Idara
zinazojitegemea;
(r) Marekebisho madogo madogo katika
baadhi ya Sheria za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali;
(s)
Kuendelea
na utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara (Blueprint)
kwa kurekebisha Ada na Tozo mbalimbali;
(t) Sheria ya Ushuru wa Barabara na
Mafuta, SURA 220;
(u)
Sheria ya Petroli, SURA
392; na
(v)
Sheria
ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, SURA 306.
A. Sheria ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani, SURA 148
57. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani,
SURA 148 kama ifuatavyo:
(i)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwenye vyumba vya ubaridi (cold rooms) vinavyotambuliwa kwa
H.S Code 9406.10.10 na 9406.9010. Lengo la msamaha huu ni kuwapunguzia gharama
wazalishaji wa mbogamboga na maua nchini ili kuchochea kilimo cha kisasa;
(ii)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwenye madini (precious metals) na makinikia yatakayoingizwa
nchini kwa ajili ya kuchenjuliwa, kuongezewa thamani na kuuzwa kwenye masoko ya
madini yanayotambulika nchini. Lengo la pendekezo hili ni kuviwezesha viwanda
vya uchenjuaji vilivyoanzishwa nchini kupata malighafi ya kutosha kwa ajili ya
uchakataji na hatimaye kuongeza ajira na mapato ya Serikali;
(iii)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwenye huduma za bima ya mifugo. Lengo la marekebisho haya ni
kuchochea shughuli za ufugaji nchini;
(iv)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwenye bidhaa na huduma zitakazoingizwa au kununuliwa hapa nchini
kwa ajili ya kutekeleza mradi wa mafuta ghafi (EACOP). Lengo la marekebisho
haya ni kutoa unafuu wa kodi katika utekelezaji wa miradi tajwa;
(v)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwenye mafuta ghafi yanayotambulika kwa H.S Code 2709.00.00 kwa
lengo la kutoa unafuu kwa mlaji ikiwemo Kampuni ya uendeshaji wa bomba la
mafuta (EACOP);
(vi)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwenye Nyasi Bandia zinazotambulika kwa HS Code 5703.30.00 na
5703.20.00 kwa ajili ya Viwanja vya Mpira vilivyoko kwenye Majiji. Msamaha huo
utahusisha ridhaa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania. Lengo la hatua hii ni kuendeleza michezo na
kukuza vipaji nchini;
(vii)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye kadi za
kutengeneza vitambulisho vya taifa zinazotambulika kwa H.S Code 3921.11.90.00
na malighafi nyingine za kutengeneza kadi hizo zinazotambulika kwa H.S Code
3921.11.90.00 zitakazoingizwa nchini na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA). Lengo la pendekezo hili ni kupunguza gharama za kutengeneza
Vitambulisho vya Taifa na kuharakisha upatikanaji wake;
(viii)
Kumekwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za misaada
kwenye miradi ya maendeleo kwa hitaji la
kisheria la kusubiri idhini ya Baraza la Mawaziri likae ili kuidhinisha misamaha. Napendekeza Kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani
kwa Taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s), kwenye bidhaa na huduma
zitakazotumika kwenye miradi inayotekelezwa na taasisi husika. Aidha, taasisi
zitakazonufaika na msamaha huo ni zile ambazo zina mikataba na Serikali yenye
kipengele kinachotoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani;
(ix)
Sekta ya mawasiliano imekuwa ikikua vizuri na kuwa kiungo
muhimu cha kuongeza wigo wa wananchi ambao wako kwenye ulimwengu wa kidijitali
na kwenye sekta ya fedha (Financial Inclusion). Napendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye
simu janja za mkononi (smart phones) HS Code 8517.12.00, vishikwambi (Tablets)
HS Code 8471.30.00 au 8517.12.00 na modemu (modems) HS Code
8517.62.00 au 8517.69.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya huduma
za mawasiliano ili kufikia lengo la asilimia 80 ya watumiaji wa intaneti
ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 46 iliyopo sasa;
(x)
Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye
mikebe inayotumika kuhifadhia maziwa inayotambuliwa kwa H.S Code 7310.29.20
ambayo kwa sasa haitumiki kwa ajili ya kazi hiyo na badala yake napendekeza
kutoa msamaha wa kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mikebe ya kubebea maziwa
inayotambulika kwa H.S Code 7310.29.90, 7310.10.00 na 7612.90.90. Lengo la
Pendekezo hili ni kuwapunguzia gharama wazalishaji na kuchochea ukuaji wa sekta
ya maziwa nchini;
(xi)
Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye taa
zinazotumia umeme wa jua zinazotambulika kwa H.S. Code 85.13 na 94.05. Lengo la
pendekezo hili ni kuwianisha msamaha huu sambamba na msamaha unaotolewa chini
ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ambayo inasamehe Kodi kwenye vifaa vinavyotumika
kuzalisha nishati ya umeme wa jua pekee na kurahisisha usimamizi wake. Aidha,
pendekezo hili linalenga kuweka usawa katika ulipaji kodi kwa watumiaji wa taa
zinazotumia nishati za aina zote;
(xii)
Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha
asilimia sifuri kwenye huduma ya usafirishaji na huduma zinazohusiana na
usafirishaji wa mafuta ghafi kupitia bomba linalojengwa kwa pamoja baina ya
Serikali ya Tanzania na Uganda (EACOP). Lengo la pendekezo hili ni kuwezesha
huduma tajwa kutekelezwa bila kodi sanjari na uzoefu wa kimataifa kwa bidhaa
zilizopita hapa kwenda nchi jirani au ng’ambo;
(xiii)Kuzitambua bidhaa za mtaji zilizomo kwenye
Sura ya 84, 85 na 90 ya Kitabu cha Ushuru wa Pamoja wa Forodha wa Afrika
Mashariki kuwa bidhaa za mtaji zitakazostahili kupata kivutio cha ahirisho la
malipo ya VAT. Lengo la pendekezo hili ni kuwianisha maana ya bidhaa za mtaji
kwenye Sheria za kodi na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali kwenye
kifungu tajwa;
(xiv)
Kubadilisha utaratibu wa kutoa msamaha kwenye miradi ya
Serikali inayogharamiwa na fedha za serikali na fedha za wafadhili ambapo
mnufaika wa msamaha huo atawasilisha maombi kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania badala ya utaratibu wa kuwasilisha kwa Waziri wa Fedha kwa
ajili ya kupata ridhaa na kutoa Tangazo la Serikali (GN) kwa kila mradi.
Utaratibu huu utarahisisha na kuharakisha utoaji wa misamaha badala ya
utaratibu wa sasa kutokana na TRA kuwa na ofisi kwa kila mkoa nchini kote ambazo
zinaweza kupokea, kuchambua na kusimamia matumizi sahihi ya misamaha; na
(xv)
Kuhusu Zanzibar, Napendekeza kufanya marekebisho ya
Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kurudisha utaratibu wa kurejesha VAT
kwa bidhaa zinazonunuliwa Tanzania Bara na kutumika Tanzania Zanzibar. Hii
inatokana na mfumo wa kutoza VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri kwa bidhaa za
viwandani pekee kutowanufaisha wafanyabiashara wa Zanzibar wanaonunua bidhaa na
kutozwa VAT Tanzania Bara na kutozwa tena VAT bidhaa hizo zinapopelekwa Zanzibar.
Aidha, inapendekezwa marejesho ya VAT yatakayofanyika kwa bidhaa zinazotoka
Tanzania Bara kwenda Zanzibar yafanyike pia kwa bidhaa zitakazotoka Zanzibar
kwenda Tanzania Bara sambamba na marekebisho ya vifungu husika vya Sheria za
VAT kwa pande zote mbili za muungano. Ili kuwa na ufanisi wa marejesho,
maboresho ya mifumo yatafanyika ili isomane baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kutokana na utaratibu huu, kiwango cha asilimia sifuri ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani kilichokuwa kinatozwa bidhaa hizo kitasitishwa.
Hatua zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla
zinatarajiwa kupunguza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni
55,499.97.
B. Sheria ya Kodi ya Mapato,
SURA 332
58. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya
Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo:
(i)
Kupunguza kiwango cha chini
cha kutoza Kodi ya Mapato yanayohusiana na ajira kutoka asilimia 9 hadi
asilimia 8 kama ilivyobainishwa katika Jedwali Na. 1A na 1B.
Hatua hii
inachukuliwa ikiwa ni dhamira ya Serikali ya muda mrefu kuwapunguzia
mzigo wa Kodi wafanyakazi. Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato kwa shilingi
milioni 14,178.06;
(ii)
Kutoa msamaha wa Kodi ya
Mapato kwenye hatifungani za Serikali. Sheria ya Kodi ya Mapato ilisamehe Kodi
ya Mapato kwenye hatifungani kwa mwaka 2002/03 pekee. Lengo la hatua hii ni
kuhakikisha soko la ndani la hatifungani linaendelea kusaidia kugharamia miradi
ya Serikali;
(iii)
Kumekuwepo na ukiritimba katika kupokea fedha za kutoka
kwa nchi wahisani zinazokwenda kutekeleza Miradi ya maendeleo. Napendekeza
Kurejesha utaratibu wa Mamlaka ya Waziri mwenye dhamana ya Fedha kutoa msamaha
kwa kutoa tangazo la Serikali (GN) bila sharti la kupata ridhaa ya Baraza la
Mawaziri kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za wafadhili kupitia mikataba iliyoingiwa baina ya nchi hizo na Serikali yenye kifungu
kinachoruhusu msamaha wa kodi ya mapato. Lengo la marekebisho haya ni
kuharakisha utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa kwa misaada na mikopo yenye
gharama nafuu ambayo utekelezaji wake umekuwa ukichelewa kusubiri ridhaa ya
Baraza la Mawaziri;
(iv)
Kutoza Kodi ya Zuio kwa kiwango cha asilimia mbili (2)
kwenye malipo yanayohusisha mauzo ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi
yanapouzwa kwenye kampuni na mashirika yote yanayojihusisha na usindikaji na
ununuzi wa mazao. Kwa sasa, Taasisi za
Serikali pekee kama vile (Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ndizo
zinakata kodi hiyo kwa kiwango cha asilimia mbili (2). Aidha, pendekezo hili
halitahusisha wakulima wadogo na wale wanaouza mazao yao kwenye masoko ya msingi
(AMCOS) na kwenye magulio. Lengo la pendekezo hili ni kuweka usawa katika
utozaji wa kodi kwa Kampuni zote zinazojishughulisha na mazao ya Kilimo, mifugo
na uvuvi. Pendekezo hili linatarajiwa kuongeza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni
43,954.2;
(v)
Kufanya maboresho ya Sheria ya Kodi ya Mapato ili
kuwezesha ukokotoaji wa gharama za uchakavu kwa kiwango maalum cha asimilia
tano (5) kwenye gharama za mali za ujenzi wa bomba la mafuta (EACOP). Lengo la
pendekezo hili ni kuwianisha gharama za uchakavu na muda wa matumizi wa bomba
husika kwa kuzingatia masharti ya mkataba uliosainiwa baina ya Serikali za
Uganda na Tanzania;
(vi)
Kuweka utaratibu maalum wa utozaji kodi kwa wachimbaji
wadogo wa madini wenye mauzo ghafi yasiyozidi shilingi milioni 100 kwa mwaka
kama ifuatavyo: -
(a) Kutoza kodi wachimbaji wadogo wa madini kwa
kiwango mfuto cha asilimia tatu (3) kwenye thamani ya mauzo ya madini pindi
yanapopatikana;
(b) Kuweka muda wa ulipaji kodi kuwa ni wakati
wanapouza madini na kulipa mrabaha kwenye Tume ya Madini au maeneo maalum
yaliyoanzishwa chini ya sheria ya madini;
(c) Kuweka wajibu kwa mchimbaji mdogo wa madini
kama mwajiri wa kukata kodi ya mapato ya ajira kutoka kwa wafanyakazi wake pale
tu madini yatakapokuwa yamepatikana na kuuzwa katika masoko ya madini;
(d) Kuweka muda maalum wa kulipa kodi ya zuio ya
ajira kuwa ni wakati mchimbaji mdogo anapouza madini na kulipa mrabaha katika
masoko ya madini au vituo vingine vya uuzaji na ununuzi wa madini
vinayotambuliwa na Tume ya Madini; na
(e) Kuweka kiwango cha kodi cha mapato ya ajira
(PAYE) cha asilimia 0.6 ya thamani ya mauzo ya madini ambayo italipwa na
mwajiri (mchimbaji mdogo wa madini) kwa niaba ya wafanyakazi wake.
Lengo la mapendekezo haya ni kurahisisha utozaji na
ulipaji wa kodi kutoka kwa wachimbaji wadogo wa sekta ya madini ili kuongeza
mchango wa kodi ya mapato kutoka kwenye sekta hiyo. Hatua hizi kwa pamoja
zinatarajia kuongeza mapato ya
Serikali shillingi milioni 29,776.14
C. Sheria ya Ushuru wa
Bidhaa, SURA 147
59.
Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa kifungu cha 124(2) cha Sheria
ya Ushuru wa Bidhaa, marekebisho ya viwango maalumu vya ushuru wa bidhaa (specific duty rates) kwa bidhaa zote zisizo za petroli yanaweza kufanyika kila
mwaka ili kuvihuisha na mfumuko wa bei na viashiria vingine vya uchumi jumla.
Hata hivyo, kutokana na biashara za bidhaa hizi kuzorota kutokana na athari za
kiuchumi zilizosababishwa na ugonjwa wa UVIKO-19, napendekeza kutofanya mabadiliko ya viwango maalumu vya ushuru wa
bidhaa kwa bidhaa zote zisizo za petroli isipokuwa vinywaji vikali na bia
zitakazotengenezwa kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini.
