Mmoja wa wafanyabiashara Rabia Burhan akielezea
faida alizozipata tangu ajiunge na huduma ya Lipa kwa Simu,akibainisha ni kwa
namna gani huduma ya Lipa kwa simu imemsaidia kuongeza wateja na mapato katika
biashara yake.
Kauli hiyo ilitolewa na Mtaalamu wa Huduma ya Ezypesa wa
Zantel Eunice Hubert Alelyo, wakati akizungumza katika mkutano wa
wafanyabiashara mbalimbali wanaotumia huduma ya lipa kwa simu huko Kiembesamaki,Unguja.
Alisema huduma hiyo ina faida kubwa hasa uhifadhi na usalama
wa fedha za mfanyabiashara hivyo ni vyema kuitumia ili kukuza soko la fedha na
kumrahisishia mteja kuitumia muda wowote anapohitaji bidhaa.
Aidha alisema lengo kubwa la mkutano huo ni kutoa elimu kwa
wafanyabiashara wanaotumia huduma ya lipa kwa simu ambao bado hawana uelewa wa
kina juu ya umuhimu na faida za huduma hiyo .
Eunice alibainisha kwamba huduma hiyo inawahusu zaidi
wafanyabiashara wa Zanzibar wanaotoa huduma mbalimbali za kibiashara ikiwemo
nguo, mikahawa na inamsaidia mfanyabiashara kukusanya mapato yake kwa urahisi.
Alisema hadi sasa wana wafanyabiashara zaidi ya 4000 hasa
katika maeneo ya mjini ambao wameipokea huduma hiyo lakini pia kwa upande wa
Pemba katika maeneo ya Wete na Chake Chake pia wameipokea kwa muamko mkubwa.
Kwa upande wake,
Yassir Baharudin, mtaalamu
wa teknolojia
ya mtandao,
alisema kuwa kutokana
na kukua
kwa huduma
za intaneti, ni muhimu kwa
wafanyabiashara kujiunga na huduma hii adhimu ili kurahisisha mchakato mzima wa
kufanya biashara.
‘’Huduma hii ni salama na inarahisisha kazi sana ukilinganisha na malipo ya
kawaida, inaokoa muda na usumbufu wa kurekodi kila manunuzi anayofanya mteja.
Kutokana na kukua kwa teknolojia jambo hili limewezekana na ni muhimu kwenu
nyinyi wafanyabiashara kulipokea na kuhakikisha mmejisajii katika huduma hii ya
Lipa kwa simu na Zantel.”
Nao wafanyabiashara wanaotoa huduma zao kupitia mtandao
walisema huduma hiyo kwa kiasi kikubwa inarahisisha utoaji wa huduma kwa wateja
wao.
Rabia Burhan Saleh alisema awali alikuwa akipata changamoto kubwa katika biashara yake lakini hivi sasa anafurahishwa na huduma hiyo kwani ina faida kubwa hivyo anatoa wito kwa wafanyabiashara wengine kujiiunga na huduma hii kwani ina faida kubwa kwao na haina makato.
No comments:
Post a Comment