Habari za Punde

NMB yatoa msaada wa vifaa vya kuezekea kwa baadhi ya maskuli na vitanda vya Hospitali kwa mkoa wa Kusini Unguja

AFISA Mkuu wa wateja binafsi na Biashara benki ya NMB Filbert Mponzi, akitoa ufafanuzi wa msaada wa vifaa vya kuezekea baadhi ya skuli, na vitanda vya hospitali viliyotolewa na benki hiyo kwa mkoa Kusini Unguja huko Binguni.

AFISA Mkuu wa wateja binafsi na Biashara bank ya NMB Filbert Mponzi (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi Rashid, msaada wa vitanda vya hospitali vilivyotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya hospitali za mkoa Kusini Unguja huko Binguni.MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi Rashid, akizungumza na wananchi mbali mbali baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kuezekea kwa baadhi ya skuli, na vitanda vya hospitali viliyotolewa na benki ya NMB kwa mkoa Kusini Unguja huko Binguni.

MKUU wa Mkoa  wa Kusini Unguja Rashid Hadidi Rashid wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa benki ya NMB, na maofisa wa afya, na elimu mkoa wa Kusini Unguja, baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kuezekea kwa baadhi ya skuli, na vitanda vya hospitali viliyotolewa na benki hiyo kwa mkoa Kusini Unguja huko Binguni.

WATENDAJI wa benki ya NMB, na mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja ,wakiwa  katika picha wa pamoja na wanafunzi wa skuli ya msingi Binguni baada ya baada benki hiyo kukabidhi msaada wa vifaa vya kuezekea skuli hiyo huko Binguni.

WATENDAJI wa benki ya NMB, wakiwa  katika picha wa pamoja na wanafunzi wa skuli ya msingi Binguni baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa vifaa vya kuezekea skuli hiyo  huko Binguni.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.