60. Mheshimiwa Spika, napendekeza pia kufanya marekebisho ya
Ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zifuatazo:
(i)
Kupunguza Ushuru wa Bidhaa kwenye bia zinazotengenezwa
kwa kutumia shayiri iliyozalishwa hapa nchini kutoka shilingi 765 kwa lita za
sasa hadi shilingi 620 kwa lita. Lengo la mapendekezo haya ni kuchochea kilimo cha shayiri hapa nchini;
(ii)
Kuanza kutoza Ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye
nyuzi na kamba za plastiki (synthetic fibres) zinazoingizwa kutoka nje
ya nchi au kuzalishwa hapa nchini zinazotambuliwa kwa heading 55.11 na 56.07 isipokuwa zile zinazotumika kwenye Uvuvi (HS
Code 5607.50.00). Lengo la marekebisho haya ni kulinda mazingira na kuchochea
uzalishaji na matumizi ya bidhaa za katani. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa
shilingi milioni 2,644; na
(iii)
Kuanzisha tozo ya ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha
asilimia 10 kwenye pikipiki zilizotumika kwa zaidi ya miaka 3 zinazoingizwa
nchini zinazotambuliwa kwa HS Code 8711. Lengo la marekebisho haya ni kudhibiti
uingizaji wa pikipiki chakavu na kulinda mazingira. Hatua hii inatarajiwa kuongeza ya mapato ya Serikali kwa
shilingi milioni 263.7.
Hatua za kutoza Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zisizo za
petroli kwa ujumla wake zinatarajiwa
kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 2,907.7.
D. Sheria ya Usimamizi
wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004
61.
Mheshimiwa Spika, Kikao cha Mawaziri wa Fedha wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Maandalizi ya Bajeti (EAC Pre-Budget
Consultative Meeting of Ministers of Finance) kilichofanyika tarehe 7 Mei
2021 mjini Arusha, kilipendekeza kufanya marekebisho ya Viwango vya Pamoja vya
Ushuru wa Forodha (EAC-Common External Tariff) na Sheria ya Usimamizi wa
Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004)
kwa mwaka wa fedha 2021/22. Mapendekezo hayo yanalenga katika Kuboresha Maisha
ya Watu Kupitia Maendeleo ya Viwanda na Kutengeneza Ajira kwa ajili ya Ustawi
wa Pamoja wa Watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
62. Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya
Mawaziri wa Fedha ya kufanya marekebisho kwenye Viwango vya Pamoja vya Ushuru
wa Forodha yanahusisha hatua mpya na zinazoendelea ambazo zimekuwa
zikitekelezwa katika Mwaka wa Fedha 2020/21. Hatua hizo ni kama zifuatazo:
(i)
Mapendekezo ya hatua mpya
za Viwango vya Ushuru wa Forodha ni kama ifuatavyo:
(a)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye mabasi ya abiria yanayotambulika kwa HS
Codes 8702.10.99 na 8702.20.99 yanayoingizwa nchini kwa ajili ya mradi wa
mwendokasi. Hatua hii inalenga kupunguza gharama za uingizaji
wa mabasi hayo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi;
(b)
Kuongeza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 10 hadi
asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyuzi za pamba (cotton yarn) zinazotambulika
kwa Headings 52.05, 52.06 na 52.07. Lengo la
hatua ni kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo na kuongeza thamani ya zao
la pamba (value addition) nchini;
(c)
Kuongeza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 10 hadi
asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye matairi mapya ya pikipiki (new pneumatic
tyres of rubber) yanayotambulika kwa HS Code 4011.40.00. Lengo la
hatua ni kuongea
mapato ya Serikali kwa kuwa matairi haya ni bidhaa zilizokamilika kwa ajili ya
mtumiaji;
(d)
Kuongeza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye siagi ya karanga (peanut butter)
inayotambulika kwa HS Code 2008.11.00. Lengo la
hatua ni kulinda wazalishaji wa bidhaa hiyo nchini;
(e)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 10 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye nyaya (wire of other alloy steel)
zinazotambulika kwa HS Codes 7229.20.00 na 7229.90.00. Lengo la
hatua hii ni kupunguza gharama kwa wazalishaji wanaotumia bidhaa hiyo kama
malighafi;
(f)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye milk
cans zinazotambulika kwa HS Codes 7310.10.00 na 7310.29.90. Lengo la
hatua hii ni kutoa unafuu kwenye sekta ya maziwa nchini;
(g)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 10 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye LABSA (Organic
surface-active agents – Anionic) inayotambulika kwa HS Code 3402.11.00 kwa
utaratibu wa duty remission. Lengo la
hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa sabuni za unga na maji nchini;
(h)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 au 10
hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kuchakata ngozi zinazotambulika kwa HS Code 3208.20.00
na 3210.00.10 kwa utaratibu wa duty
remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa
wachakataji wa ngozi nchini;
(i)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 au 10
hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza mbolea zinazotambulika kwa HS Codes
2710.99.00, 2528.00.00 na 3505.20.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni
kutoa unafuu kwa wazalishaji wa mbolea nchini;
(j)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya tumbaku iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Code 5310.10.00
kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la
hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa tumbaku nchini;
(k)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya chai iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Codes
4819.20.90, 5407.44.00 na 3923.29.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni kutoa
unafuu kwa wachakataji wa chai (tea blenders) nchini;
(l)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi ya kutengeneza masufuria ya aluminium inayotambulika kwa HS Code
7606.92.00 kwa utaratibu wa duty remission.
Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa masufuria hayo
nchini;
(m) Kupunguza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia
25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa waunganishaji wa pikipiki za matairi
matatu bila kujumuisha fremu kwa kuwa zinatengenezwa hapa nchini (CKD for
three-wheel motorcycles excluding chassis and its components)
zinazotambulika kwa HS Code 8704.21.90 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo la hatua hii ni
kutoa unafuu kwa waunganishaji wa pikipiki hizo nchini ili kurahisisha usafirishaji
wa mizigo;
(n)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 au 10
hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza mabomba ya
plastiki (glass reinforced plastic pipes) zinazotambulika kwa HS Codes
3920.61.10, 7019.39.00, 7019.31.00, 6006.90.00, 7019.12.00, 3920.10.10,
4016.93.00, na 3907.91.00 kwa utaratibu wa duty
remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa
watengenezaji wa mabomba hayo nchini ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuwezesha ujenzi
wa miundombinu ya maji; na
(o)
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwenye mabati (Flat-rolled products of
other alloy steel, of a width of 600mm or more, not further worked than
hot-rolled, in coils) yanayotambulika kwa HS Code 7225.30.00. Lengo la
hatua hii ni kupunguza gharama kwa wazalishaji wanaotumia bidhaa hiyo kama malighafi.
(ii)
Mapendekezo ya kuendelea
na utekelezaji wa Viwango vya Ushuru wa Forodha vya mwaka 2020/21 ni kama
ifuatavyo:
(a)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha hadi asilimia 0 kutoka viwango
vya awali vya asilimia 10 na asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi zinazotumika
katika uzalishaji wa vifaa maalum vinavyotumika katika kupambana na ugonjwa wa
homa kali ya mapafu (UVIKO-19) vikiwemo Barakoa
(Masks), kipukusi (sanitizer), mashine za
kusaidia kupumua (ventilators), na
mavazi maalum
ya kujikinga yanayotumiwa na madaktari na wahudumu wa afya (PPE). Msamaha huu
utatolewa kwa utaratibu wa “duty
remission”. Hatua hii inalenga kutoa unafuu wa uzalishaji wa vifaa hivyo
hapa nchini ili kuongeza kasi katika kupambana na ugonjwa huo;
(b)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 10 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye mashine za kielektroniki zinazotumika
kukusanya mapato ya Serikali (Cash registers, Electronic Fiscal Device (EFD)
Machines and Point of Sale (POS) machines zinazotambulika katika HS Code
8470.50.00 na 8470.90.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya vifaa
hivi katika kuhasibu mapato ya Serikali;
(c)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vinavyotumiwa na wazalishaji wa
maziwa kwa joto la juu yanayodumu kwa muda mrefu (UHT Milk) vinavyotambulika kwa HS codes 4819.50.00. Lengo la hatua
hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa maziwa hapa nchini. Utaratibu wa Duty Remission utakaotumika kutoa unafuu
huo;
(d)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka kiwango cha asilimia
10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifuniko vya chupa
za mvinyo (corks and stoppers) vinavyotambulika kwa HS Codes 4503.10.00
kwa kuzingatia kuwa havizalishwi hapa nchini. Hatua hii inalenga kuwapunguzia
gharama wazalishaji wa mvinyo ili kuhamasisha na kuendeleza kilimo cha zao la
zabibu nchini pamoja na ajira. Utaratibu wa Duty
Remission utakaotumika kutoa unafuu huo;
(e)
Kuongeza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za marumaru
zinazotambulika kwa HS Code 6907.21.00; 6907.22.00; na 6907.23.00 zinazoingizwa
kutoka nje. Lengo la hatua hii ni kulinda na kukuza viwanda vya ndani vinavyozalisha
marumaru pamoja na kuongeza ajira;
(f)
Kuongeza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye chai inayotambulika kwa HS Code 09.02
inayoagizwa kutoka nje. Lengo la pendekezo hili ni kulinda viwanda vya ndani na
kuhamasisha kilimo cha chai hapa nchini pamoja na kuongeza ajira katika sekta
ya kilimo;
(g)
Kuongeza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye magunia ya kitani (sacks and bags of jute
or other textile bast fibers of heading 53.03) yanayotambulika kwa HS Code
6305.10.00 yanayoagizwa kutoka nje. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya
ndani vinavyotengeneza magunia ya katani, kukuza na kuendeleza kilimo cha zao
la mkonge hapa nchini pamoja na kuongeza ajira na mapato ya Serikali;
(h)
Kuongeza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 0 hadi
asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye unga wa kakao
unaoingizwa kutoka nje unaotambulika kwa HS Code 1805.00.00. Lengo ni kuchochea
na kuhamasisha kilimo cha zao la kakao nchini pamoja na kuongeza mapato ya
Serikali;
(i)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia kahawa vinavyotumiwa na viwanda vya
kusaga kahawa nchini. Vifungashio vitakavyohusika ni vile
vinavyotambulika katika HS codes 7310.21.00; 6305.10.00; 3923.50.10; 3923.50.90
na 3920.30.90. Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la kahawa na
kuvipa unafuu wa gharama viwanda vinavyosaga kahawa hapa nchini. Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika katika
kuagiza vifungashio hivyo;
(j)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia korosho.
Vifungashio vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika HS code
3923.21.00. Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la korosho na kuvipa
unafuu wa gharama viwanda vinavyochakata korosho hapa nchini. Aidha utaratibu
wa “Duty Remission” utatumika katika
kuagiza vifungashio hivyo;
(k)
Kupunguza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya
kuhifadhia pamba. Vifungashio vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika
HS codes 3920.30.90; 6305.39.00 na 7217.90.00. Hatua hii inalenga kuvutia
uwekezaji ili kuongeza thamani ya zao la pamba nchini;
(l)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye
malighafi za kutengeneza taulo za watoto (Baby Diapers) zinazotumbulika
kwa HS code 3506.91.00 Hot Melt Adhesive; PE film HS Code
3920.10.90, Empty bag for Baby Diapers HS Code 6305.33.00, Plastic
cask HS Code 3926.90.90; na kiwango cha awali cha asilimia 10 kwenye Super Absorbent Polymer HS
Code 3906.90.00, Wet strength paper HS Code 4803.00.00, Non-woven
HS Code 5603.11.00, Polyethylene laminated Nonwovens HS Code 5903.90.00,
Spandex HS Code 5402.44.00 na Dust free paper HS Code 4803.00.00.
Aidha, msamaha huu utatolewa kwa utaratibu wa “Duty Remission”. Hatua hii inatarajiwa kutoa unafuu wa gharama za
uzalishaji na kuongeza ajira;
(m)
Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye vifaa
vinavyotumika katika kukata, kung’arisha na kuongeza thamani ya madini ya vito
vinavyotambulika kwa HS Codes 6804.10.00; 7018.90.00; 7020.00.99; na kiwango
cha awali cha asilimia 10 kwenye HS Codes 3606.90.00; 6813.20.00; 8202.20.00;
8202.99.00; 8203.20.00; 8205.10.00; 8423.89.90; 8513.10.90; na 9002.19.00.
Hatua hii inalenga kuchochea uongezaji wa thamani kwenye madini. Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika katika
kuagiza vifaa hivyo;
(n)
Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye makaratasi (HS Code
4805.24.00 na 4805.25.00) yanayotumika kama malighafi ya kutengeneza
vifungashio aina ya maboksi (corrugated boxes). Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika. Lengo la
hatua hii ni kuwapa unafuu wazalishaji wa vifungashio hivyo hapa nchini ili
wananchi waweze kuvipata kwa bei nafuu;
(o)
Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwenye vifungashio vya mbegu
vinavyotambulika katika HS codes 3923.29.00; 6305.10.00;
4819.40.00; 7310.29.90; 6305.33.00; 6305.20.00; 6304.91.90 na 7607.19.90.
