Habari za Punde

Spika BLW aishauri Skuli ya Sheria kushirikiana na Tume ya kurekebisha Sheria

 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid akipokea kitabu cha sheria ya kuanzishwa Skuli ya Sheria Zanzibar kutoka kwa Mwenyekiti wa Skuli hiyo Dkt Ali Uki wakati alipofika ofisini kwa spika kwa ajili ya kujitambulisha.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid ameishauri Taasisi ya Skuli ya Sheria Zanzibar kushirikiana kwa karibu na tume ya kurekebisha sheria ili kusaidia kuwa na sheria bora zinazotekelezeka.

Mhe Zubeir ametoa ushauri huo ofisini kwake Chukwani wakati alipokutana na Mwenyekiti wa Skuli ya Sheria Zanzibar aliyefika kwa ajili ya kujitambulisha.

 Amesema kumekua na sheria mbali mbali zilizoanzishwa  lakini changamoto iliyopo ni katika utekeelzaji wake ambapo hupelekea sheria hizo kufanyiwa marekebisho kwa kipindi kifupi.

 Aidha amemuhakishia Mwenyekiti wa Skuli ya Sheria Zanzibar kuwa Baraza la Wawakilishi lipo tayari kusaidia kufanikisha katika kufikia lengo la kuanzishwa taasisi hiyo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.