Habari za Punde

Rais wa Jahmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Amemteua Mhe. Balozi Batilda Buriani Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Bi Zuwena Jiri Kuwa Ras Mpya Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Juni 11,2021 amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa na kuteua wengine. Katika mabadiliko hayo , amemteua Bi. Batilda Salha Buriani kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi  ya Ally Hapi ambaye anahamia mkoa wa Mara  huku aliyekuwa Katibu Tawala wilaya ya Simanjiro, Zuwena Omari Jiri akiteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.


Mkuu wa Mkoa wa Mara , Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi anahamia Mkoa wa Mwanza ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila uteuzi wake umetenguliwa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.