Utaratibu utakaotumika kutoa unafuu huo ni wa “duty remission”. Lengo la
hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa mbegu hapa nchini;
(p)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka
mmoja kwenye kahawa
inayotambulika kwa Heading 09.01
inayoagizwa kutoka nje ya nchi. Lengo la pendekezo hili ni kulinda viwanda vya
ndani na kuhamasisha kilimo cha kahawa hapa nchini pamoja na kuongeza ajira
katika sekta ya kilimo;
(q)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 10 au dola za kimarekani
125 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwenye bidhaa za chuma kwa
mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa. Bidhaa hizo ni “Flat
-rolled products of iron or Non-alloy steel na Flat –rolled products of other
alloy steel.” Bidhaa hizi
hutambulika katika HS Codes 7209.16.00; 7209.17.00; 7209.18.00; 7209.26.00;
7209.27.00; 7209.28.00; 7209.90.00; 7211.23.00; 7211.90.00; 7225.50.0 na
7226.92.00. Lengo la kuendelea kutoza viwango hivyo ni kulinda viwanda vya hapa
nchini, kukuza ajira pamoja na kudhibiti udanganyifu wa thamani halisi ya
bidhaa hizo kutoka nje;
(r)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 25 au dola za kimarekani
250 kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton)
kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika kwa HS codes 7210.41.00; 7210.49.00;
7210.61.00; 7210.69.00; 7210.70.00 na 7210.90.00 kutegemea kiwango
kitakachokuwa kikubwa badala ya ushuru wa asilimia 25 au dola za kimarekani 200
kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton), kwa mwaka mmoja. Lengo la
hatua hii ni kuwalinda wazalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini kutokana na
ushindani wa nje;
(s)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 10 au dola za kimarekani
250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwa
mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye bidhaa za mabati
zinazotambulika katika HS Code 7212.60.00 badala ya ushuru wa asilimia 10
pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu
wa thamani halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing
and under valuation), na kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(t)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 25 au dola za kimarekani
250 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton)
kwenye bidhaa za mabati kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa. Ushuru huo unahusu bidhaa
zinazotambulika katika HS Code 7212.30.00; 7212.40.00 na 7212.50,00. Hatua hii
ina lengo la kulinda viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani
halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and under
valuation), na kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(u)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 25 au dola za kimarekani 250 badala ya kiwango cha asilimia 25 au
dola za kimarekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo (metric ton) kwenye
bidhaa za chuma kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye
nondo kwa mwaka mmoja. (Reinforment bars and hallow profile). Hatua hii
inahusu bidhaa zinazotambulika katika Hs codes 7213.10.00; 7213.20.00;
7213.99.00; 7214.10.00; 7214.20.00; 7214.30.00; 7214.90.00; 7214.99.00;
7215.10.00; 7215.50.00; 7215.90.00; 7225.90.00; 7225.92.00; 7225.99.00;
7306.30.00; 7306.50.00; 7306.61.00; 7306.69.00; na 7306.90.00. Lengo la hatua
hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha nondo hapa nchini na kuongeza ajira;
(v)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za mboga
mboga (horticultural products) zinazotambulika kwa HS codes 0603.11.00;
0603.12.00; 0603.13.00; 0603.14.00; 0603.15.00; 0603.19.00; 0604.20.00;
0604.90.00; 0701.90.00; 0702.00.00; 0703.10.00; 0703.20.00; 0703.90.00;
0706.10.00; 0706.90.00; 0710.10.00; 0710.21.00; 0710.22.00; 0710.30.00;
0714.10.00; 0714.20.00; 0804.30.00; 0804.40.00; 0804.50.00; 0805.10.00;
0805.40.00; 0805.50.00; 0806.10.00; 0807.11.00; 0807.20.00; 0808.10.00;
0808.30.00; 0910.11.00 na 0910.12.00. Lengo la hatua hii ni kulinda wakulima wa
ndani ili kuendeleza kilimo cha matunda, mbogamboga na maua hapa nchini;
(w)
Kutoza ushuru wa forodha
kwa kiwango cha asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa
za fito za plastiki zijulikanazo kama PVC
Profiles HS Code 3916.10.00; 3916.20.00; 3916.90.00 ambazo hutumika kwa
ajili ya kutengenezea fremu za milango, madirisha n.k. Lengo la hatua hii ni
kuongeza mapato ya Serikali;
(x)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 25 badala ya asilimia 10
kwa mwaka mmoja kwenye karatasi zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini
ambazo zinazotambulika kwa HS codes 4804.11.00; 4804.21.00; 4804.29.00;
4804.31.00 na 4804.41.00. Lengo la hatua hii ni kuendelea kulinda viwanda
vinavyozalisha karatasi hizo hapa nchini;
(y)
Kutoza Ushuru wa Forodha
kwa kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 35 kwenye ngano inayotambulika kwa HS Code 1001.99.10 na HS Code
1001.99.90 kwa utaratibu wa “Duty
Remission” ambapo wanaonufaika na unafuu huu ni wenye viwanda vya kusaga
ngano. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa Viwanda vinavyozalisha unga
wa ngano;
(z)
Kutoza Ushuru wa Forodha
kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 25 kwa utaratibu wa duty
remission kwenye bidhaa ijulikanayo kama “Printed Alluminium Barrier Laminates” (ABL) HS Code 3920.10.90
ambayo hutumika kama malighafi ya kutengeneza vifungashio vya dawa ya meno
kwenye viwanda vya ndani. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu wa gharama kwa
viwanda vinavyozalisha dawa ya meno nchini;
(aa) Kutoza Ushuru
wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali
cha asilimia 10 kwa utaratibu wa “Duty
Remission” kwenye malighafi ya kutengeneza sabuni ijulikanayo kama RBD
Palm Stearin (HS Code 1511.90.40) kwa viwanda vinavyotengeneza sabuni
nchini. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa viwanda vya kuzalisha sabuni
nchini;
(bb) Kutoza kwa
mwaka mmoja Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 1.35 kwa
kilo moja ya viberiti (safety match boxes) vinavyotambuliwa kwenye HS
code 3605.00.00 kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa badala ya asilimia 25
pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha viberiti nchini dhidi ya bidhaa zenye ruzuku kutoka
nje na hivyo kuwa na ushindani sawa katika soko;
(cc)
Kutoza kwa mwaka mmoja
Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za kimarekani 350 kwa kila tani moja
ya ujazo (Metric ton) kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye
bidhaa za chuma za misumari zinazotambulika kwa HS code 7317.00.00 (nails,
tacks, drawing pins, corrugated nails, and staples other than those of heading
83.05) badala ya asilimia 25 pekee. Hatua hii inalenga kulinda viwanda
vinavyozalisha bidhaa hizo nchini.
(dd) Kutoza Ushuru
wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye soseji (sausages)
na bidhaa za aina hiyo zinazotambulika kwa HS code 1601.00.00. Lengo ni kuendelea
kulinda wajasiriamali wa ndani wanaozalisha bidhaa hizo;
(ee)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye chingamu (chewing
gum HS Code 1704.10.00), biskuti (Heading 19.05) na peremende (HS code
1704.90.00) zinazoagizwa kutoka nje. Lengo ni kuendelea kulinda viwanda vya
ndani vinavyozalisha bidhaa hizo na kukuza ajira;
(ff)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye chokoleti (chocolates)
Heading 18.06 kwa mwaka mmoja. Lengo ni kulinda viwanda vya ndani na kukuza
ajira;
(gg)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyanya
zilizosindikwa (tomato sauces) zinazotambulika katika HS code
2103.20.00. Hatua hii inalenga kulinda viwanda vinavyosindika nyanya nchini;
(hh) Kutoza Ushuru
wa Forodha wa asilimia 60 badala ya asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye maji ya
kunywa (mineral water) yanayotambulika katika HS code 2201.10.00. Hatua
hii inalenga kulinda viwanda vinavozalisha maji ya kunywa nchini;
(ii)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 35 badala ya asilimia 25 kwenye nyama zilizoainishwa katika SURA ya
2 katika Viwango vya pamoja vya ushuru wa forodha (meat and edible meat
offal of Chapter 2) kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni kuendelea
kulinda na kuchochea sekta ya ufugaji nchini;
(jj)
Kutoza Ushuru wa Forodha
kwa kiwango cha asilimia 25 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha awali cha
asilimia 10 kwenye mafuta ghafi ya kula yanayotambulika kwa HS codes
1507.10.00, 1580.10.00, 1511.10.00, 1512.11.00, 1513.11.00, 1514.11.00, 1514.91.00,
1515.11.00, 1515.21.00 na 1515.30.00. Hatua hii inalenga kulinda na kuhamasisha
uzalishaji wa mbegu za mafuta ya kula nchini, kuongeza ajira mashambani,
viwandani pamoja na kulinda fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta hayo
nje ya nchi;
(kk) Kutoza Ushuru
wa Forodha wa asilimia 35 badala ya asilimia 10 au 25 kwa mwaka mmoja kwenye
mafuta ya kula yaliyochakatwa kwa kiwango cha kati na mwisho (semi-refined
and refined)
yanayotambulika kwa HS codes 1507.90.00, 1508.90.00, 1509.90.00, 1510.00.00, 1511.90.10,
1511.90.30, 1511.90.90, 1512.19.00, 1512.29.00, 1513.19.00, 1513.29.00,
1514.19.00, 1514.99.00, 1515.19.00, 1515.20.00, 1515.50.00 na 1515.90.00. Lengo
la hatua hii ni kuhamasisha uchakataji wa mbegu za mafuta ya kula nchini,
kuongeza ajira viwandani na mashambani pamoja na kulinda fedha za kigeni
zinazotumika kuagiza mafuta hayo nje ya nchi;
(ll)
Kutoza Ushuru wa Forodha
wa asilimia 10 badala ya asilimia 0 kwenye Gypsum Powder HS code
2520.20.00 kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni kulinda wazalishaji wa Gypsum Powder nchini;
(mm)
Kutoza Ushuru wa Forodha
kwa kiwango cha asilimia 35 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango cha asilimia 100
kwenye sukari ya matumizi ya kawaida (consumption sugar) inayoagizwa
kutoka nje ya nchi kwa vibali maalum kwa lengo la kuziba pengo (gap) la uzalishaji hapa nchini;
(nn) Kutoza kwa
mwaka mmoja Ushuru wa Forodha wa asilimia 35 kwenye mitumba inayoingia kutoka
nje badala ya asilimia 35 au dola za
marekani 0.40 kwa kilo moja kutegemea kiwango kipi kikubwa kwa lengo la kutoa
unafuu kwa watumiaji nchini;
(oo) Kutoa unafuu
wa Ushuru wa Forodha kwenye malighafi, vipuri na mashine vinavyotumika katika
kutengeneza viatu vya ngozi na nguo. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha ukuaji
wa sekta ya nguo na viatu vya ngozi nchini; na
(pp) Kutoza Ushuru
wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa utaratibu wa “Duty Remission” kwenye
malighafi ya kutengeneza leaf springs
za magari inayotambulika kwa HS Code 7228.20.00. Lengo la hatua hii ni kutoa
unafuu kwa viwanda vya kuzalisha bidhaa hiyo nchini.
(iii) Mawaziri wa Fedha wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
walikubaliana kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Customs Management
Act, 2004) kwa kuweka thamani ya
chini ya bidhaa isiyopaswa kutozwa ushuru wa Forodha kuwa Dola za Marekani 50.
(iv) Serikali inapendekeza kuliachia jukumu la uthaminishaji wa vitenge
vinavyoingizwa nchini kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ili
uthaminishaji wa bidhaa hiyo uzingatie Kanuni zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria
ya Usimamizi wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (2004). Sambamba na
hatua hiyo, napendekeza utaratibu wa kuthaminisha vitenge kuwa dola za Marekani
kati ya 0.55 hadi dola za Marekani 1 kwa mita ya kitenge cha Polyester na dola za Marekani kati ya
0.60 hadi dola za Marekani 1 kwa mita ya kitenge chenye pamba inapotokea
thamani iliyowasilishwa (declared) kuwa chini ya kiwango hicho maalumu
kwa kuzingatia taratibu za uthaminishaji wa bidhaa hizo.
(v)
Kuondoa sharti la kuweka
dhamana ya asilimia 15 ya ziada ya Ushuru wa Forodha inayopaswa kurejeshwa (refundable)
kwenye sukari ya matumizi ya viwandani. Lengo la hatua hii ni kuwaongezea
wazalishaji ukwasi (liquidity) kwa kutowazuilia mtaji wa uzalishaji (working
capital). Hata hivyo, wazalishaji watakaobainika kufanya udanganyifu
watarejeshewa sharti hili pamoja na kuchukuliwa hatua nyingine zilizopo
kisheria.
Hatua hizi kwa ujumla
wake zinatarajiwa kupunguza mapato
ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 32,626.38.
E. Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438
63. Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanyia Marekebisho ya Sheria
ya Usimamizi wa Kodi SURA 438 kama ifuatavyo:
(i)
Kufuta kifungu cha 92A kwa lengo la kuziwezesha mahakama
kukusanya mapato yanayotokana na adhabu na faini zinazolipwa mahakamani badala
ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kama ilivyo kwa faini na adhabu kwa makosa
mengine ambayo mahakama huyatolea maamuzi na hivyo kurahisisha ukusanywaji wa
mapato hayo;
(ii)
Kufuta kifungu cha 70(2) ili kumpa Mamlaka Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato kutekeleza matakwa ya Sheria husika na kurahisisha
upunguzaji au uondoaji wa riba na adhabu ya madeni iwapo kutakuwa na sababu za
msingi za kufanya hivyo; na
(iii)
Kufanya marekebisho ya Kanuni Na. 15 ya ukokotoaji wa
kodi za kimataifa (Transfer Pricing Regulations) kwa kufuta kifungu
kinachoweka adhabu ya asilimia 100 kwa kushindwa kutekeleza matakwa ya Sheria.
Lengo la hatua hii ni kuwaondolea walipakodi adhabu kubwa ili kuboresha
mazingira ya ufanyaji biashara na kuvutia uwekezaji nchini.
F. Sheria ya Fedha za
Serikali za Mitaa, SURA 290
64. Mheshimiwa Spika,
Napendekeza kufanya Marekebisho kwenye Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa
kama ifuatavyo:
(i)
Kubainisha mazingira
ambayo Kampuni iliyolipa tozo ya huduma haitawajibika kulipa tozo ya
uzalishaji. Marekebisho hayo yanalenga kutatua mgongano uliojitokeza kwenye
kutafsiri kifungu husika; na
(ii)
Kupunguza ada za matangazo
kama ifuatavyo:
(a)
Mabango yanayowaka kutoka
shilingi 18,000 hadi shilingi
13,000;
(b) Mabango
yasiyowaka kutoka shilingi 15,000 hadi shilingi 10,000;
(c)
Matangazo ya ukutani
kutoka shilingi
15,000 hadi shilingi 10,000;
(d) Matangazo ya
kielectroniki kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 10,000;
(e)
Matangazo kwenye magari kutoka shilingi 15,000
hadi shillingi 10,000 kwa watangazaji wanaotangaza bidhaa za watu wengine;
(f)
Matangazo ya muda
mfupi/promosheni kwa siku kutoka shilingi 55,000 hadi shilingi 50,000; na
(g)
Kila mabango 100 ya
promosheni ya kwanza au sehemu ya fungu la mabango 100 ya kwanza kutoka
shilingi 100,000 hadi shilingi
50,000.
