Habari za Punde

MITHOO(LATA MANGESHKAR) MWANAMKE MTIMIZA AHADI

 

Na.Adeladius Makwega-DODOMA.

Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati umekuwa na ujirani mkubwa sana na watu wa Asia. Wana historia wanadai kuwa ndugu zetu hawa kutoka Asia walishafika pwani ya Afrika ya Mashariki mwaka 200 baada ya Yesu Kuzaliwa. Baadhi ya watu wakidai kuwa unaposema Utanzania wa sasa; Wahindi na Waarabu wana Utanzania wa muda mrefu kuliko hata wa Wangoni waliofika katika ukanda huu karne ya 17 na 18.

Ndugu hawa waliweza kuchangamana na kuzaliana na watu wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa miaka mingi, ndiyo kusema wapo ndugu zetu kadhaa ukiwaona leo hii ni weusi lakini wana damu za Uhindi na Uarabu.

Nina rafiki zangu wawili mmoja anaitwa Rachel Mariam huyu ni Mnyamwezi nilisoma naye Chuo Kikuu ukimuona ni mweusi sana lakini anayo damu ya Uarabu ndani yake. Pia ninaye ndugu yangu mwingine anaitwa Ashura Modestus Mpili huyu nimesoma naye shule ya msingi mama yake ana asili ya Uarabu kutoka huko Kilindoni-Mafia baba yake ni Mmatumbi.

Kwa sasa unaweza usione asili ya Uarabu ninaozungumzia lakini kwa mbali unaweza kuona nywele zao ni tofauti na zetu. Jambo hili linaonesha kuwa Waarabu na Wahindi ni sehemu ya watu wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa muda mrefu. Kwa hoja hiyo utamaduni wao umeingia katika maisha yetu kitambo.

Nakumbuka nikiwa mdogo wazazi wangu walikuwa wananinunulia fulana zenye picha za waigizaji kama Amitabh Bachchan na hata mwanamuziki Leta Mengashkar (Mithoo).

Utamaduni na sanaa ya jamii fulani una mambo mengi ikiwamo muziki nah ta filamu. Ndiyo maana hata sasa unasikia muziki wa kihindi ikiimbwa katika Pwani ya Afrika Mashariki mathalani Tanzania yetu miaka ya 1990 kulikuwa na kundi la muziki la Vard Arts walipiga muziki wenye maadhi ya kihindi. Huku wengine wakidai kuwa hata hii taarabu ya leo in asili ya Bara Asia.

Kutokana hayo yote hapo juu kwa siku ya leo namtazama mwanamauzi Leta Mangshkar (Mithoo) ambaye ni mwamuziki aliyeimba kwa zaidi ya miaka 75 kwa lugha 36 za ikiwamo Kiswahili akiwa na nyimbo zaidi ya 1000, ambaye amefariki Februari 6, 2022 akiwa na umri wa miaka 92.

Miaka 92 ni mingi sana maisha yake yana habari nyingi

Leo hii mwanakwetuu ninajibu swali moja tu, Kwanini Lata Mangeshkar hakuwahi kuolewa?

Mwanamama huyu alizaliwa septemba 28, 1929 alikuwa ni mwanamuzi mkubwa na mkongwe aliyeheshimika mno katika ulimwengu wa muziki na filamu za kihindi. Hilo lilimsaidaia kunyakuwa tuzo ya Dadasahed Phalke mwaka 1989, na kufanikiwa kutumbuiza katika ukumbi kifalme wa Albert Hall, London.

Japokuwa jina lake lilipambwa na medali, makombe na nishani, sifa na pongezi kedekede lakini maisha yake binafsi yamewashangaza wengi kwamba hadi anafariki hakuwa kuolewa.

Swali ni je alikuwa mtawa?

Lakustajabisha mwanamama huyu hakuwai kuinua mdomo wake katika kulitamka jambo hilo. Kitendo hiki kiliwafanya wambea kuibuka na kuchunguza kuna siri gani ndani ya utawa huo wa kujitakia?

