Habari za Punde

Tangazo la Uhakiki Kwa Wastaafu Wanaolipwa Pencheni ZSSF. Januari 2022

 

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR (ZSSF) UNAWATANGAZIA WASTAAFU WANAOLIPWA PENCHENI YA ZSSF KUWA ZOEZI LA UHAKIKI WAO WA MWANZO WA MWAKA SASA UTAFANYIKA KUANZIA JUMATATU YA TAREHE 03/01/2022 HADI JUMAPILI 09/01/ 2022.

KWA WASTAAFU WA UNGUJA UHAKIKI HUO UTAFANYIKA KWA UTARATIBU UFUATAO:-

 TAREHE : 03 JANUARI HADI 09 JANUARI 2022

MUDA   : KUANZIA SAA 2:00 ZA ASUBUHI  MPAKA SAA 7:00 

                  MCHANA

PAHALA: KIWANJA CHA KUFURAHISHIA WATOTO  KARIAKOO.

AIDHA KWA KUWAPUNGUZIA USUMBUFU WASTAAFU WALIOPO MASHAMBA, UHAKIKI HUO PIA UMESOGEZWA KARIBU NA MAENEO WANAYOISHI KAMA IFUATAVYO:-

Ø KWA WASTAAFU WA KASKAZINI UNGUJA WANATAKIWA KUFIKA KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA KUANZIA TAREHE 03/01/2022 HADI TAREHE 04/01/2022

Ø KWA WASTAAFU WA WILAYA YA KATI WANATAKIWA KUFIKA KITUO CHA WAALIMU TC DUNGA KUANZIA TAREHE 05/01/2022 HADI 06/01/2022

Ø KWA WASTAAFU WA WILAYA YA KUSINI UNGUJA WAFIKE KITOGANI KATIKA AFISI ZA HALMASHAURI KUANZIA TAREHE 07/01/2022 HADI 08/01/2022

KWA WASTAAFU WA PEMBA UHAKIKI HUO UTAFANYIKA:-

 TAREHE : 03 JANUARI HADI 09 JANUARI 2022

MUDA       : KUANZIA SAA 2:00 ZA ASUBUHI  MPAKA SAA 7:00 

                      MCHANA

 

PAHALA  : AFISI ZA ZSSF TIBIRINZI CHAKECHAKE PEMBA.

 KWA KASKAZINI PEMBA, WASTAAFU WANATAKIWA WAFIKE JAMHURI HALL WETE TAREHE 03 HADI TAREHE 04/01/2022.

Ø NA PIA UKUMBI WA SHAAME MATTA MICHEWENI KWA TAREHE 05 HADI 06/01/2022

Ø NA KWA KUSINI PEMBA, WASTAAFU WANATAKIWA KUFIKA AFISI YA BARAZA LA MJI MKOANI KUANZIA TAREHE 07/01 HADI 08/01/2022

 

AIDHA KWA WASTAAFU WALIOPO DAR ES SALAAM UHAKIKI WAO UTAFANYIKA:-

TAREHE: 03/01/2022 HADI 07/01/2022

PAHALAAFISI ZA IDARA YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ   

                   ZILIZOPO MTAA WA LITHULI MKABALA NA JENGO LA   

                  WIZARA YA FEDHA YA JAMHURI YA MUUNGANO  WA

                   TANZANIA

                                     

 

 

MUHIMU KUZINGATIA:-

1.     WASTAAFU WATAKAPOKWENDA KUHAKIKIWA WANATAKIWA KUCHUKUA VITAMBULISHO VYAO VYA USTAAFU VYA ZSSF NA ASIYEHAKIKIWA PENCHENI YAKE ITAZUIWA.

2.     WAHUSIKA WANAOMBWA KUFUATA WAKATI NA SIKU HIZO ZA UHAKIKI KAMA ZILIVYOPANGWA.

3.     UHAKIKI WA WASTAAFU HAUTAFANYWA KATIKA AFISI ZA KILIMANI MNARA WA MBAO

4.     WASTAAFU AMBAO NI WAGONJWA AU WASIOJIWEZA WANAOMBWA KUBAKI NYUMBANI. WATEGEMEZI AU WASAIDIZI WAO WAWASILISHE KADI ZAO KWA AJILI YA KUHAKIKIWA.

KILA ATAKAESIKIA TANGAZO HILI ANAOMBWA AMUARIFU MWENZIWE.

 

ZSSF NI UFUNGUO WA MAISHA YA BAADAE!!!

 

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA:

KITENGO CHA MASOKO NA UHUSIANO

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR - ZSSF

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.