Ada zote hizi zinatozwa kwa futi za mraba. Kushushwa kwa ada hizi
kutapunguza gharama za kutangaza biashara nchini na hatimaye kukuza ushindani
kwenye biashara.
G. Sheria ya Kodi ya Majengo, SURA 289;
65.
Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya kodi ya majengo,
SURA 289 ili ukusanyaji wa kodi ya majengo ufanyike kwa kutumia mfumo wa
ununuzi na utumiaji wa umeme kupitia mashine za LUKU. Kila mita ya umeme ina uhusiano na mmiliki wa jengo au mtumiaji wa mita, na
kwa kuwa Sheria ya Kodi ya Majengo inataka kodi hiyo ikusanywe kwa mmiliki au
mtumiaji wa jengo, hivyo, napendekeza kodi ya majengo ya kiwango cha shilingi
1,000/= kwa mwezi kwenye nyumba za kawaida zenye mita moja na itakatwa kwenye
ununuzi wa umeme (LUKU). Aidha, napendekeza kiwango cha shilingi 5,000/= kwa
mwezi kwa kila ghorofa au apartment zenye mita moja na itakatwa kwenye
ununuzi wa umeme (LUKU). Serikali itaweka utaratibu kwenye nyumba za kawaida na
za ghorofa zinazochangia mita moja na zinazotumia mita zaidi ya moja.
H. Sheria ya Ardhi, SURA 113
66. Mheshimiwa Spika,
Napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Ardhi, SURA ya 113 na Kanuni zake
za mwaka 2001 kwa kupunguza tozo ya mbele (premium) inayotozwa wakati wa
umilikishaji wa ardhi kama ifuatavyo:
(i)
Kupunguza tozo kutoka
asilimia 2.5 hadi asilimia 0.5 kwa umiliki mpya wa ardhi; na
(ii)
Kupunguza tozo kutoka
asilimia 1 hadi asilimia 0.5 kwa urasimishaji.
Lengo la pendekezo hili ni kuhamasisha wamiliki wa ardhi
kukamilisha taratibu za kupata hatimiliki na kufanikisha sehemu kubwa ya ardhi
kuandikishwa na kupunguza migogoro. Hatua za kufanya marekebisho ya Sheria ya
Ardhi kwa ujumla wake zinatarajiwa
kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 9,000.
I.
Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189
67. Mheshimiwa Spika,
Napendekeza kuifanyia Marekebisho Sheria ya Ushuru wa Stempu kwa lengo la
kuhuisha viwango vilivyopo sambamba na mfumuko wa bei kwa kuwa viwango hivyo ni
vya muda mrefu tangu mwaka 2006. Marekebisho hayo ni kama ifuatavyo:
(i)
Ushuru wa Stempu kutoka
shilingi 500 hadi shilingi 2,000;
(ii)
Ushuru wa Stempu kwenye
Katiba za Makampuni kutoka shilingi 5,000 hadi shilingi 10,000;
(iii)
Ushuru wa Stempu kwenye
nyaraka za Ubia ambazo mtaji wake unazidi shilingi 100,000 lakini hauzidi
shilingi 1,000,000 kutoka shilingi 2,000 hadi shilingi 5,000;
(iv)
Ushuru wa Stempu kwenye
nyaraka za Ubia ambazo mtaji wake unazidi shilingi 1,000,000 kutoka shilingi
5,000 hadi shilingi 10,000; na
(v)
Ushuru wa Stempu kwenye
nyaraka za kumaliza ubia kutoka shilingi 1,000 hadi 10,000.
Hatua za kufanya marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Stempu kwa
ujumla wake zinatarajiwa kuongeza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 2,500.89.
J. Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82
68. Mheshimiwa Spika,
Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
stadi kama ifuatavyo:
(i)
Kupandisha kiwango cha
chini cha idadi ya waajiriwa wanaostahili kulipiwa kodi kutoka 4 wa sasa hadi
10. Lengo la marekebisho haya ni kuwapunguzia mzigo wa kodi waajiri wenye idadi
ndogo ya waajiriwa na kuchochea ukuaji wa uwekezaji wa uwekezaji nchini;
(ii)
Kufuta tozo ya Elimu na
mafunzo ya Ufundi Stadi kwa hospitali zinazomilikiwa na taasisi za kidini kwa
kuwa taasisi hizi zimekuwa zikiisaidia sana Serikali kufikisha huduma za afya
hata kwenye maeneo ambayo Serikali haijaweza kupeleka huduma kutokana na ufinyu
wa Bajeti. Aidha, taasisi hizi zimekuwa na ushirikiano na Serikali kwa
makubaliano maalum kwa baadhi ya maeneo ya kutoa huduma za afya. Lengo la hatua
hii ni kutoa unafuu wa utoaji huduma za afya kwa vituo vya Afya; na
(iii)
Kuanzisha utaratibu
mahsusi wa ulipaji wa tozo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuwa ni asilimia 0.4
ya thamani ya mauzo ya madini itakayolipwa na mchimbaji mdogo wa madini pindi
atakapouza madini hayo kwenye masoko na vituo vya madini vinavyotambulika na
Tume ya Taifa ya Madini.
K.Sheria ya Michezo ya Kubatisha, SURA
41
69. Mheshimiwa Spika,
napendekeza kufanya mabadiliko ya Sheria ya Michezo ya Kubahatisha kama
ifuatavyo:
(i)
Kupunguza kiwango
cha kodi kwenye zawadi ya ushindi (Gaming tax on Winnings) kutoka
asilimia 20 hadi asilimia 15 kwenye Michezo ya kubahatisha ya ubashiri wa matokeo
ya michezo (Sports betting);
(ii)
Kuongeza kiwango cha Kodi
katika michezo ya kubahatisha ya ubashiri wa matokeo ya michezo (sports betting) kwa mapato ghafi (Gross
Gaming Revenue - GGR) kutoka asilimia 25 ya mauzo ghafi hadi asilimia 30 ya
mauzo ghafi. Ongezeko la asilimia 5 litapelekwa kwenye Mfuko wa Maendeleo ya
Michezo kwa ajili ya kuendeleza michezo nchini;
(iii)
Kutoza kodi ya michezo ya
kubahatisha kwa asilimia 10 ya mapato ghafi kwenye michezo ya kubahatisha
inayoendeshwa kwa kompyuta (Virtual Games); na
(iv)
Kutoza Kodi ya michezo ya
kubahatisha kwa asilimia 10 ya mapato ghafi kwenye michezo ya kubahatisha iliyo
chini ya majaribio.
Lengo la hatua hizi
ni kuleta usawa wa utozaji kodi katika michezo ya kubahatisha. Hatua hizi za
marekebisho ya michezo ya kubahatisha zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 14,925.38.
L. Sheria ya Ukaguzi wa Umma, SURA 418
70. Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanya Marekebisho kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Umma,
SURA 418 kama ifuatavyo;
(i)
Kumwezesha Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa na uwezo wa kisheria wa kukagua
mashirika yaliyoanzishwa chini ya Sheria ya Makampuni ambayo Serikali ina
umiliki wa hisa ili kumwezesha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kukagua
mashirika/makampuni hayo. Kwa sasa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali anakagua mashirika/makampuni hayo bila kuwa na nguvu za kisheria, hali
inayoweza kuleta mgogoro wa kisheria; na
(ii)
Kumwezesha Waziri mwenye
dhamana ya Fedha kuwasilisha Bungeni majibu kuhusu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kwenye kikao kinachofuata cha Bunge baada ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwasilisha taarifa yake badala
ya utaratibu wa sasa ambapo taarifa zote huwasilishwa kwa pamoja katika kikao
kimoja cha Bunge.
M. Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, SURA 134
71.
Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Mikopo, Dhamana
na Misaada SURA 134 ili kuruhusu Serikali kudhamini kampuni au taasisi yoyote
kukopa kiasi kisichozidi thamani ya Hisa za Serikali ya Tanzania kwenye mradi
husika baada ya kupata ridhaa ya Baraza la Mawaziri.
N. Sheria ya Usajili wa Magari, SURA 124
72.
Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Usajili wa Magari SURA 124,
kwa kupunguza ada ya usajili wa magari kwa namba binafsi kutoka shillingi
10,000,000 hadi shillingi 5,000,000 kila baada ya miaka mitatu. Lengo la hatua
hii ni kuwezesha wamiliki wa magari kuchagua namba binafsi ya usajili wa gari
kwa gharama nafuu na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa kuwa kiwango cha
sasa hakina mwitikio mzuri.
Hatua hizi za
marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Magari inatarajiwa kuongeza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 270.
O.Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168
73.
Mheshimiwa Spika, vijana
wengi wamejiajiri kwenye sekta ndogo ya kuendesha bajaji na pikipiki
zikijulikana kama bodaboda. Hata hivyo, Vijana hawa hupata usumbufu mkubwa wa
kulipa faini kutoka kwenye vipato vyao pale panapotokea uvunjaji wa Sheria ya
Usalama Barabarani umefanywa na abiria wao. Hali hii imekuwa ikisababisha
baadhi yao kushindwa kulipa faini na hivyo kuzitelekeza pikipiki zao kwenye
vituo vya polisi. Mheshimiwa Rais alielekeza
jeshi la Polisi kujikita kwenye kutoa elimu kuhusu usalama barabarani badala ya
kuwekeza kwenye makosa na kugeuza faini kuwa chanzo cha mapato. Hivyo basi,
Napendekeza kupunguza adhabu zinazotolewa chini ya Sheria ya Usalama Barabarani
SURA 168 kwa makosa ya Pikipiki na Bajaji kutoka shilingi 30,000 za sasa hadi
shilingi 10,000 kwa kosa moja. Lengo la hatua hii ni kuweka adhabu kwa
kuzingatia uwezo wa kulipa. Aidha,
adhabu kwa makosa mengine ya vyombo vya moto zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria
zinaendelea kubaki kama ilivyo sasa.
P. Sheria ya Raia wa Kigeni
(Uratibu wa Ajira), Na. 1 ya mwaka 2015
74. Mheshimiwa Spika,
Napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Raia wa Kigeni (Uratibu wa Ajira),
Na. 1 ya 2015 kama ifuatavyo:
(i)
Kuweka adhabu ya kiasi cha
shilingi 500,000/= kwa kila mwezi kwa mwajiri aliyeajiri raia wa kigeni na
kushindwa kuwasilisha ritani za kila mwezi zenye taarifa za raia wa kigeni
aliowaajiri ikiwemo taarifa zao za mishahara kwa Kamishna wa Kazi. Lengo la
pendekezo hili ni kuhimiza uwajibikaji wa hiari;
(ii)
Kuweka adhabu ya kifungo
cha miezi 12 au faini ya shilingi millioni kumi (10) au vyote kwa mwajiri aliyeajiri
raia wa kigeni na kushindwa kuwasilisha ritani za mwezi zenye taarifa za raia
wa kigeni aliowaajiri ikiwemo taarifa zao za mishahara kwa Kamisha wa kazi.
Lengo la pendekezo hili ni kuhimiza uwajibikaji wa hiari.
Q.Marekebisho
ya Ada na Tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa, Wakala, Mamlaka za Udhibiti na Idara zinazojitegemea
75.
Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanya marekebisho ya viwango
vya ada na tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Mikoa, Wakala, Mamlaka za
Udhibiti na Idara zinazojitegemea ili kuvihuisha kulingana na hali halisi ya
ukuaji wa uchumi. Aidha, marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria
ya Fedha ya mwaka 2021 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).
Marekebisho hayo ni kama ifuatavyo:
i.
Wizara ya Kilimo
Kuanzisha Tozo za Umwagiliaji kwa watumiaji wa miundombinu ya
umwagiliaji ili kuwezesha miradi hiyo kuwa endelevu na kuwezesha ujenzi wa
miundombinu mipya. Viwango vinavyopendekezwa kama ifuatavyo:
(a)
Kutoza
ada ya shillingi 60,000 kwenye usajili wa vyama vya umwagiliaji; na
(b)
Kutoza
ada ya Huduma ya umwagiliaji ya asilimia tano (5) ya mavuno ya msimu kwa eneo
la vyama vya umwagiliaji.
ii.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kufanya marekebisho kwenye Kanuni za Jumuiya ya Kijamii, SURA 337
ili kuhuisha viwango vilivyokuwa vinatumika awali na kuanzisha tozo katika
maeneo ambayo hayakuwa yanatozwa. Marekebisho hayo ni kama ifuatavyo:
(a) Kutoza tozo ya shilingi 100,000 ya
uharibifu wa cheti cha Jumuiya ya Kijamii unaolazimu kupewa cheti kipya;
(b) Kutoza tozo ya shilingi 50,000 ya
kukosea kwa jina kulikosababishwa na mwombaji atakayepaswa kupewa cheti kipya;
(c) Kutoza tozo ya shilingi 50,000 ya
kubadili taarifa za anuani ya Posta au makao makuu ya Jumuiya;
(d) Kuongeza ada ya kuwasilisha maombi ya
usajili wa Jumuiya ya Kijamii kutoka shilingi 10,000 hadi shilingi 50,000;
(e) Kuongeza ada ya mwaka kwa taasisi za
kidini kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 100,000;
(f) Kuongeza ada ya mwaka kwa taasisi
zisizo za kidini kutoka shilingi 40,000 hadi shilingi 50,000;
(g) Kuongeza ada ya mwaka kwa jumuiya za
dini kutoka nje ya Nchi kutoka Dola za Marekani 30 hadi Dola za Marekani 60;
(h) Kuongeza ada ya mwaka kwa jumuiya
zisizo za kidini kutoka nje ya Nchi kutoka Dola za Marekani 30 hadi Dola za
Marekani 60;
(i) Kuongeza tozo ya maombi ya kubadili
jina la jumuiya kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 100,000;
(j) Kuongeza tozo ya maombi ya marekebisho
ya katiba ya jumuiya kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 100,000;
(k) Kuongeza tozo ya maombi ya nakala kwa
ajili ya ushahidi katika vyombo vya utoaji haki kwa jumuiya kutoka shilingi
50,000/= hadi shilingi 100,000;
(l) Kuongeza tozo ya maombi ya nyaraka kwa
jumuiya yenyewe kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 50,000;
(m) Kuongeza tozo ya upotevu wa cheti cha
jumuiya kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 100,000;
(n) Kuongeza tozo ya upotevu wa cheti cha
jumuiya kwa mara ya pili kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 200,000;
(o) Kuongeza ada ya upekuzi kwa jumuiya
yenyewe kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 100,000; na
(p) Kuongeza ada ya upekuzi kwa mwombaji
mwingine kutoka shilingi 50,000 hadi shilingi 200,000.
iii.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Kuanzisha kanuni za ada na tozo za Shirika la Viwango ya mwaka 2021 ambazo zinaanzisha ada na tozo mpya pamoja
na kupitia ada na tozo zilizokuwa zinatozwa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na
Dawa Tanzania (TFDA) hapo awali. Mapendekezo hayo yameainishwa katika Kiambatisho
Na. 5.
iv.
Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu
Kufanya marekebisho kwenye kanuni za ada na tozo za Hifadhi za
Bahari na maeneo Tengefu ya mwaka 2009 ili kupitia ada na tozo mbalimbali
zilizoanzishwa kwa ajili ya hifadhi za bahari na maeneo tengefu kama
ilivyoambatishwa kwenye Kiambatisho Na. 6.
R. Marekebisho madogo madogo
katika baadhi ya Sheria za Kodi na
Sheria nyingine mbalimbali.
76.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho mengine madogo yasiyo ya kisera
katika sheria mbalimbali za kodi pamoja na sheria nyingine ili ziwe sanjari na
azma ya kurahisisha utekelezaji wake. Marekebisho hayo yataainishwa katika
Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2021
na Matangazo ya Serikali (Government
Notices).
S. Kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa
Kuboresha Mazingira ya kufanya Biashara (Blueprint)
kwa kurekebisha Ada na Tozo mbalimbali
77. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufuta au kupunguza ada na tozo mbalimbali
zinazotozwa na Wizara, Idara na Taasisi zinazojitegemea ili Kuondoa kero na
urasimu kwa wafanyabiashara na kuboresha mazingira ya biashara na
uwekezaji hasa katika kipindi hiki cha mlipuko wa janga la homa kali ya mapafu
duniani. Hatua hizi ni sehemu ya mwendelezo wa
utekelezaji wa Mpango wa kuboresha Mfumo
wa udhibiti wa Biashara (Blueprint for Regulatory Reforms to Improve the
Business Environment). Marekebisho hayo yatajumuisha:
i. Wizara ya Maliasili
na Utalii
Kupunguza ada ya leseni ya Biashara ya Utalii (TTBL) kwa Wakala za
Safari kutoka Dola za Marekani 2000 hadi Dola za Marekani 500 ili kuhamasisha
biashara ya utalii.
ii. Wizara ya Mifugo na
Uvuvi
Kutoza ada ya shilingi 40,000 kwenye kibali cha kupeleka nyama nje
ya nchi kwa nyama zote bila kujali aina ya nyama badala ya ada ya shilingi 100
kwa kilo moja ya nyama ya ng’ombe na shilingi 50 kwa kilo moja ya nyama ya
mbuzi na kondoo.
iii. Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi.
Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, SURA
263 kwa kupunguza kiwango cha mchango kwa Sekta Binafsi kutoka asilimia 1.0
inayotozwa sasa hadi asilimia 0.6 ya mapato ghafi ya wafanyakazi. Lengo la
hatua hii ni kutoa unafuu wa kutosha kwa biashara zilizopo na uwekezaji mpya
utakaofanyika nchini.
iv. Tume ya nguvu za mionzi Tanzania
Kufuta ada ya Utambuzi wa Mionzi ambayo
inatozwa kwa kiwango cha asilimia 0.2 ya Malipwani kwenye mizigo ya vyakula
inayosafirishwa kwenye nchi ambazo hazina sharti la uhitaji wa cheti cha
utambuzi wa mionzi. Lengo la hatua hii ni kupunguza tozo kero na gharama za
biashara na hivyo kuchochea mauzo ya bidhaa nje ya nchi sambamba na kupunguza
utoroshaji wa mazao hayo kwenda nchi jirani kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi.
v.
Idara ya Uhamiaji
(a)
Kuondoa ada ya kibali cha
kuingia nchini (VISA/PASS FEE) kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka nchi ya Msumbiji
kwa ajili ya Mpango wa kubadilishana Wanafunzi wa Elimu ya Juu baina ya
Tanzania na Msumbiji (TAMOSE). Lengo la pendekezo hili ni kutekeleza matakwa ya
makubaliano kati ya nchi hiyo na Tanzania kuondoleana ada hizo ambapo Msumbiji
imeshaanza kutekeleza makubaliano hayo; na
(b)
Kuhusu Zanzibar,
napendekeza kutekeleza utaratibu wa kuruhusu mapato yanayotokana na Kodi na
tozo za Muungano kwenye mapato yanayotokana na tozo za VISA ili yaweze kutumika
pale yalipokusanywa (Derivation Principle) kama ilivyo kwenye mapato
mengine ya Muungano. Mapendekezo haya yanafanya suala hili liondolewe kwenye
orodha ya changamoto za Muuungano. Mapato yatokanayo na tozo za VISA upande wa
Zanzibar yaonekane kwenye bajeti upande wa Zanzibar, kuidhinishwa na kutumika
Zanzibar.
vi. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kufanya
marekebisho ya Sheria ya Jeshi ya Zimamoto na Uokoaji SURA 427 kwa kufuta na kupunguza ada na tozo
zifuatazo:
(a)
Kufuta tozo ya
ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto kwenye kilimo cha mbogamboga
na maua;
(b)
Kufuta tozo ya Cheti cha
Umahiri (Certificate of Competence) cha Kinga na tahadhari ya moto inayotozwa kwenye Vituo vya Mafuta nchini;
(c)
Kufuta tozo ya
ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto kwenye mashamba makubwa na nyumba za makazi
yaliyopo ndani ya mashamba hayo yaliyokuwa yakitozwa kati ya shillingi 100,000
hadi 1,000,000;
(d)
Kuongeza
ukubwa wa eneo lisilopaswa kutozwa tozo ya Ukaguzi wa Kinga na tahadhari ya
moto linatumika kwa maonyesho ya biashara kuanzia mita za mraba zisizopungua
2000 hadi mita za mraba 10,000; na
(e)
Kuongeza
idadi ya wanafunzi wa bweni kwa shule zisizopaswa kutozwa tozo ya Ukaguzi wa Kinga na tahadhari za moto kutoka
wanafunzi wasiozidi 100 hadi wanafunzi 200.
vii. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
Kufanya marekebisho kwenye
kanuni ya ada na tozo Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2019 kama ifuatavyo:
(a)
Kupunguza ada ya kuharibu
dawa zilizoisha muda wa matumizi yake kutoka shilingi 1,000,000 hadi shilingi
100,000; na
(b)
Kupunguza ada ya kila
mwaka ya mazingira kutoka shilingi 200,000 hadi shilingi 100,000.
viii. Bodi ya Nyama
Tanzania
Kutoza ada ya shilingi 70,000 kwa Cheti cha Kukubaliwa kupeleka
nyama nje ya Nchi badala ya kiwango cha asilimia 1 ya malipwani.
ix. Wakala wa Usalama na
Afya Mahali pa Kazi (OSHA)
Kupunguza
tozo ya ukaguzi wa Umeme kwa kipimo kimoja (electrical
inspection, electrical insulation test and general inspection) kutoka
shilingi 590,000 hadi 150,000. Tozo hii inatozwa kabla ya kuanza biashara ya
mafuta. Pendekezo hili linatarajia kuchochea mazingira wezeshi ya biashara
nchini hususan katika maeneo ya vijijini.
x. Utoaji Leseni za Bima kwa Makampuni
Napendekeza kubadili utaratibu wa sasa wa makampuni ya bima
kulazimika kuomba leseni upya kila mwaka na badala yake makampuni yanayofanya
vizuri yawe na leseni ya kudumu, na makampuni yalioko kwenye hali ya uangalizi
yapewe leseni ya miaka mitatu huku yakiwa kwenye uangalizi na yakiimarika na
kufanya vizuri yaingie kwenye leseni za kudumu. Taratibu za ufuatiliaji na
malipo ya kila mwaka yaendelee kama ilivyo sasa. Lengo ni kupunguza ukiritimba.
xi. Uboreshaji wa Mazingira ya Ufanyaji Biashara
Sambamba na hatua za kikodi zilizolenga
kupunguza gharama ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara, Serikali
itakamilisha mfumo wa kimtandao wa kuwa na dirisha moja la upatikanaji wa
vibali mbalimbali katika Idara zote zinazohusika na usajili na vibali ili kuwapunguzia
wawekezaji mizunguko ya kutembea ofisi zaidi ya moja kuhangaika nenda rudi
kutafuta vibali vinavyotolewana ofisi zaidi ya moja. Lengo la hatua hii
nikurahisisha mazingira ya kufanya biashara kama ilivyobainishwa kwenye Blueprint.
T. Maeneo Mahususi
i.
Barabara za Mijini na
Vijijini
78. Mheshimiwa Spika, hali ya barabara vijijini hairidhishi ambapo bado vipo vijiji ambavyo
havina barabara kabisa. Barabara nyingi zinazosimamiwa na TARURA zina
hali mbaya. Kwa sasa mtandao wa barabara zilizo chini ya TARURA una urefu
usiopungua kilomita 108,946.2 ambazo zinaunganisha maeneo mbalimbali ya mijini
na vijijini. Hadi Desemba 2020, mtandao wa barabara zilizo chini ya TARURA
wenye kiwango cha lami ulifikia kilometa 2,250.69, sawa na asilimia 2.1 tu,
changarawe kilometa 27,809.26 (asilimia 25.6) na udongo kilometa 78,886.25 (asilimia 72.4).
79. Mheshimiwa Spika, hali hii ya barabara ina madhara makubwa sana
kwa jamii yetu kwani baadhi ya akina mama wajawazito wanapoteza maisha kwa
kuchelewa kufika kwenye vituo vya afya. Aidha, wapo wengine ambao
wanajifungulia njiani kutokana na kuchelewa kufika kwenye vituo vya afya. Vilevile, wapo baadhi ya wanafunzi wanaosombwa na maji
na kufariki kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, hususan katika maeneo
ya vijijini. Kadhalika, bado kuna changamoto ya usafirishaji wa mazao na bidhaa
kutoka au kwenda barabara kuu katika baadhi ya maeneo. Serikali imeona ipo haja
ya kutafuta vyanzo vipya vya mapato kuongezea katika mgawo wa sasa kupitia
Mfuko wa Barabara ili kufanikisha ugharamiaji wa mtandao wa barabara hizo.
ii.
Upatikanaji wa Maji Safi na Salama Mijini na Vijijini
80.
Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa maji safi na salama
mijini na vijijini bado hairidhishi. Maji hayana mbadala, maji ni uhai, maji ni
maisha kwa viumbe hai vyote. Bado vipo vijiji ambavyo havina kisima hata kimoja
cha maji safi na salama na badala yake hutumia maji ya mapalio, maji ya
madimbwi, maji ya mito wanayochangia na wanyama. Tanzania ina vyanzo vikubwa na vya uhakika vya maji ikiwa ni pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa Rukwa, Ziwa Chala,
Mto Kiwira, Ruvu, Rufiji na Ruvuma pamoja na mingine. Aidha, kuna uwezekano wa
kutumia mabwawa makubwa kama ya Kidunda,
Ndembela na Farkwa kama yangekamilika lakini
utekelezaji wake haujaanza pamoja na fidia kutolewa na Serikali kutokana
na uhaba wa fedha. Ipo miradi mingi katika mikoa ya Iringa, Kagera, Kigoma,
Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma,
Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora, Tanga na Simiyu inayotakiwa
kutekelezwa katika mwaka 2021/22, lakini haikuwa katika bajeti. Mikoa mingine
ambayo sikuitaja hapa iko kwenye bajeti ya Wizara husika.
81. Mheshimiwa Spika, hali ya ukosefu wa maji safi na salama ina madhara
makubwa sana kwa jamii yetu. Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa inampa nafuu
mwanamke katika kufanya shughuli zake za kiuchumi, lengo likiwa ni kumtua mama
ndoo kichwani na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowakumba akina mama na
mabinti katika harakati za kutafuta maji. Aidha, kuna baadhi ya wanafunzi
wanakosa masomo na kuharibu maisha yao kutokana na uhaba wa maji katika maeneo
yao. Hivyo, Serikali imeona ipo haja ya kuongeza fedha za kugharamia miradi ya
maji kwa kubuni vyanzo mbadala vya mapato kwa ajili ya kugharamia miradi ya
maji hususan katika maeneo ambayo yana uhaba mkubwa wa maji.
iii.
Afya na Bima ya Afya kwa Wote
82.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya Afya ni sekta muhimu katika ustawi
wa jamii yetu na ni moja ya mahitaji muhimu sana katika maisha ya sasa ya
mwanadamu. Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa sana katika sekta hii, ingawa
bado kuna kazi kubwa ya kufanya kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na
mabadiliko ya hali za kiafya kwenye kizazi cha leo. Aidha, wananchi katika
maeneo mbalimbali wametumia nguvu kubwa katika kutafuta ufumbuzi wa masuala ya
upatikanaji wa huduma za afya kwa kujenga maboma karibu na maeneo yao. Majengo yaliojengwa
kwa nguvu za wananchi yamekaa kwa muda mrefu, kati ya miaka mitano (5) hadi 15. Hadi kufikia Juni
2021, kuna jumla ya maboma 8,004 ya zahanati
ambayo yapo katika mikoa mbalimbali nchini na yapo katika hatua mbalimbali za
kukamilishwa. Vilevile, yapo maboma
kwenye ngazi ya vituo vya afya zaidi ya 1,500 ambayo yametumia nguvu ya
wananchi na yanahitaji kukamilishwa. Serikali itaendelea na jitihada za
kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma hayo pamoja na kuajiri
wataalamu wa afya na kuimarisha upatikanaji wa dawa, vitendanishi, vifaa na
vifaa tiba.