Kulingana na taarifa zilizochapisha na mtandao wa Partric .com wanadai kuwa uamuzi wa mama huyo kutokuolewa ulibainika akiwa bado na umri mdogo mno. Kwani alikuwa na jukumu la kuwatunza wadogo zake ambao ni Meena, Asha, Usha na Hridayanath. Kuwatunza ndugu zake hao kupata elimu na kuwafanya wawe imara inadaiwa kuwa ilikuwa ni nadhili yake kubwa maishani. Lata aliamua kutowadhulumu ndugu zake hao haki hiyo ya kutunza na dada yao.

Kwa hiyo miaka ilisonga, ikawa mamoja, makumi na huku ikikaribia mamia ya umri, bibi huyo hakuwahi kushuhudiwa akifunga ndoa na mwanaume yoyote yule. Umri wa Lata Mangeshkar ulivyokuwa ukisonga ndivyo na kiu ya wapenzi wa muziki wake wakitaka kujua nani alikuwa akimiliki mrembo huyo?

Partric.com wanadai kuwa mchezaji maarufu wa mchezo wa kriketi na rais wa zamani wa shirikisho la mchezo huo la India BCCI Raj Singh alikuwa rafiki wa karibu wa kaka wa Lata Mangeshkar anayejulikana kama Hridaynath Mangeshkar. Ikiaminika kuwa mchezaji huyu wa zamani wa Kriketi alikuwa akizaliwa katika familia ya kifalme ya Rajasthan akiwa mtoto wa mwisho wa Maharawal Singhji, mtawala wa zamani wa Dungarpur.

Inaaminika kuwa Hridaynath Mangeshkar na Raj Singh walikuwa kweli maswahiba na mikutano yao mingi ilifanyika nyumbani mwa Hridaynath na huku Raj Singh akijenga urafiki na Lata Mangeshkar taratibu kama mchwa anayeubugua mti kwa siri ndani yake.

Safari zisizokwsiha za Raj Singh zikasababisha akamuhusudu dada wa rafiki yake. Mapenzi yana mambo kweli. Raj Singh kwa kuwa alimpenda mno Lata Mangeshkar hadi kumpa jina la utani la Mithoo.

Wapiga umbeya wanasema kuwa Leta Mangeshkar na mpenzi wake Raj Singh walikubaliana na wakawa wapenzi na waliweka mipango ya kufunga ndoa yao. Kama desturi ya ndoa zote, taarifa zikafikishwa kwa baba Raj Singh aliyefahamika kama Maharawal Singhji. Kweli mzee huyu aliupokea ujumbe huo kutoka kwa mtoto wake na akakataa katakata mtoto wake kufunga ndoa na binti familia isiyo ya kifalme.

Kwa hiyo ndoto ya Lata Mangeshkar na mpenziwe ya kufunga ndoa ilipotea kwa sekunde moja tu mbele ya mzazi ambae hakutaka kijana wake kuoa binti wa kawaida. Cha kustajabisha Raj Singh aliamua kutii maamuzi ya wazazi wake lakini alienda mbali zaidi na kutofunga ndoa na mwanamke yoyote yule katika uhai wake huku akiwaeleza wazazi wake juu ya uamuzi huo.

Je Lata Mangeshkar aliamua nini katika hili? Kwa kuwa Lata Mangeshkar alimuhusudu pia Raj Singh matokeo yake nayeye aliweka nadhiri hiyo hiyo na wawili hao walibaki kuwa marafiki milele.

Septemba 12, 2009 Raj Singh alifariki dunia huko Mumbai kwa ugonjwa wa akili unasababishwa na uzee. Naye Leta Mangeskara amefariki Februari 6, 2022. Mambo yote yakaishia hapo.

Mwanakwetu umeipata hiyo habari ya wapenzi hawa? Kubwa na la kujifunza kwa maisha ya sasa ni ule kutokusalitiana tu, kama mmekubaliana jambo fulani kama kweli mnapendana msisalitiane.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.