Habari za Punde

Serikali itatoa ushirikiano kwa mohoteli yaliyoathiriwa na janga la moto Paje

Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed  alipokuwa akimsikiliza mmoja wa wamiliki wa hoteli hoteli zilizoathiriwa na janga la moto huko Jambiani na kuwahakikishia kwamba serikali itatoa kila aina ya ushirikiano katika kurudisha hali ya hoteli zao.
Muonekano wa mali zilizoathiriwa na janga la moto lilivyoathiri jumala ya hotel nne huko Jambiani Kibigija Mkoa wa Kusini Unguja
Muonekano wa mali zilizoathiriwa na janga la moto lilivyoathiri jumala ya hotel nne huko Jambiani Kibigija Mkoa wa Kusini Unguja
Wamiliki wa hoteli zilizopatwa na athari ya kuungua moto wakimueleza Makamu wa Pili wa Rais juu ya faraja yao kutokana na ushirkiano walioupata kutoka serikalini.
Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed akiwahakikishia wamamiliki wa hoteli zilizoathiriwa na janga la moto huko Jambiani kuwa serikali itatoa kila aina ya ushirikiano katika kurudisha hali ya hoteli zao.
Muonekano wa mali zilizoathiriwa na janga la moto lilivyoathiri jumala ya hotel nne huko Jambiani Kibigija Mkoa wa Kusini Unguja

Na Kassim Abdi, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali itatoa kila aina ya ushirikiano katika kurudisha hali za hotel zilizoathiriwa na janga la moto.

Mhe. Hemed alieleza hayo wakati alipofanya ziara ya kuzikagua hotele nne zilizoathiwa na janga la moto huko Jambiani Kibigija Mkoa wa Kusini Unguja pamoja na kuwafariji wawekezaji wa hotel hizo.

Katika kufanikisha azma hiyo Makamu wa Pili wa Rais aliziagiza mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya sekta ya utalii kukaa pamoja na kuja na mapendekezo ya kuishauri serikali yatakayosaidia kurudisha hali za hoteli hizo.

Aliwataka wawekezaji hao kujenga Imani kuwa serikali imeguswa na kadhia hiyo na itatoa ushirikiano wake katika kuwasaidia wawekezaji waliopatwa na athari.

Katika hatua nyengine Mhe. Hemed alizitaka mamlaka zinzohusika na utoaji wa huduma kwa wawekezaji kuendelea kutoa taaluma kwa wawekezaji juu ya miundombinu bora ya kutumia katika ujenzi wa hotel ili kuepukana na athari.

Aidha, aliupongeza uongozi wa serikali za mkoa na wilaya kwa hatua za haraka walizozichukua katika kukabiliana na janga hilo ambapo hakuna taarifa yoyote ilioripotiwa ya majeruhi wala kifo.

Akitoa taarifa kuhusiana na janga hilo la moto Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi Rashid alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa, jumla ya hotel nne zimetekea kwa janga la moto lililosababishwa na kuungua kwa sehemu jikoni katika hoteli ya Villa De Coco.

Mhe. Hadidi alieleza kwamba moja kati ya changamoto iliojitokeza ni kukosekana kwa miundombinu bora ya kupambamba na janga la moto na kuishauri serikali kuangalia namna nzuri ya kuimarisha miuondombini hiyo ikizingatiwa Mkoa wa kusini ni Ukanda wa uwekezaji wa hoteli za kitalii.

Alibainisha kuwa kufuatia tukio hilo la janga la moto bado thamani halisi ya athari iliopatikana hajifahamika ambapo wahusika wanaendelea na zoezi la kufanya tahhmini.

Nao, wamiliki wa hoteli hizo waliipongeza serikali kwa jitihada zake kwa kushirikiana nao katika zoezi zima la uokoaji wa wageni waliokuwepo katika eneo la tukio.

Waliiomba serikali kungalia jinsi itakavyoweza kuwasaidia kwani athari iliowapata ni kubwa na ikizingatiwa kwa kipindi kirefu sasa hawakufanya biashara kutokana na wimbi la ugonjwa wa UVIKO-19.

Hoteli hizo zilizoathiriwa na janga la moja ni pamoja na Villa de Coco, Kobe House, Fan Beach na Spice Island na kusababisha jumla ya wafanya 48 watakuwa hawana ajira kufuatia tukio hilo la hoteli kuungua moto.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.