Mkoa wa Kaskazini Unguja
NA RAYA HAMAD – OMKR
Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia ofisi za viongozi wakuu wa
Kitaifa imetoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha kisiwa cha Mnemba kinalindwa, kinaenziwa
na kinaendelezwa licha ya kuwa Serikali kupitia ZIPA imetoa utaratibu wa
kukodishwa kwa visiwa vidogo vidogo
Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa Kitaifa Mhe
Hassan Hafidh ameyasema hayo walipofanya ziara ya kuangalia maeneo ya hifadhi
za mazingira na kushuhudia uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya
tabianchi pamoja na mwanadamu
Mhe Hassan amesema watakaokodishwa visiwa wawe watiifu katika kulinda na
kuhifadhi mazingira ya visiwa na kuwasikiliza wataalamu ushauri wanaoutoa kwa kuhakikisha
wanaufuata ili kuvilinda visiwa viendelee kuwepo miaka na miaka
Aidha baadhi ya wajumbe nao wameishauri Serikali kupitia Ofisi ya Makamu
wa Kwanza wa Rais kuhakikisha maeneo yaliyochimbwa mchanga yanarudi katika
uhalisia wake kwa kuotesha miti ya asili ili kuepuka athari zaidi za
kimazingira zinazoweza kutokea na kuhatarisha usalama wa maeneo jirani na
wanajamii
Nae katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Omar Dadi Shajak amesema
kuna kazi kubwa ya kuhifadhi mazingira kwenye kisiwa cha Mnemba na vyengine
vyote vya Unguja na Pemba ili kukuza uchumi wa nchi.
Dkt Shajak amesema pamoja na kukuza uchumi wa nchi pia wanachi
wanaozungukwa na kisiwa cha Mnemba nao waweze kunufaika na kuona umuhimu wa
uhifadhi wa kisiwa hiki ambacho ni moja kati ya rasilimali muhimu za Zanzibar
“Ni lazima tuweke mazingira ambayo yanakuza uchumi wetu tusibakie tu
kuwa tuna rasilimali halafu zimekaa tukaanza kuzivuruga Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais inachukuwa nafasi yake katika kuhakikisha elimu inatolewa,
mazingira yanahifadhiwa na sheria zinafuatwa katika kila hatua”
Kisiwa cha
Mnemba ni miongoni mwa visiwa vidogo ambacho kipo kilomita 3 kutoka usawa wa
bahari na Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Unguja chenye ukubwa wa hekta
10.74 ina vuvutio vingi ikiwemo kivutio cha matumbawe ambayo yapo katika eneo
la hifadhi ya bahari, kina sifa za kipekee ukilinganisha na visiwa vyengine
ambapo asili yake imetokana na uwepo wa fungu mchanga linalozunguka kisiwa
chote.
Nae Mkurugenzi wa
Hoteli ya Kisiwa cha Mnemba Bw Jonathan Braack amesema mmong’onyoko mkubwa wa fukwe hasa upande wa
Mashariki na Kusini ya kisiwa, Uwegeshaji na Utupaji mbaya wa nanga wa boti za
kitalii ambao huharibu mwamba na idadi kubwa ya watalii wanaoogelea kwa wakati
mmoja ndani ya mwamba wa hifadhi ni changamoto ambazo zinakikabili kisiwa hicho.
Jonathan ameelezea baadhi ya hatua zinazochukuliwa kutatua changamoto hizo ikiwemo kuhamasisha upandaji na utunzaji wa miti ya asili katika kisiwa cha Mnemba ili kurudisha uoto wa asili na kuimarisha uhimili wa kisiwa hicho, kutoa elimu na kushirikiana na vijiji jirani katika kukiweka salama kisiwa cha Mnemba na kusaidia miradi kadhaa ya wanajamii
Akielezea kazi zilizopangwa kutekelezwa katika kipindi cha April na Juni
2021 kwa niaba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt Saada
Mkuya Salum, Dkt Shajak amesema kazi moja wapo ni kufanya mapitio ya sera na
sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, kuelimisha jamii
masuala yanayohusu UKIMWI na afya ya uzazi.
Kutekeleza shughuli za uratibu na ufatiliaji wa masuala ya Watu wenye
Ulemavu, kuteleza shughuli zilizolenga kudhibiti usambazaji,kuuza pamoja na
matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo kuandaa vikao vya ulinzi na usalama katika
Shehia za Unguja na Pemba, kukamilisha maandalizi ya mpango wa muda wa kati wa
matumizi ya Bajeti ya Ofisi
Dkt Saada ameendelea kuwakumbusha watumishi wote wa Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais na jamii kwa ujumla kuwa janga la Korona bado lipo na inatupasa
kuzingatia miongozo na maelekezo inayotolewa nawataalamu wa afya
Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za viongozi wakuu wa
kitaifa imetembelea eneo lilokuwa likitumiwa kuchimbwa mchanga Bumbini
Pangatupu na eneo lilikuwa likichimbwa mawe kwa ajili ya ujenzi wa barabara
shehia ya Kidaanzini na kisiwa cha Mnemba.
Pia ziara hio itamalizia kwa kutembelea Mamlaka ya Kudhibiti na
kupambana na Dawa za Kulevya Dar es Salaam ili kupata uzoefu kutoka Mamlaka
hiyo, Baraza la Taifa la Uhifadhi na usimamizi Mazingira NEMC na kuelekea
Kisarawe kwenye mitambo ya kampuni ya Tindwa Medical and Health ya kuchomea
taka hatarishi
No comments:
Post a Comment