Habari za Punde

Chama cha walimu waomba busara kutumika wakishughulikia mashauri ya Kada ya Ualimu

 
 Naibu Katibu Mkuu kutoka Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) Salim Ali Salim akitoa ufafanuzi  kwa Waandishi wa habari juu ya tukio lilotokea katika Skuli ya Sunni Madrasa iliyopo Mkunazi Mkoa wa Mjini Magharibi, wa kwanza (kulia) ni Afisa Jinsia kutoka Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) Shuwena Faki Haji hafla iliyofanyika katika Ofisini za Chama hicho Kijagwani Mjini Unguja.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiskiliza Ufafanuzi uliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu kutoka Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) Salim Ali Salim (hayupo pichani) juu ya tukio lilotokea katika Skuli ya Sunni Madrasa iliyopo Mkunazi Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika katika Ofisini za Chama hicho Kijagwani Zanzibar.

Na Kijakazi Abdalla Maelezo 

Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU),wameziomba mamlaka zinazosimamia makosa ya kinidhamu kutumia busara wakati wakishughulikia mashauri ya kada ya ualimu. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za chama hicho, huko Kijangwani Mjini Unguja, Naibu Katibu Mkuu wa ZATU, Bwana Salim Ali Salim kufuatia tukio la kupigwa kwa Mwalimu wa Skuli ya Sunni Madrasa na mzee wa mwanafunzi anayesoma katika Skuli hiyo. 

Amesema kua walimu ni washirika wakubwa wa kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora ili kuona taifa linapata wasomi wazuri. 

Amesema kufuatia kwa kupigwa kwa Mwalimu Chama cha Walimu Zanzibar, kimeiomba Wizara ya Elimu Zanzibar inaposhughulikia migogoro ya walimu busara zitumikie ili kuepusha uhasama na kuharibu ufanisi wa kada ya uwalimu. 

Alieleza kuwa, Chama hicho kinasikitishwa kwa baadhi ya wazazi kuingia katika maeneo ya skuli na kuwashambulia walimu kwa kisingizio kuwa watoto wamepigwa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.