WADAU wa kutoa maoni
juu ya sheria ya Kupambana na dawa
za Kulevya Zanzibar, wakiwa katika mkutano huo ulioandaliwa na Tume ya
Kurekebisha sheria Zanzibar
MKURUGENZI
Mtendaji tume ya kitaifa ya kuratibu
na udhibiti wa dawa za kulevya Zanzibar Kanali Burhani Zuberi Nasoro, akiwasihi
wajumbe kutoka maoni yao ili kuboresha shehia ya kupambana na dawa za kulevya
Zanzibar, mkutano uliofanyika mjini chake chake.
MWENYEKITI
wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Khadija Shamte Mzee, akizungumzia sababu
iliyopelekea tume hiyo kukusanya maoni kwa wadau juu ya sheria ya kupambana na
dawa za kulevya Zanzibar, mkutano uliofanyika mjini chake chake.
MKUU
wa Mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor Massoud, akifungua kikao cha wadau wa
kupitia sheria ya kupambana na dawa za kulevya Zanzibar, mkutano uliofanyika
mjini Chake Chakena kuwashirikisha wadau kutoka taasisi mbali mbali za serikali
na kamati za ulinzi na usalama Pemba.
WATENDAJI
kutoka Tume ya tume ya kitaifa ya
kuratibu na udhibiti wa dawa za kulevya Pemba, wakifuatilia kwa makini utoaji
wa maoni juu ya sheria ya kupambana na dawa za kulevya Zanzibar, mkutano
uliofanyika mjini Chake Chake.
KATIBU
Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba Khatib Juma Mjaja, akichangia maoni yake katika
mkutano wa utoaji wa maoni juu ya sheria ya kupambana na dawa za kulevya Zanzibar,
mkutano ulioandaliwa na tume ya kurekebisha sheria Zanzibar na kufanyika mjini
Chake Chake.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA Mhandishi Dkt.Salha Mohamed
Kassim(mwenye miwani) akiangalia moja ya chemchem ya kutolea maji katika eneo
la Patini Wete.
KATAPILA la Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, likiweka sawa barabara ya Wesha kwenda ndagoni hadi Mkumbuu, kama ililivyokutwa na mpiga picha wetu.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
No comments:
Post a Comment