Mshitakiwa Bwana Sadalla Juma Sadalla mwenye umri wa miaka 74 aliyembaka mfanyakazi wake wa nyumbani (house Girl) mwenye umri wa miaka 15
Alifikishwa mahakamani tena leo 31 Augosti 2021 katika mahakama ya Vuga,Unguja. na baada ya kusimamishwa kizimbani Hakimu ameamru mshitakiwa arudishwe mahabusu hadi tarehe 19 Septemba 2021 kesi hiyo itakaposikilizwa tena.
Mshitakiwa Bwana Sadalla Juma Sadalla anashitakiwa kwa kumbaka msichana wake wa kazi (jina linahifadhiwa).
Bwana Sadalla Juma Sadalla ameripotiwa na analalamikiwa na kuwa ni mzoefu wa tabia za ubakaji na mara nyingi kesi zake huzimaliza kienyeji lakini mara hii vyombo vya dola katika kukomesha vitendo vya ubakaji vimemtia nguvuni na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeazimia kukomesha kabisa vitendo vya ubakaji,udhalilishaji wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment