Habari za Punde

Wanadiaspora watakiwa kuwa Mabalozi wazuri kuitangaza Zanzibar

 Baadhi ya Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, wakiwa katika Mkutano kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, wakiwa katika Mkutano kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa TDH Nassor Mh’d Ali, akielezea kuhusu TDH katika Mkutano wa Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa TDH Nassor Mh’d Ali, akielezea kuhusu TDH katika Mkutano wa Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Diaspora Adila Hilali Vuai, akielezea Umuhimu wa Diaspora katika Mkutano wa Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.


Katibu Mkuu, Afisi ya Rais, Kazi na Uwekezaji Dk. Habiba Hassan Omar, akifunguwa Mkutano wa Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.

 Khamiss Dunia kutoka Idara ya Uwenezi na Masoko ZIPA na Khalfani Ali Mohamed Afisa Masoko Mkuu Kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar wakiwasilisha mada kuhusu Zanzibar na Utalii uliopo ndani yake, katika  Mkutano wa Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.


 Mkurugenzi wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Hamad Bakar Hamad, akiwasilisha mada kuhusu Zanziba na Uchumi wa Buluu katika  Mkutano wa Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.
 Aisha Juma Issa akiuliza Swali kuhusu Vijana na Ajira katika Kilimokatika  Mkutano wa Wanadiaspora na Taasisi za Umma na Binafsi, kwa ajili ya kujadili na kuandaa Mikakati ya Ushirikishwaji wa Diaspora, katika Fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, huko Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.

PICHA NA MARYAM KIDIKO / MAELEZO ZANZIBAR.

Na Issa Mzee – Maelezo   31/12/2021

Wanadiaspora wa Zanzibar wanaoishi katika mataifa mbalimbali ulimwenguni  wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kuzitangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana Zanzibar ili kukuza uwekezaji na  maendeleo nchini.

Agilzo hilo limetolewa na Katibu Mkuu Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Dk.Habiba Omar, katika Mkutano wa Wanadiaspora, Taasisi za Umma na Binafsi uliolenga kujadili na kuandaa mikakati ya ushirikishwaji wa Wanadiaspora, katika fursa za Uwekezaji na Biashara Zanzibar, uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Zanzibar.

Alisema endapo wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni watawekeza Zanzibar, katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii unaisaidia Serikali kutekeleza mipango ya maendeleo.

Alisema kuwa, Zanzibar zipo fursa nyingi za uwekezaji katika katika sekta tofauti ikiwemo Uchumi wa Buluu, Uvuvi wa Bahari kuu, Mwani pamoja Bandari, hivyo amewataka wanadiaspora kuwa mabalozi wazuri wa kuzitangaza fursa hizo.

“Hata kama munaishi nje na nyumbani bado, munahitajika katika kuungana na wananchi na Serikali katika kuunga mkono jitihada za kuleta maendeleo kupitia uwekezaji kwa kuwahamasisha wananchi wetu wanaoishi mataifa mbalimbali waje wawekeze nyumbani”,  alisema Katibu Mkuu.

Aidha alisema ushirikishwaji wa wandiaspora katika makongamano mbalimbali ya maendeleo umesaidia kwa kiasi kikubwa katika kuvuta uwekezaji na kuzitangaza fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo nchini.

Nae  Mkurugenzi wa Diaspora Adila Hilali Vuai, amesema wanadiaspora wamekuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kutekeleza Sera na Ajenda mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ili kuijenga Tanzania.

Alieleza kuwea, wanadiaspora wanaendelea kushirikiana na Serikali katika kushiriki na kutekeleza miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umoja wa Miradi ya Wawekezaji (TDH), Nassor Ali Basalama, amesema Sera nzuri ya Uwekezaji iliowekwa Zanzibar pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji yameuhamasisha umoja huo kuweka nia ya kuwekeza Zanzibar katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo.

Alisema kuwa, umoja huo umeamuwa kwa makusudi kufika Zanzibar ili kutizama na kukagua maeneo yote yenye mazingira ya uwekezaji kwa lengo la kuwekeza visiwani hapa.

Akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Zanzibar, Afisa kutoka Mamlaka ya Kukuza  Uwekezaji  Zanzibar (ZIPA), Khamis Dunia amesema Zanzibar kuna fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo visiwa vidogo vidogo, Bandari pamoja uwepo wa mafuta na gesi hivyo amewataka wanadiaspora kuwekeza katika fursa hizo.

Alisema kuwa Mamlaka inaendelea kuengeza vivutio mbalimbali vya uwekezaji ili kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wawekezaji.

Akiwasilisha mada kuhusu fursa za Uwekezaji katika Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uchumi wa Buluu na Uratibu,  kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Hamad Bakari Hamad amesema zipo fursa nyingi za uwekezaji katika Uvuvi wa Bahari kuu kupitia meli za uvuvi na uwekezaji wa viwanda vya kusarifu samaki.

Alifahamisha kuwa, Serikali imeamuwa kuifanya Pemba kuwa eneo maalumu la uwekezaji, hivyo amewataka wanadiaspora kitembelea maeneo mbalimbali ya kisiwa hicho ili kuona fursa mbalimbali za kuwekeza.

Aidha alifahamisha kuwa, Serikali inaendelea na mpango wa kujenga bandari mpya Mangapwani, hivyo ni vyema Wanadiaspora hao wakawekeza katika Bandari hiyo, na kuyashawishi mataifa mbalimbali kuja kuwekeza katika Bandari.

Nae Afisa Masoko kutoka Kamisheni ya Utalii Khalfan Ali Mohammed, amesema sekta ya utalii ina maeneo mengi ya kuwekeza nchini, ikiwemo uwekezaji katika visiwa vidogo vidogo  ikiwemo ujenzi wa hoteli.

Alifahamisha kuwa ,uwepo wa huduma mbalimbali za kifedha, usafiri pamoja na matamasha mbalimbali ya kiutamaduni, unaweza kushawishi kwa kiasi kikubwa katika kuwavuta wawekezaji wa sekta ya utalii, hivyo amewataka wanadiaspora kuzitangaza fursa hizo.

Akitoa maoni kuhusu fursa za uwekezaji Mwanadiaspora kutoka Zanzibar anaeishi Saudia Rabia amesema ipo haja ya kuwawezesha vijana wenye nia ya kuwekeza kwa kuwapatia mitaji ili waweze kuwekeza Zanzibar.

Alisema kuwa, wapo baadhi ya vijana wazalendo wenye mawazo mazuri ya biashara ambao wanahitaji kuwekeza hivyo ni vyema  kuwawezesha vijana hao kimtaji.

Hata hivyo baadhi ya wanadiaspora hao waliishauri Serikali kuzingatia matumizi sahihi ya ardhi pamoja na uhifadhi wa mazingira ili kuepusha athari za kimazingira na kuyatunza mazingira ya Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.