83. Mheshimiwa Spika, kuna mradi mkubwa wa bima kwa wote (Universal Health
Care) unaolenga kuwafikia watanzania wote. Tanzania ina jumla ya kaya
milioni 12.827, ambapo asilimia 20 ya kaya hizo inakadiriwa kuwa ni kaya
zisizokuwa na uwezo. Katika kufanikisha utekelezaji wa dhana ya bima ya afya kwa
wananchi wote, Serikali itahitaji zaidi ya shilingi bilioni 149 katika mwaka wa
kwanza kwa ajili ya kaya zisizo na uwezo. Kiasi hicho cha fedha kitaendelea
kuongezwa kila mwaka ili ifikapo mwaka 2034/35, wananchi wote wawe wamefikiwa
na bima ya afya. Serikali imeendelea kuboresha na kusogeza huduma za afya
karibu na wananchi ambapo vituo vya kutolea huduma za afya kwa ngazi mbalimbali
vimeendelea kujengwa ili bima ya Afya iweze kutumika na kuwanufaisha wananchi
wote.
iv.
Elimu
84.
Mheshimiwa Spika, kuhusu sekta ya elimu kuna kazi kubwa bado
iko mbele yetu. Bado kuna shule ambazo zina wanafunzi wengi
kuliko idadi ya madarasa na zipo zinazogawa mikondo ili wanafunzi wengine
wasome asubuhi na wengine wasome mchana. Hali hii inapunguza muda wa wanafunzi
kusoma. Zipo shule ambazo kwenye darasa moja wanaweka uzio wa ubao kutenganisha
ili chumba kimoja wasome wanafunzi wa madaraja mawili. Aidha, zipo shule ambazo
miundombinu yake imechakaa sana kiasi cha kutishia usalama wa watoto na walimu
wetu. Yapo pia madarasa yaliyoezekwa kwa nyasi na yana sakafu ya vumbi.
Kadhalika, mwaka ujao utakuwa wa kwanza wa kupokea wanafunzi kidato cha kwanza
waliodahiliwa darasa la kwanza kwa mpango wa elimumsingi bila ada. Jambo hili
lisipoangaliwa mapema litakuja kusababisha wanafunzi kuchaguliwa kujiunga
kidato cha kwanza na kukosa pa kwenda hadi miundombinu ijengwe kwa zimamoto. Kwa hatua ya maendeleo nchi yetu iliyofikia katika sekta
mbalimbali, hali hii haipendezi na haitakiwi kuendelea. Kujenga miundombinu
ya shule zetu kwa kusubiri irushwe kwenye mitandao ya kijamii ndio tuone
inatutia aibu, au kusubiri watoto wakose pa kwenda au wakose pa kukaa ndipo
tukimbizane na kufukuzana, ni ishara ya kutopanga vizuri. Hili tusingependa
liendelee kuwepo.
85. Mheshimiwa Spika, kila mwaka kuna wanafunzi kati ya asilimia 15 - 20
wanatoka kwenye mfumo wa elimu kwa kutoendelea na kidato cha kwanza kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo kupata ujauzito, utoro na hali ngumu ya maisha.
Ukosefu wa mpango wa kugharamia mahitaji ya sekta ya elimu ndiyo chanzo cha
tatizo hili.
86. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa elimu ya juu, zaidi ya wanafunzi 11,000
wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu ambao tayari walishapata udahili katika
vyuo mbalimbali walikosa mikopo. Naongelea mkopo, sio fedha ya bure, bali ni
mkopo ambao ataurejesha. Katika jamii nyingi za kitanzania, mtoto akikosa mkopo
huku akiwaona wenzake wanaendelea, inamfadhaisha sana. Ni mfadhaiko kwake na
familia nzima. Kwa hatua ya maendeleo ambayo nchi yetu imepata katika sekta mbalimbali
hali hii haipendezi na haitakiwi kuendelea. Serikali inakusudia kuchukua hatua
za kuhakikisha kuwa inaongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ili kuwanufaisha
vijana wote wenye sifa za kupata mkopo.
v.
Miradi ya Kielelezo ya Bwawa la Kufua Umeme wa Maji
la Mwalimu Nyerere na Reli ya Kisasa
(SGR)
87. Mheshimiwa Spika, Miradi ya bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere na
Reli ya Kisasa (SGR) sio tu ni miradi ya kielelezo bali ni miradi “mama” kwa
kila mtanzania. Ni miradi inayoashiria uhuru wa nchi yetu, ni miradi inayoashiria
kujitegemea kwa nchi yetu, ni miradi inayoashiria heshima ya mtanzania na
inajengwa na mtanzania. Kama alivyosema Mheshimiwa Rais, kutokamilika kwa
miradi hii itakuwa laana kwa Taifa letu. Hatutajengewa miradi hii na mtu
yeyote, tutawaenzi wabeba maono wa miradi hii kwa kujenga na kuikamilisha.
Mwalimu Nyerere alibeba maono ya miradi hii, Rais Magufuli alianzisha miradi hii,
Rais Samia anakwenda kuijenga miradi hii. Niwahakikishie watanzania hapatakuwepo
GOFU hata la Mradi mmoja wala kusimama kwa mradi unaotekelezwa hata kwa mwezi
mmoja.
88.
Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na maeneo mahsusi
hayo niliyotangulia kuyasema, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria
zifuatazo:
a.
Sheria ya Ushuru wa Barabara na
Mafuta, SURA 220
Kufanya
marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta kama ifuatavyo:
(i) Kuongeza Ushuru wa barabara kwa shilingi
100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli;
(ii)
Kufanya
marekebisho ya kifungu cha 4 A(a) cha sheria ili kuelekeza fedha
zitakazokusanywa kutokana na ongezeko la ushuru wa barabara na mafuta la
shilingi 100 kwa aina zote za mafuta ziwe kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa
barabara za vijijini kupitia TARURA.
Hatua hii ya marekebisho
ya Sheria inatarajiwa kuongeza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 322,158.20.
b.
Sheria ya Petroli, SURA 392
Kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Petroli ili kuongeza tozo ya Mafuta ya Taa kutoka shillingi
150 hadi shillingi 250. Lengo la hatua hii ni kupunguza uchakachuaji wa mafuta
kufuatia ongezeko la ushuru wa mafuta kwenye dizeli na petroli.
c.
Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, SURA 306
Kufanya marekebisho
kwenye Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki kama ifuatavyo:
(i)
Kutoza tozo ya shillingi
10 hadi shilingi 10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa. Kiasi cha
tozo kinatofautiana kulingana na thamani ya muamala wa fedha unaotumwa au
kutolewa. Pendekezo hili litaongeza mapato ya Serikali kiasi cha shillingi milioni 1,254,406.14;
na
(ii)
Kutoza kiasi cha shilingi
10 hadi shilingi 200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa
kuongeza salio kwa watumiaji. Pendekezo hili litapelekea kuongeza mapato ya
Serikali kiasi cha shillingi milioni
396,306.0.
d.
Sheria ya
Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
Kutokana na vinywaji vikali kuwa na kiwango
kikubwa cha kilevi, napendekeza kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 30 ili
kuwa na uwiano wa viwango vya kodi kati ya Vinywaji kali na Bia. Hatua hii
inatarajia kuiongezea mapato
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni
60,769.35.
Utekelezaji wa hatua hizi nne kwa pamoja unatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa
kiasi cha shilingi milioni 2,033,639.66.
U.
Tarehe ya Kuanza
Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi.
89.
Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kikodi zinazopendekezwa zitaanza
kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2021, isipokuwa
pale itakapoelezwa
vinginevyo. Aidha, Marekebisho hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na Matangazo ya Serikali
(Government Notices).
V. Njia Mbadala za Kutekeleza Miradi Mikubwa
90.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2020 nchi yetu ilifanikiwa kuingia
katika kundi la nchi zenye kipato cha kati cha chini (Lower Middle-Income
Country). Kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati kunaifanya nchi
yetu kutakiwa kujiendesha kiuchumi bila kutegemea kwa kiwango kikubwa misaada
na mikopo yenye masharti nafuu ambayo, hupewa nchi zenye kipato cha chini.
Hivyo, ni lazima Serikali iboreshe mbinu inazotumia na kubuni mbinu mpya za
kupata mapato. Katika kutekeleza hatua hii, Serikali imeanza kufanya uchambuzi
wa vyanzo mbadala vya rasilimali fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama
vile ufadhili mchanganyiko (Blended Finance). Wafadhili wanaotoa
aina hii ya ufadhili hutoa fursa kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania,
kurekebisha au kujumuisha (restructuring or consolidation) deni lake kwa
makubaliano ya kutumia sehemu ya malipo ya deni katika uhifadhi wa mazingira au
kuimarisha sekta za kiuchumi na kijamii.
91. Mheshimiwa
Spika, Katika mwaka 2021/22, Serikali inadhamiria kukamilisha mchakato
wa Tathmini na Ukadiriaji wa Kukopesheka kwa Nchi (Sovereign Credit Rating).
Hatua hii inalenga kutuwezesha kujua nafasi yetu katika
masoko ya fedha ya kimataifa na jinsi wakopeshaji wanavyotuona hasa katika
uwezo wa kusimamia uchumi na kulipa madeni yetu. Hatua hiyo itatuwezesha pia
kuongeza wigo wa wakopeshaji ambao wako tayari kutukopesha, hususan katika Masoko
ya Mitaji ya Kimataifa (International Capital Markets). Serikali itaanza
mara moja mchakato wa wazi wa kutekeleza na kukamilisha kazi ya Sovereign
Credit Rating ndani ya mwaka 2021/22.
92. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kupanua wigo wa vyanzo vya
rasilimali fedha, Serikali itaangalia uwezekano wa kutumia Hati Fungani zitakazotolewa na Halmashauri za Manispaa
na Majiji kama njia mbadala ya kupata rasilimali fedha kwa ajili ya miradi ya
kimkakati. Hatua hii itapunguza mzigo kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali
hasa kwa Halmashauri zenye miradi ambayo imefanyiwa upembuzi yakinifu na kuwa
na uhakika wa uwezo wa miradi hii kujiendesha kwa faida (bankable projects).
Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (United
National Capital Development Fund - UNCDF) na Mamlaka ya Usimamizi wa
Masoko ya Mitaji (Capital Markets and Securities Authority - CMSA)
imeanza mchakato wa kuhakikisha kwamba Halmashauri, Manispaa na Majiji
yatakayokidhi vigezo na masharti ya matumizi ya Hati Fungani hizi yanaanza
kutumia utaratibu huu.
93. Mheshimiwa Spika, Serikali inaona umuhimu wa kutumia Masoko ya Hati
Fungani za Kimataifa maarufu kama “Eurobonds” ikiwa ni chanzo cha
kuaminika na thabiti cha kugharamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia Mkakati
wa Deni la Muda wa Kati (Medium Term Debt Strategy - MTDS). Hatua hii
inakwenda sambamba na hatua nyingine inayopendekezwa katika hotuba hii ya
kufungua soko la dhamana za Serikali ili kuruhusu wawekezaji wa nje ya Tanzania
na Afrika Mashariki kununua hati fungani zetu ili kuongeza ukwasi katika soko
la ndani.
94.
Mheshimiwa Spika, Soko la Eurobond ulimwenguni linakadiriwa kuwa na
zaidi ya dola za Marekani trilioni 30 zilizotolewa kwa nchi zinazotafuta
rasilimali fedha kwa njia ya mikopo kutoka kwenye masoko ya kimataifa yenye
ukwasi mkubwa ili kugharamia miradi ya maendeleo. Njia hii pia hutumiwa na
mashirika ya kimataifa kama Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika wanapotafuta
fedha kwa ajili ya kufadhili miradi yao kote duniani. Aidha, nchi mbalimbali za
kusini mwa Jangwa la Sahara zinazofanya vizuri kiuchumi zimekuwa zikitumia Soko
la eurobond kama chanzo thabiti na chenye masharti rafiki katika
kugharamia utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo. Tanzania itahitaji kufanyiwa
tathmini ya kukopesheka ili kufikia masoko ya mitaji ya kimataifa kupitia eurobonds.
Hivyo, zoezi la kukadiria au kutathmini kukopesheka kwa Tanzania ni hatua isiyoepukika.
95. Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2010 tulipopitisha Sheria ya PPP hatujapata mafanikio ya
kujivunia katika eneo hili pamoja na faida kubwa na nyingi ambazo Taifa linaweza
kupata kupitia mfumo wa PPP hasa katika miradi mikubwa inayohitaji fedha nyingi
na utaalamu kutoka sekta binafsi. Utekelezaji wa miradi ya PPP hupunguza mzigo
kwenye deni la Serikali na hata katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali na hutoa
nafuu ya kibajeti (Fiscal Space) kwa kuiwezesha Serikali kutekeleza
majukumu mengine ambayo hayawezi kugharamiwa na sekta binafsi. Hivyo, ni muhimu
kutumia PPP kwenye miradi mbalimbali inayokidhi Sheria ya Ubia baina ya Sekta
ya Umma na Sekta Binafsi, Sura 103.
96.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia manufaa ya PPP, Serikali itaongeza kasi ya kushughulikia
miradi ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ikiwa ni pamoja na: Ujenzi wa viwanda
vya dawa muhimu na vifaa tiba; ujenzi wa Hoteli ya Nyota Nne na Kituo
Changamani cha Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere; ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika mikoa ya Dar es
Salaam, Lindi na Mtwara; na ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza simu za mkononi
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Aidha, wananchi na wawekezaji
wengine wanaalikwa kubainisha maeneo ambayo wanaweza kushiriki katika
utekelezaji wa miradi ya PPP kulingana na uwezo wao wa mitaji na utaalamu.
V.
