Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.,Dkt.Mpango Amezindua Sera ya Taifa ya Mazingira.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizindua Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya uwekezaji, viwanda, biashara na mazingira, David Kihanzile.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo kitabu cha Mkakati pamoja na Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 kwaajili ya utekelezaji mara baada ya kuzindua Sera hiyo katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi, wadau wa mazingira, wanafunzi na wananchi mbalimbali juu ya uhifadhi wa mazingira wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Februari 12,2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.