Habari za Punde

Wanafunzi wa Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST) Wapata Mafunzo ya Ujasirimali

Afisa kutoka Idara ya Maendeleo na Vijana iliyopo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sheila Makungu Mwinyi akitoa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia  Zanzibar  (KIST), Kuhusu kutumia Fursa mbali mbali zinazotolewa kwa Vijana ikiwemo Mikopo, kwa lengo la kujiajiri, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dkt. Idrissa Muslim Hija. Mbweni Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia  Zanzibar (KIST) Dkt. Mahmoud Abdulwahab akitoa neno la shukurani kwa Wanafunzi wa Chuo cha AP kutoka Belgum, wakati akiwaaga mara baada ya kufanya Project mbali mbali kwa Muda wa Mwezi Mmoja, kwa  Wanafunzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia  Zanzibar  (KIST), hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Dkt. Idrissa Muslim Hija, Mbweni Mjini Zanzibar.

PICHA NA MARYAM KIDIKO - KIST. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.