SURA YA BAJETI KWA MWAKA
2021/22
97.
Mheshimiwa Spika, kwa
kuzingatia shabaha, malengo pamoja na sera za bajeti kwa mwaka 2021/22, Sura ya
Bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi trilioni 36.33 zinatarajiwa kukusanywa
na kutumika. Mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 26.03, sawa na
asilimia 71.7 ya bajeti yote. Kati ya mapato hayo, mapato ya kodi ni shilingi
trilioni 22.18, sawa na asilimia 13.5 ya Pato la Taifa. Aidha, Serikali
inalenga kukusanya mapato yasiyo ya kodi ya shilingi trilioni 2.99 na mapato
kutoka vyanzo vya Halmashauri shilingi bilioni 863.9.
98. Mheshimiwa Spika, Washirika wa Maendeleo wanatarajia kuchangia misaada na
mikopo nafuu yenye jumla ya shilingi trilioni 2.96, sawa na asilimia 8.1 ya
bajeti yote. Kiasi hicho kinajumuisha fedha za miradi ya maendeleo shilingi
trilioni 2.67 na Mifuko ya Pamoja ya Kisekta shilingi bilioni 282.3. Napenda
kuwashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea kutoa fedha za misaada na
mikopo nafuu ili kufanikisha miradi na programu mbalimbali za maendeleo zitakazotekelezwa
katika bajeti ya mwaka 2021/22.
99.
Mheshimiwa Spika, kipekee ningependa kuwatambua Washirika wetu wa Maendeleo kama ifuatavyo:
Serikali za Canada, China, Denmark, Finland, India, Ireland, Italia, Korea ya
Kusini, Japan,Ufaransa, Ujerumani, Norway, Poland, Ubelgiji, Uholanzi, Uswisi,
Uingereza, Sweden na Marekani. Vilevile, kuna Mashirika ya Kimataifa ambayo ni
Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya
Kiuchumi katika Afrika, Mfuko wa Abu Dhabi, Mfuko wa Kuwait, Mfuko wa kimataifa
wa kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi, kifua kikuu na malaria, Umoja
wa Ulaya, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Umoja wa mataifa na mashirika yote
yaliyopo chini yake, Mfuko wa OPEC kwa Maendeleo ya Kimataifa, Mfuko wa
Mazingira, pamoja na Shirikisho la GAVI. Ninapenda pia kuyatambua Mashirika
yasiyo ya Kiserikali ya ndani na nje pamoja na mashirika ya ufadhili - philanthropies
kwa misaada yao kwenye sekta mbalimbali.
100.
Mheshimiwa Spika, Serikali
inatarajia kukopa shilingi trilioni 7.34 kutoka soko la ndani na nje kwa
masharti ya kibiashara. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 4.99 ni mikopo
ya ndani ambayo inajumuisha shilingi trilioni 3.15 kwa ajili ya kulipia
hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na shilingi trilioni 1.84 kwa
ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Aidha, shilingi trilioni 2.35
zinatarajiwa kukopwa kutoka soko la nje kwa lengo la kuongeza kasi katika
utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
101.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka
2021/22, Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 36.33 kwa
matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 23.0
zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 13.33 kwa
ajili ya matumizi ya maendeleo. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya
kawaida zinajumuisha shilingi trilioni 10.66 kwa ajili ya ulipaji wa deni la
Serikali, shilingi trilioni 8.15 kwa ajili ya mishahara na shilingi trilioni
4.19 kwa ajili ya matumizi mengineyo. Aidha, Serikali imetenga jumla ya
shilingi bilioni 200.0 kwa ajili ya kulipa madeni yaliyohakikiwa ya watumishi,
wazabuni na watoa huduma.
102.
Mheshimiwa Spika, jumla ya shilingi trilioni 13.33 zimetengwa kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo, sawa na asilimia 37 ya bajeti yote. Kati ya kiasi hicho,
fedha za ndani ni shilingi trilioni 10.37 na fedha za nje shilingi trilioni
2.96. Aidha, fedha za maendeleo zinajumuisha, shilingi trilioni 1.19 kwa ajili
ya miradi ya reli ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa;
shilingi trilioni 2.08 kwa ajili ya miradi ya barabara, ujenzi wa madaraja, na
viwanja vya ndege; shilingi trilioni 2.34 kwa ajili ya miradi ya kuzalisha,
kusafirisha na kusambaza umeme ikiwemo mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius
Nyerere; shilingi bilioni 589.4 kwa ajili ya miradi ya maji mijini na vijijini;
shilingi bilioni 233.3 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na
vitendanishi; shilingi bilioni 500 ni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu
ya juu; shilingi bilioni 215.6 kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2022; na shilingi bilioni 312.1 kwa ajili ya elimumsingi bila
ada. Aidha, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 400.0 kwa ajili ya
kulipa madeni yaliyohakikiwa ya miradi ya maendeleo.
103.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mfumo wa bajeti kama nilivyoeleza, sura ya bajeti kwa mwaka 2021/22 ni kama inavyooneshwa katika Jedwali
Na. 2.
Jedwali Na. 2: Mfumo wa Bajeti ya Mwaka 2021/22
VI.
HITIMISHO
104.
Mheshimiwa Spika, ninapoelekea
mwisho wa hotuba hii, napenda
kumshukuru kwa dhati “MAMA YETU” kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Fedha na Mipango. Ninamuahidi
Mheshimiwa Rais, Waheshimiwa wabunge na Watanzania wote kwamba, nitaibeba
dhamana hii kwa uadilifu, weledi na uwezo wangu wote na ninamuomba Mwenyezi
Mungu anijalie afya njema, hekima na busara katika kutekeleza majukumu hayo. Naomba
nielezee masuala machache muhimu kabla ya kuhitimisha hotuba hii.
105.
Mheshimiwa Spika, kwanza natoa
pongezi kwa “MAMA YETU” kwa matumaini makubwa aliyowapa watanzania. “MAMA YETU”
ameonesha ni Kiongozi
Makini, ni Kiongozi Shupavu, ni Kiongozi Mchapa
Kazi, ni Kiongozi Mwadilifu, ni Kiongozi Msikivu, ni Kiongozi aliye na dira
thabiti na maono ya kuendelea kuiletea nchi yetu maendeleo makubwa. Ameweka wazi kuwa hataki kodi ya
dhuluma, hataki kuendesha Serikali kwa mapato ya dhuluma, ameweka wazi kusimama
imara kwenye masuala ya mapato na matumizi ya Serikali, ameweka
wazi kuwa atakuwa imara kwenye vita dhidi ya rushwa.
106.
Mheshimiwa Spika, kwa kauli hizo
“MAMA YETU” ameonesha kuwa, kukaa kwake katika nafasi mbalimbali katika Serikali za
awamu mbalimbali SMT na SMZ kumemfanya awe kiongozi aliyeandaliwa na KUIVA na
aliye tayari kuiongoza nchi kwa ufanisi mkubwa. Itakumbukwa mbali na nafasi
zingine nyingi alizoshika katika miaka yake takribani ishirini Serikalini, MAMA
YETU amekuwa Waziri katika Awamu ya Nne na amekuwa Makamu wa Rais katika Awamu
ya Tano. “Kuna style za uongozi amejifunza”.
107.
Mheshimiwa Spika “kuna style
za uongozi amejifunza” kupitia Awamu hizo
alikopewa nafasi kuhudumu katika nafasi mbalimbali. “MAMA YETU” alikuwa Waziri katika awamu
ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete. Mheshimiwa Kikwete alikuwa Mzalendo wa kweli, alikuwa na maono (Visionary Leader), alikuwa mwalimu, alikuwa mzazi,
alikuwa mlezi na kiongozi, alikuwa rahim sana,
alikuwa mvumilivu sana aliyeamini kwenye Mifumo, Taasisi na Utendaji wa
Kitaasisi. Hii naweza kuifananisha kama “Refa kwenye mchezo” wa mpira
wa miguu, ambaye anachezesha mechi zake akiwa na “kadi ya njano tu”, kadi
nyekundu anaiacha nyumbani. Ukicheza rafu mara ya kwanza anakuonya kwa
kukuelekeza, ukicheza rafu mara ya pili anakupa kadi ya njano, ukikosea anakupa
kadi ya njano tena na alipotakiwa kutoa kadi nyekundu mara nyingi alionya kwa
mdomo, kwa kuwa kadi nyekundu alikuwa anaiacha nyumbani. Rais Kikwete aliamini
sana kwenye Mifumo na Utendaji wa Kitaasisi. Kwa mtazamo wangu, jinsi “MAMA
YETU” alivyoanza ni dhahiri amepata funzo kwenye awamu hiyo ikiwemo funzo la
Uzalendo, maono na kuamini kwenye “Mifumo, Taasisi na Utendaji wa Kitaasisi”,
na hapa naweza kusema ameichukua “kadi ya njano”, anayo na
ameanza kutumia kama mnavyoona.
108.
Mheshimiwa Spika, “MAMA YETU” alikuwa
Makamu wa Rais katika awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Rais Magufuli alikuwa mzalendo
wa kweli, alikuwa na Maono (Visionary Leader), alijitoa kwa nguvu zote (Dedicated),
alikuwa na uthubutu sana, mtu wa vitendo sana na muumini wa matokeo na
kuchukua hatua za papo kwa papo. Kama refa wa mchezo wa mpira wa miguu,
alikuwa akienda kuchezesha Mechi zake akiwa na “kadi
nyekundu tu”, kadi ya njano alikuwa
anaiacha nyumbani. Ukicheza rafu mara ya kwanza tu anakupa kadi nyekundu,
wakati mwingine hata asipoiona rafu yeye, mchezaji au shabiki akisema ameona
rafu anakupa kadi Nyekundu (no nonsense), hata mimi mwenyewe
niliwahi kutembelewa na kadi nyekundu nikakosa michezo kadhaa. Hayati
Dkt. Magufuli aliamini kwenye nidhamu ya hali ya juu ya mchezo. “MAMA
YETU” alikuwa Line one na Mheshimiwa Majaliwa akiwa Line
two. Hivyo, “MAMA YETU” amepata mafunzo kwenye awamu hiyo ya Uzalendo, Uthubutu, mtu wa vitendo
kuamini kwenye matokeo na nidhamu kazini na ameichukua “kadi ya nyekundu”.
109.
Mheshimiwa Spika
“kuna style za uongozi amejifunza”. “MAMA YETU” anazo kadi zote, “kadi ya
njano” na “kadi nyekundu”. MAMA YETU” ni Mzalendo wa kweli, ni
Mwadilifu sana, ana Uthubutu, ana Maono, anaamini kwenye “Mifumo,
Taasisi na Utendaji wa Kitaasisi”, hataki maneno anataka vitendo.
Nitoe rai kwa watumishi wote wa umma na watanzania kwa ujumla tuchape kazi kwa
bidii, kwa uadilifu na uzalendo mkubwa. Kwa watumishi wa umma tusimamie matumizi
ya fedha za walipa kodi kwa uadilifu mkubwa na kwa watanzania tulipe kodi bila
shuruti. Tabia moja ya refa asiyependa kuonea upande wowote, huwa hawezi
kupendelea upande wowote. Kwenye michezo ya mieleka huwa mnapewa tahadhari ya don’t
try this at home, kwenye maslahi ya nchi wanaotaka kumjaribu MAMA YETU
nawaonya “Don’t try at all”. Tujiepushe na kadi Nyekundu.
110.
Mheshimiwa
Spika,
lazima tujenge utamaduni wa kuheshimu
mali na rasilimali hapa nchini (mali za umma na mali binafsi). Kwa upande wa
mali za umma, lazima tutangulize uzalendo na uadilifu tunapotekeleza majukumu
yetu. Serikali inapoteza fedha nyingi kwenye kutekeleza Sheria ya Ununuzi wa
Umma kwa kutojali thamani ya fedha kwenye miradi. Watumishi wa Serikali wasio
waaminifu wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuongeza
gharama za miradi ikilinganishwa na gharama halisi ingawa wanafuata taratibu
zote za ununuzi. Taratibu za ununuzi zinapokamilika, watumishi na wafanyabiashara hawa hugawana fedha na
kiasi kidogo tu kilichosalia ndicho kinaelekezwa kwenye mradi husika na
hatimaye kupata mradi ulio chini ya kiwango. Ukiwafuatilia kisheria hupati moja
kwa moja pa kuwashika, hivyo wanakuwa wameiba kwa kuzingatia sheria. Nawaelekeza wote wanaohusika na ununuzi wa umma kuzingatia
sheria, taratibu, kanuni na kutanguliza mbele uzalendo na uadilifu.
Serikali itachukua hatua za makusudi katika kuimarisha usimamizi wa sheria na
taratibu za ununuzi.
111.
Mheshimiwa
Spika,
kwa upande wa mali binafsi, ni lazima
tuheshimu biashara zetu na mali zinazotokana na biashara hizo. Kuna hatua
tunazozifanya sekta zote za umma na binafsi zinadumaza uchumi wetu. Kwa mfano,
kuna tabia ya kutolipa madeni kwenye benki zetu, jambo ambalo linapunguza uwezo
wa benki kutoa mikopo kwa watu wengine. Aidha, wapo watu wengine ambao wakidaiwa
kwa makusudi ya kuchelewesha malipo wanakimbilia mahakamani. Tusitumie vibaya
vyombo vyetu vya sheria. Vilevile, kuna baadhi ya wakopeshaji ambao hawaheshimu
mali za wateja wao. Mfano, mteja anakuwa amelipa sehemu kubwa ya mkopo wake
lakini ikitokea mkopeshaji, rafiki au dalali akaipenda dhamana iliyowekwa, hufanya
njama ya kupiga mnada dhamana hiyo kwa bei isiyolingana na thamani ya dhamana
au sehemu ya deni iliyobaki sio hata robo ya dhamana hiyo. Natoa wito kwa
vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia kila eneo panapokuwa na minada kwenye
sekta binafsi na hata sekta ya umma na pale patakapoonekana kuwepo kwa njama za
kudhulumu wamiliki wa mali au kuchepusha sehemu ya mali zinazouzwa kwa mnada
hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.
