TAARIFA YA MHESHIMIWA WAANDISHI WA HABARI WA KUHUSU
ZOEZI LA UHAKIKI WA VIKUNDI VILIVYOOMBA MIKOPO YA UVIKO 19 AMBALO LITAFANYIKA KUPITIA MIKOA MITATU YA UNGUJA KUANZIA TAREHE
06/12/2021
Ndugu
Waandishi wa Habari,
Ndugu
Wananchi,
Mabibi
na Mabwana,
Assalaamu
Alaykum.
Awali
ya yote sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia neema ya uzima na Afya njema na kukutana hapa asubuhi. Naomba
nikushukuruni nyote kwa kuitikia wito wetu wa kuungana nasi ili kupokea taarifa
zetu mbalimbali za Afisi yetu.
Ndugu Waandishi wa Habari;
Lengo
la kukutana nanyi hapa ni kukupeni taarifa kuhusiana na zoezi linalotakiwa
kufanywa na Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji kwa kushirikiana na Afisi
za Mikoa na wadau wengine wanaohusiana na Programu ya Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi la kufanya Uhakiki wa Vikundi vilivyoorodheshwa juu ya uhitaji wa
kupatiwa mikopo ya fedha zilizotokana fedha za Mkopo wa IMF za ahueni ya janga
la Uviko 19 ambapo Serikali yetu imezipokea na kuzisimamia.
Kama
mnavyofahamu fedha hizi zimelengwa kuwanufaisha wananchi wote wa Zanzibar
(Unguja na Pemba) ambao wanaohitahi wa fedha hizo na wamekidhi vigezo
vilivyowekwa. Aidha fedha hizo ni za masharti mepesi ili wananchi wenye uwezo
mdogo/duni kufaidika.
Ndugu Waandishi wa Habari;
Napenda
kueleza kuwa wananchi wengi kupitia vikundi vyao wameshajihika na kuomba
kupatiwa fedha hizo. Nachukua fursa hii kuzishukuru Asasi mbalimbali za Umma na
Binafsi kuwashajihisha Wananchi. Shukrani za pekee napenda kuzitoa kwa Serikali
za Mikoa na Wilaya kwa kazi kubwa walioifanya kuhusu jambo hili la
kuwashajihisha wananchi. Pia nina
kushukuruni sana Nyinyi waandishi kwa ufanisi mkubwa wa kuwaeleza
wananchi juu ya fedha za COVID 19 au UVIKO 19.
Ndugu Waandishi wa Habari;
Kwa
kuwa fedha hizi za UVIKO 19 ni za Serikali hivyo watapatiwa wananchi kupitia
vikundi vyao, kabla ya fedha hizo kutolewa Afisi yangu, Afisi ya Rais, Kazi,
Uchumi na Uwekezaji kwa kushirikiana na
Serikali za Mikoa na Wadau wengine kuanzia Jumatatu tarehe 06 Disemba,2021
tutafanya zoezi la Uhakiki kwa vikundi vyote viliomba na kuorodheshwa kupata
mikopo.
Ndugu Waandishi wa Habari;
Uhakiki
huu itaangalia na kupitia taratibu na miongozo iliowekwa Serikali kupitia Afisi ya Rais,Kazi,Uchumi na
Uwekezaji kwa kushirikiana na Wizara zinazohusika moja kwa moja na sekta zilizomo
katika mradi huu.Vigezo hivyo uwepo wa kikundi au ushirika ulio rasmi wenye
kutambulika kisheria kwa kupata usajili ,uwepo wa Biashara ,kikundi kiwe na
uhitaji wa mkopo huo pamoja na kufuata taratibu za maombi ili kuweka misingi imara
ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.
Ndugu Wananchi na Ndugu Waandishi wa Habari;
Napenda
kukujulisheni ili nanyi muweze kuwaeleza Wananchi wetu kwamba, kwa wote
waliomba kupatiwa fursa ya fedha hizi za UVIKO 19 wanapaswa kutambua kwamba
mikopo hii ni yenye masharti nafuu ili kuweza kuimarisha uzalishaji wa bidhaa
na utoaji wa huduma kwa lengo la kujiajiri na kuzalisha ajira,hivyo Serikali za
Mikoa tayari zimetoa mashirikiano kwa kuwataarisha wajasiriamali wetu kupitia
shehia mbali mbali ili kuweza kunufaika na fedha hizi.
Ndugu Waandishi wa Habari;
Mbali
na kuwekwa kwa taratibu hizo, Afisi ya Rais,kazi,Uchumi na Uwekezaji kwa
kushirikiana na Wadau pamoja na Serikali za Mikoa, imeanza utaratibu wa awali
wa kuhakiki vikundi vyote ambavyo vimewasilishwa kutoka mikoani kupitia shehia
mbali mbali ili kuhakikiwa na wajumbe kutoka Kamati ya Ufuatiliaji ili
kujiridhisha juu ya uwepo wa vikundi na shughuli zake,baadae kufanyiwa tathmini
itakayofanywa na Watendaji wa Benki, Mfuko na Watendaji wengine watakaoteuliwa
katika kazi hiyo. Ili kujua kiasi gani cha fedha kinahutajika kwa mradi ulioomba.
Ndugu Wananchi na Ndugu Waandishi wa Habari;
Napenda
kuwajuulisha wananchi ambao wamejitokeza katika kuorodhesha vikundi vyao
kupitia Serikali za Mikoa kwamba zoezi la uhakiki wa vikundi litafanyika
kuanzia siku ya jumatatu na tarehe
06/12/2021 kwa Mkoa wa Kusini Unguja na kufuatiwa na mikoa mengine ya Kaskazini
na Mjini Magharibi.Aidha napenda kuwaomba wajasiriamali wetu kutoa mashirikiano
ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa lengo la kukamilisha program hii na
kuhakikisha vikundi vya wajasiriamali mbali mbali walioainishwa wananufaika kwa
mujibu wa taratibu zilizowekwa zoezi la kuhakiki ni endelevu kwa sababu program
za Uwezeshaji nazo ni endelevu.Kwa hivyo naomba viongozi tuwaelimishe na kuwatayarisha
wajasiriamali wetu ili waweze kushiriki kikamilifu katika program hii.
Ndugu Wananchi na Ndugu Waandishi wa Habari;
Zoezi
hili ni la kawaida kama Utafiti na Ufuatiliaji mwengine unavyofanywa hivyo
wananchi wasiwe na wasiwasi wawote. Natoa wito kwa kushiriki zoezi hili na
kutoa taarifa sahihi kwa manufaa yao, Serikali na Wananchi wote. Serikali ipo
kwa ajili yao, itawalinda, kuwaenzi na kuwasaidiwa kadri hali inavyoruhusu.
Ahsanteni
sana kwa kunisikiliza na kuwaombeni ushirikiano wenu mkubwa.
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA
No comments:
Post a Comment