Habari za Punde

Wajumbe wa kamati ya ushauri mradi wa Viungo wafurahishwa na utekelezaji mradi huo kwa mwaka mmoja
Wakati utekelezaji wa mradi wa    Viungo visiwani Zanzibar ukingia mwaka wa pili kamati ya ushauri ya mradi huo (ZIMAG) imefanya ziara ya kukagua baadhi ya mashamba ambayo ni ya wanufaika wa mradi huo katika maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Unguja.


Ziara ya ukaguzi huo wa mashamba iliongozowa na Mwenyekiti wa kamati hio Mohamed Khamis Rashid pamoja na wajumbe wengine ambao ni wa kamati hio pamoja na Meneja mkuu wa  utekelezaji mradi Amina Ussi Khamis.


Akizungumza mara baada ya kufanya ziara Mwenyekiti wa kamati hio ambae pia ni Mkurugenzi idara ya kilimo Zanzibar alisema wamejifunza mengi kupitia ziara hio ikiwemo kuona maendeleo makubwa ya wakulima ambao ni wanufaika wa mradi wa Viungo.


Alisema cha kufurahisiwa zaidi kuona mradi huo umejikita  kwa walengwa na kwa kiasi kikubwa kuna maendeleo ambayo yameifariji kamati hio ya ushauri.


Alieleza kuwa wao kama wajumbe wa kamati  imewanufaisha kwa kiasi kikubwa ikiwemo kujua kinachoendelea na wataendelea kufanya ziara nyengine zaidi kila muda.


Sambamba na hayo aliwataka wakulima katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba kuitumia fursa ya mradi huo kama sehemu ya kujiendelea kiuchumi na wasikubali kabisa kutojihusha na mradi huo kwa kuwa ni aina ya mradi ambao una malengwa makubwa ya kuwainua wananchi kiuchumi.


‘’Ninapenda kutoa wito kwa wakulima wote katika kipindi hichi cha utekelezaji wa mwaka wa pili wa mradi huu kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujisajili ili wanufaika wengi zaidi waweze kupatikanka’’aliongezea.


Awali Meneja utekelezaji mradi huo Amina Ussi Khamis alisema ziara ya wajumbe hao imeratibiwa kwa lengo la kukusanya maoni ya kamati hio ya ushauri ili waweze kutoa ushauri baada ya kuona kile kinachoendelea shambani.


Alieleza kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja mradi huo umeshafanya mengi ambayo wajumbe wakamati hio ya ushauri wangepeswa kuyaona na na kuja na ushauri utakao jenga zaidi na kuleta tija.


Mmoja miongoni mwa wakulima ambae anajihusisha na uzalishaji wa miche ya miti ya Matunda Kurwa Othman Chande alisema kupitia mradi ameongeza elimu na ujuzi ambao awali hakuwahi kuwa nao na ndio kitu pekee hivi sasa anachoendelea kujivunia.


Alisema kupitia mradi wa viungo umefanya kuongeza ari zaidi ya uzalishaji wa miti tofauti ya matunda na kuwauzia watu mbali mbali jambo ambalo anaamini limekuza soko lake.


Mkulima mwengine wa pilipili boga kutoka shehia ya mwache alale  Sheikha Khamis Sheikha alisema kabla ya utekelezaji wa mradi huo walikua wakifanya kilimo hicho lakini hakikua na manufaa makubwa.


Alisema mara baada ya kutekeleza mradi huo hivi sasa wanafika hadi kuvuna pilipili boga kilo 2000 na wametanua soko zaidi kwa kuuza bidhaa hizo Bagamoyo.Alisema uamuzi wa kuuza bidhaa hizo nje ya Zanzibar umetokana na changamoto kubwa ya masoko visiwani hapa pamoja na ulanguzi aliodai unafanywa na madalali katika masoko mbali mbali.Mradi wa huu wa Viungo unatekelezwa katika shehia  60 Unguja na Pemba kwa mashirikiano kupitia taasisi ya PDF,CFP pamoja na TAMWA-ZNZ chini ya ufadhili wa umoja wa Ulaya (EU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.