112.
Mheshimiwa Spika,
Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea
kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Kuna wanaodhani tunapoongelea kukusanya kwa
weledi, sheria na haki wanachukulia tutaacha kukusanya kodi. Nataka nisisitize
kuwa, tutakusanya Mapato ya Serikali. Tutakusanya Mapato ya Serikali. Tutakusanya
Mapato ya Serikali. Nitoe rai kwa watumishi wote wa Serikali wanaohusika na
kukusanya kodi, maduhuli na ushuru kuelewa vizuri maelekezo haya kwa kuzingatia
sheria, weledi na kutenda haki kama Mheshimiwa Rais alivyoelekeza. Nimeanza kusikia visingizio kila kona, mara
mfumo, mara mtandao mara EFD haifanyi kazi. Kwa watoza kodi na walipakodi
wote visingizio hivi vitaturudisha kwenye ukaguzi. Tusiwekeze kwenye kusaidiwa
kukwepa kodi bali tusaidiwe kwenye kufuata sheria. Akiwepo mtumishi akakusaidia
kukwepa kodi nawe ukampa asante unatengeneza tatizo tu sio unafuu kwani kuna
siku utakuja kukaguliwa huku aliyekusaidia akiwa amehamishwa au kuachishwa kazi.
Nitumie fursa hii kumwelekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato kuweka watu
mahususi wa kufanya doria kila kona, nchi nzima kuangalia mwenendo wa matumizi
sahihi ya EFD na mifumo mingine ya malipo kuwa muda wote inafanya kazi.
113.
Mheshimiwa
Spika,
tutasimamia nidhamu katika matumizi. Tutasimamia
nidhamu katika matumizi. Tutasimamia nidhamu katika matumizi na tutaendeleza
mapambano dhidi ya Rushwa na Ufisadi. Nazijua mbinu zote za udanganyifu,
nazijua njia zote za majizi na watakaoendelea na tabia za kudokoadokoa fedha za
walipa kodi, nitawashukia kama mwewe. Kazi inaendelea, watanzania endeleeni
kumwamini Mheshimiwa Rais wetu, yuko macho na wasaidizi wake tuko macho,
tutapambana na MCHWA wote, kuna mengine mnayasikia, kuna mengine mnayaona na
mengine hata hamyaoni, yote tunaendelea kuyafanyia kazi kwa maelekezo thabiti
na ya kizalendo ya Mheshimiwa Rais wetu. Kinyiramba kuna msemo usemao “MWINDA
KANGA HAPIGI YOWE.”
114.
Mheshimiwa Spika, tuendeleze kwa
kasi na kukamilisha miradi ya kimkakati ambayo inalenga kukuza uchumi,
kuimarisha huduma za jamii na kuongeza fursa za ajira, hususan ajira kwa
vijana. Tutakamilisha ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere, tutaendelea
na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) mpaka itakamilika, tutamalizia ujenzi wa barabara
zinazounganisha mikoa zilizosalia, tutakamilisha ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi
na madaraja mengine kuwaunganisha wananchi wetu, tutaendelea na usambazaji wa
umeme kutoka kila kijiji kwenda kila kitongoji na hatimaye kila nyumba.
115.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya Jiji la Dodoma na kulifanya
kuwa la kisasa. Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa
ofisi za wizara na taasisi zake katika mji wa Serikali Mtumba; kujenga barabara
za mzunguko; na kuboresha miundombinu ya maji. Aidha, Serikali itaanza ujenzi
wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika eneo la Msalato.
116.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa
Rais amenituma niwahakikishie watanzania kupitia hotuba hii kuwa, tunaendelea kuijenga nchi, tunaendelea kuijenga
nchi, ije mvua, lije jua, tunaendelea kuijenga nchi, uwe usiku au mchana,
tunaendelea kuijenga nchi. Hakuna mradi hata mmoja
utakaokwama, wala hakuna Sekta ya maendeleo itakayozorota. “KAZI INAENDELEA.”
117.
Mheshimiwa
Spika, nampongeza Dkt. Philip Isdor
Mpango aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais na
kuthibitishwa na Bunge kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, napenda kumpongeza kwa
dhati kwa kazi nzuri aliyoifanya katika usimamizi wa uchumi kama Waziri wa
Fedha wa Serikali ya Awamu ya Tano ulioiwezesha nchi yetu kuingia katika kundi
la nchi za hadhi ya uchumi wa kipato cha kati cha chini. Vilevile, nampongeza
kwa kazi nzuri iliyotukuka katika kuisimamia Wizara ya Fedha na Mipango ambayo
kwa hakika imeweka msingi mzuri wa utekelezaji wa majukumu yangu.
118.
Mheshimiwa
Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa
Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuchaguliwa na wananchi wa Zanzibar kuwa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mhe Rais
Mwinyi, ameanza kazi vizuri sana na kuwapa matumaini mapya wananchi wa Zanzibar
katika kukuza uchumi na maendeleo hasa kwa kuwekeza kwenye “Blue Economy”.
119.
Mheshimiwa
Spika,
napenda kumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Mbunge wa Jimbo la
Ruangwa kwa kuteuliwa na kuthibitishwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Nampongeza kwa uongozi wake hodari ndani ya Serikali na
hapa Bungeni pamoja na kuendelea kumsaidia Mheshimiwa Rais kufuatilia kwa
karibu utekelezaji wa ahadi zilizomo katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025.
120.
Mheshimiwa Spika, naomba niwapongeze wakuu wa mihimili mingine
ya Dola kwa usimamizi na uongozi shupavu, nikianza na wewe Mheshimiwa Job
Yustino Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa
Jimbo la Kongwa na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Naibu Spika na Mbunge wa Jimbo
la Mbeya Mjini kwa kuongoza Bunge hili kwa umahiri na busara. Aidha, nampongeza
Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamisi Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania kwa uongozi makini
wa Mhimili wa Mahakama unaozingatia, miiko,dira na dhima ya mhimili huo. Hakika
uongozi wake umefanikisha upatikanaji wa HAKI kwa wanyonge na kujenga misingi
imara ya utawala wa sheria hapa nchini.
121.
Mheshimiwa Spika, niruhusu pia kumpongeza
Mheshimiwa Balozi Hussein Athman Kattanga kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu
Kiongozi ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Mawaziri na Mkuu wa Utumishi wa
Umma. Nampongeza kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa umakini na kwa
weledi mkubwa. Vilevile, nawapongeza Mheshimiwa Othman Masoud Othman kwa
kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na
Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
122.
Mheshimiwa
Spika, napenda niwapongeze na kuwashukuru kwa dhati
wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na Usalama. Kipekee, naomba niwatambue Mkuu wa
Majeshi, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo; Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon
Nyakoro Sirro; Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Diwani Athuman Msuya; Kamishna
Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee; Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala; Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa, CP Salum Hamdun; Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kuzuia na
Kupambana na Madawa ya Kulevya, Gerald Kusaya Musabila; na Kamishna Jenerali wa
Zimamoto na Uokoaji, John William Masunga. Utumishi wao uliotukuka na uzalendo
wa hali ya juu umetuwezesha kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii na
kiuchumi kwa amani Tunawaomba muendelee kutimiza wajibu wenu wa kulinda amani
na usalama wa nchi yetu kwa moyo wa uzalendo.
123.
Mheshimiwa
Spika, kwa moyo wa dhati napenda
kuipongeza na kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti chini ya uongozi
thabiti wa Mheshimiwa Sillo Daniel Baran, Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na
Makamu wake Mheshimiwa Omar Mohamed Kigua, Mbunge wa Jimbo la Kilindi, kwa
umakini wao katika kuchambua na kutoa maoni na ushauri ambao umesaidia
kuboresha mapendekezo ya Bajeti hii. Aidha, ninawapongeza Wenyeviti, Makamu Wenyeviti
na Wajumbe wa Kamati zote za Kudumu za Bunge za Kisekta kwa michango waliyotoa
kupitia vikao vya Kamati za Kisekta iliyowezesha kuboresha makadirio ya mapato
na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2021/22.
124.
Mheshimiwa Spika, ninawashukuru viongozi na watumishi wenzangu
wa Wizara ya Fedha na Mipango na taasisi zake kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa
katika kutekeleza majukumu yangu ya kila siku hususan maandalizi ya bajeti hii.
Kipekee ninamshukuru Mheshimiwa Hamad Y. Masauni, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni. Ninamshukuru sana Katibu Mkuu Hazina na
Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel M. Tutuba, pamoja na Naibu Makatibu
Wakuu, Amina Kh. Shaaban, Adolf H. Ndunguru na Dkt.
Khatibu M. Kazungu pamoja na watumishi wa kada zote wa Wizara ya
Fedha na Mipango. Aidha, ninamshukuru Profesa Florens D. Luoga, Gavana wa Benki
Kuu ya Tanzania kwa kusimamia sekta ya fedha kwa weledi mkubwa.
125.
Mheshimiwa Spika, namshukuru Ndugu Alphayo J. Kidata, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kwa kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi
mkubwa. Kadhalika, namshukuru CPA
Charles E. Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kazi
nzuri anayoifanya ya kukagua na kutoa taarifa za matumizi ya fedha za umma kwa
wakati pamoja na kuishauri Serikali. Ninamshukuru CPA Athumani S. Mbuttuka,
Msajili wa Hazina kwa kuendelea kusimamia Mashirika ya Umma na kuhakikisha
Serikali inapata mchango na gawio stahiki. Ninamshukuru pia Dkt. Albina Chuwa,
Mtakwimu Mkuu wa Serikali kwa kusimamia vizuri Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
na kuendelea na maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.
126.
Mheshimiwa Spika,
nawapongeza Mawaziri wenzangu na Naibu Mawaziri wote walioaminiwa na kuteuliwa
na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwenye nyadhifa hizo. Aidha, niwapongeze pia wabunge wenzangu wote wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuaminiwa na vyama vyao na kuchaguliwa na
wananchi ili kuwawakilisha bungeni. Kwa moyo wa dhati napenda kumshukuru mke
wangu mpenzi Bi Neema Nchemba, kwa kunitia moyo na kuniombea wakati wote
ninapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yangu. Vile vile, nitumie fursa hii
kuwashukuru kwa dhati wapiga kura wangu wa Jimbo la Iramba Magharibi
walioniamini na kunichagua tena kwa kishindo kuwa Mbunge wao. Ninawaahidi kuwa
sitawaangusha.
127.
Mheshimiwa Spika, niwashukuru wafanyabiashara na wananchi wote ambao wameendelea kulipa
kodi kwa hiari. Rai yangu kwao ni kuwa, tukitumia rasilimali za nchi yetu
vizuri na kufanya kazi kwa umoja na bidii, tutaifanya Tanzania kuwa kitovu cha
uchumi na biashara sio tu kwa ukanda wa Afrika Mashariki bali kwa Afrika nzima.
Vile vile, navishukuru vyombo vyote vya habari kwa kuendelea kutoa elimu kwa
umma kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya Taifa letu.
128.
Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru viongozi wa dini kwa sala na
dua zao zilizotuwezesha kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
kwa amani na utulivu. Aidha, nawashukuru kwa kuliombea Taifa katika kipindi
kigumu tulichopitia cha kuondokewa na viongozi wa kitaifa pamoja na mlipuko wa
homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya korona. Sala na dua zao
zimetuwezesha kupita kwa amani katika kipindi cha mabadiliko ya uongozi wa
kitaifa na hatimaye kumpata Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan. Ninawasihi waendelee kuliombea Taifa letu bila kuchoka.
129.
Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa lakini si kwa umuhimu napenda nikushukuru wewe binafsi
kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha hoja hii na Waheshimiwa Wabunge wote kwa
kunisikiliza.
130.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
.
.
KIAMBATISHO NA. 5
MABORESHO
YA TOZO ZA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA
TOZO
BORESHWA ZA UPIMAJI KATIKA MAABARA
Na. |
VIPIMO |
TOZO ZA SASA KWA DOLA ZA
KIMAREKANI |
TOZO
ZA VIPIMO PENDEKEZWA KWA SHILINGI ZA KITANZANIA |
|
MAABARA
YA KEMIA |
||
1 |
Hydroquinone kwenye vipodozi |
435 |
150,000/= |
2 |
Kojiki asidi kwenye vipodozi |
435 |
150,000/= |
|
MAABARA YA CHAKULA |
||
3 |
Kiasi cha unyevu |
30 |
30,000/= |
4 |
Crude fibre |
55 |
30,000/= |
5 |
Acid insoluble ash |
55 |
30,000/= |
6 |
Protini |
55 |
60,000/= |
7 |
Asidi ya foliki |
65 |
50,000/= |
8 |
Madini joto |
60 |
30,000/= |
9 |
Total ash |
45 |
30,000/= |
10 |
Volatile oils |
55 |
30,000/= |
11 |
Sumukuvu |
120 |
150,000/= |
12 |
Aflatoxins |
225 |
150,000/= |
13 |
Kiasi cha chumvi |
35 |
30,000/= |
14 |
Chromate test |
25 |
30,000/= |
15 |
physical tests (kila moja) |
5 |
10,000/= |
16 |
Slip point (Melting point) |
25 |
30,000/= |
17 |
Acid value |
50 |
30,000/= |
18 |
Unsaponifiable matter |
50 |
30,000/= |
19 |
Peroxide value |
50 |
30,000/= |
20 |
Insoluble impurities |
25 |
30,000/= |
21 |
Soap content |
20 |
30,000/= |
22 |
Relative density |
10 |
20,000/= |
23 |
Refractive index |
10 |
20,000/= |
24 |
Saponification value |
50 |
30,000/= |
25 |
Rangi ( ICUMSA) |
30 |
20,000/= |
26 |
Ethyl alcohol (Ethanol) content |
25 |
30,000/= |
27 |
pH |
10 |
15,000/= |
28 |
Carbon dioxide |
20 |
20,000/= |
29 |
Polarisation |
25 |
30,000/= |
30 |
Water insoluble matter |
25 |
30,000/= |
31 |
Sulphated ash |
50 |
30,000/= |
32 |
Acidity |
25 |
30,000/= |
33 |
|