Habari za Punde

Nafasi za Kazi Wizara ya Afya

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi 119 za kazi katika Wizara ya Afya kwa Vituo mbali mbali vya Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1.Wauguzi Daraja la III “Nafasi 99” Unguja na Pemba

Sifa za Waombaji:

Awe ni Mzanzibari.

Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Uuguzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

MGAWANYO WA NAFASI HIZO NI:-

PEMBA

1. Wilaya ya Micheweni Nafasi 14 - Kituo cha Afya Wingwi, Konde, Makangale, Sizini, Maziwa Ng’ombe, Kiuyu Mbuyuni, Shumba Vyamboni na Tumbe

2. Wilaya ya Mkoani Nafasi 15 - Kituo cha Afya Kengeja, Kisiwa Panza, Mwambe, Bogoa, Chambani, Ukutini, Mtambile, Tasini, Kendwa, Mlangoni, Michenzani, Wambaa na Shidi

3. Wilaya ya Chake Chake nafasi 12 - Kituo cha Afya Tundaua, Wesha, Pujini, Mama na Mtoto Vikunguni, Ngomeni, Kibokoni, Ndagoni na Ziwani

4. Wilaya ya Wete nafasi 13 - Kituo cha Afya Kambini, Kangagani, Chwale, Kojani, Finya, Uondwe, Junguni, Fundo, Makongeni, Kinyasini na Kiuyu Minungwini.

UNGUJA

1. Wilaya ya Kusini nafasi 3 - Kituo cha Afya Jambiani, PHCU+ na Muyuni PHCU+

2. Wilaya ya Kati nafasi 9 - Kituo cha Afya Mwera PHCU+, Uzini PHCU+, Unguja Ukuu PHCU+ na Kidimni

3. Wilaya ya Magharibi ‘B’ nafasi 7 - Kituo cha Afya Chukwani, Magogoni na Fuoni

4. Wilaya ya Magharibi ‘A’ nafasi 6 - Kituo cha Afya Selem, Bumbwisudi na Mtofaani

5. Wilaya ya Kaskazini ‘A’ nafasi 9 - Kituo cha Afya Nungwi PHCU+, Matemwe PHCU+, Tumbatu Gomani PHCU+, Tumbatu Jongowe na Kijini

6. Wilaya ya Kaskazini ‘B’ nafasi 6 - Kituo cha Afya Bumbwini Misufini PHCU+ Mahonda PHCU+ na Kitope PHCU+

7. Wilaya ya Mjini nafasi 5 - Kituo cha Afya Mpendae, Sebleni na Mwembeladu

2.Fundi Sanifu Madawa Daraja la III “Nafasi 20”

Sifa za Waombaji:

Awe ni Mzanzibari.

Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ufamasia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

MGAWANYO WA NAFASI HIZO NI:-

PEMBA:

1. Wilaya ya Micheweni nafasi 3 - Kituo cha Afya Konde, Tumbe Maafa na Wingwi

2. Wilaya ya Mkoani nafasi 3 - Kituo cha Afya Kengeja, Wambaa na Michenzani

3. Wilaya ya Chake Chake nafasi 2 - Kituo cha Afya Pujini na Tundaua

4. Wilaya ya Wete nafasi 2 - Kituo cha Afya Mzambarauni na Kojani

UNGUJA

1. Wilaya ya Kusini nafasi 1 - Kituo cha Afya Jambiani PHCU+

2. Wilaya ya Kati nafasi 3 - Kituo cha Afya Mwera PHCU+, Uzini PHCU+ na Kidimni

3. Wilaya ya Magharibi ‘B’ nafasi 1 - Kituo cha Afya Fuoni

4. Wilaya ya Magharibi ‘A’ nafasi 1

5. Wilaya ya Kaskazini ‘A’ nafasi 3 - Kituo cha Afya Nungwi PHCU+, Matemwe PHCU+ na Tumbatu Gomani PHCU+

6. Wilaya ya Kaskazini ‘B’ nafasi 1 - Kituo cha Afya Mahonda PHCU+

Jinsi ya Kuomba:

Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,

TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,

S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Sheria House Ghorofa ya sita (6) Mazizini - Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini Gombani - Pemba.

Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi ya kazi pamoja na Wilaya na Kituo cha Afya anachokiombea.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

a)Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo

b)Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)

c)Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.

d)Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.

e)Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.

f)N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.

g)Maombi yawasilishwe kuanzia siku ya Jumatatu ya tarehe 21 Machi, 2022 na tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 01 Aprili, 2022 saa tisa kamili jioni.

Angalizo: Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wasio waaminifu (matapeli) kuwahadaa wananchi kwamba ili ufanikiwe lazima utoe kiasi cha fedha. Hivyo, Tume ya Utumishi Serikalini inawatanabahisha waombaji na wananchi wote kuwa, ajira hizi haziuzwi na zinatolewa bure, na yeyote atakae gundua vitendo hivyo vya kitapeli anaombwa awasilishe taarifa hizo kupitia Nambari 113 au 0774-824242 kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.