Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekusudia kufungua miradi 30 na miradi 13 kuwekewa mawe ya msingi katika maeneo mbalimbali Unguja na Pemba.
Akitoa taarifa kuhusu sherehe za Mapinduzi kwa Waandishi wa Habari ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dr Khalid Mohamed amesema miongoni mwa miradi hiyo itayofunguliwa ni pamoja na Jengo la Mahkama kuu ya Zanzibar,Ufunguzi wa kiwanda cha ushoni na kiwanda cha viatu vya kikosi cha Valantia Zanzibar,Ufunguzi wa nguo za Basra.
Amesema pia Uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha Afya,wodi ya wazazi na Nyumba ya Daktar iliopo Wilaya ya Mkoani Pemba.
Dr Khalid ameeleza katika kuenzi mchango uliotolewa na wazanzibar mbalimbali katika maendeleo ya nchi katika utumishi wa umma serikali imekusudia kutoa Nishani maalum za Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa wananchi waliokusudiwa kupewa kwa mwaka huu.
Amesema kwa upande mwengine Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika vikao vyao vinavyoendelea watajadili mswaada wa sheria wa kuwaenzi viongozi waliopigania Mapinduzi ili waendelee kuenziwa kisheria kwani walitoa mchango mkubwa katika taifa hili.
Amesema ipo kila sababu kwa Serikali za Mapinduzi Zanzibar kuwaenzi kwa vitendo wazee waliopigania mapinduzi ambayo hivi sasa wazanzibar wanajivunia kutokana na kupatikana kwa matunda yake.
Waziri huyo amesema miongoni mwa shughuli nyengine zitakazo fanya katika kuelekea sherehe za Miaka 58 ya Mapinduzi ni Upambaji wa maeneo ya barabara na majengo ya serikali na binafsi ambapo wananchi wametakiwa kuzingatia rangi,Usafi wa mazingira,Matembezi na mazoezi ya viungo kitaifa.
Amesema yapo mafanikio yaliyopatikana kupitia Mapinduzi katika kipindi cha miaka 58 hivyo taarifa za mawizara zitatolewa kwa vyombo vya habari kwa madhumuni ya kuelezea mafanikio ya serikali,kutakuwa na tamasha la maonesho ya biashara ya kitaifa ambapo wajasiri amali mbalimbali Zanzibar na Tanzania bara watashiriki yatakayofanyika katika viwanja vya maisara na kufunguliwa rasmi tarehe 8 Januari.
Katika Maadhimisho hayo pia kutakuwa na upigaji wa fashi fash za Mapinduzi kwa unguja katika viwanja vya maisara na kwa pemba Tibirinzi chakechake tukio hilo litakalo tanguliwa na burudani za muziki pamoja na vikundi vya ngoma vya utamaduni vya Zanzibar.
Kila ifikapo tarehe 12 Januari ya kila mwaka nchi huadhimisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambayo yamemkomboa Mzanzibar.
No comments:
Post a Comment