Habari za Punde

DC Moyo Amuokoa Diwani wa CCM Mikononi mwa Wananchi Ilolo Mpya Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Ndg. Mohammed Moyo akimsikiliza Diwani wa kata ya Ilolo Mpya Ndg.Fundi Mihayo akijibu hoja za wananchi wakati wa mkutano wa hadhara ambao ulikuwa unamtuhumu diwani huyo kutumia madaraka vibaya kwa kuwanyanyaswa wananchi
Baadhi ya viongozi wa kata wakisiliza kwa umakini kero za wananchi wanazotoa kuwashutumu wao na diwani wa kata ya Ilolo Mpya
Mmoja ya wananchi walikuwa wanatoa kero juu ya matumizi mabaya ya madaraka ya diwani wa kata ya Ilolo Mpya wilayani Iringa akisisitiza namna gani wanavyonyanyaswa na kiongozi mbele ya mkuu wa wilaya ya Iringa Ndg.Mohamed Moyo.(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa hadhara.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Wananchi wa Kijiji cha Luganga tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa wamemkataa diwani wa kata ya Ilolo mpya Fundi Mihayo kuwa sio kiongozi wao tena kutokana na kuhujumu maendeleo ya wananchi hao.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara mbele ya mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo walisema kuwa amekuwa anaongoza kwa kutumia mabavu na kupora miradi ya jumuiya.

Anjelista Pinda ni mwenyekiti wa skimu ya UKULUPA alisema kuwa umojaa kilimo cha Umwagiliji ya Luganga Pawaga UKULUPA Umedai kupata hasara kiasi milioni kumi kwa mwaka 2020/21 kutokana na migogoro ya mara kwa mara baina ya uongozi wa skimu na diwani wa kata ya Ilolo mpya

Pinda alisema kuwa Mapato ya skimu yamekua yakisuasua tangu migogoro wanayodai kuwa imesababishwa na Diwani huyo ikiwemo kupora jukumu la ukusaji wapato na kulikabidhi jukumu hilo kwa serikali.

Alisema kuwa diwani huyo amekuwa akitumia madaraka yake vibaya kwa kuwalazimisha wajumbe wa skimu hiyo kumpa fedha kinyume cha sheria za skimu na ndio chanzo cha mgogoro baina ya wananchi wa Kijiji cha Luganga na diwani Fundi Mihayo.

Pinda alisema kuwa baada kuona wajumbe wa skimu hiyo wameanza kukataa maagizo yake ndio alipoamua kuunda timu mpya ya kusimamia skimu hiyo kinyume na sheria za tume ya umwagiliaji.

Alisema kuwa uongozi wa skimu hiyo ulipoisha muda wake ilitakiwa kufanyike uchaguzi kwa mujibu wa katiba waliyonayo iliyopitishwa na time ya umwagiliaji taifa lakini kwa kutumia mabavu alikataza hakuna kufanyika kwa uchaguzi wowote jambo ambalo ni kinyume na katiba ya skimu hiyo.

Katika mkutano huo wa hadhara wananchi waliibuka na kudai kuwa diwani huyo hawafai kwa kuwa amekuwa anatumia madaraka yake vibaya kwa kuaatisha wananchi,kutowasikiliza,kutotatua kero zao bali amekuwa anawakandamiza ilimradi apate maslai kwa kutumia vyombo husika vilivyopo kwenye kata hiyo.

Walisema kuwa uongozi wa polisi kata watendaji wote wa kata na vijiji hawafanyika kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi bali wanafuata maelezo Kutoka kwa diwani jambo ambalo linapelekea wananchi wengi kunyanyaswa na kunyimwa haki zao za msingi kijijini hapo.

Kwa kauli moja wananchi hao walimuleza mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo kuwa hawataki tena kuongozwa na diwani huyo ambaye amekuwa anatumia mabavu,unyonyaji na kuwanyima haki wananchi wakati akiwaongoza.

Walimalizia kwa kumuomba mkuu wa wilaya ya Iringa awalinde maana akiondoka tu watakamatwa na kuwekwa ndani na diwani kupitia mtendaji na jeshi la polisi la kata na tarafa hiyo.

Kwa upande wake Katibu wa umoja wa skimu hiyo Boss Mongo anasema Diwani amekuwa akiwatishia pindi wanapohitaji kufanya uchaguzi akidai kuwa lengo lake ni kupandikiza watu anaowataka kinyume na muongozo wa katiba

Mongo alisema kuwa baada ya kuona diwani huyo anatumia vibaya madaraka yake waliamua kukata mlija wa kumpa fedha ndio alipoamua kuanzisha mgogoro ambao hauna msingi wowote ule kwa afya ya wananchi wa Luganga.

 Alisema Endapo Serikali ngazi ya wilaya na mkoa kwa ujumla haitoingilia kati Umoja huo hautoweza kuendelea

Akijibia malalamiko hayo ikiwemo vitisho dhidi ya viongozi wa Skimu, Diwani wa kata ya Ilolo Mpya Fundi Mihayo licha ya kukanusha amesema Serikali ilisitisha baadhi shughuli za Skimu hiyo baada ya kubaini ubadhirifu katika utendaji wake

Mihayo alisema kuwa viongozi wa skimu hiyo na baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wamekuwa wanatumika kisiasa kumchafua kwa ajili ya chaguzi zijazo kwa kuwa miongoni mwao amekuwa anawashinda mara kwa mara.

Lakini diwani huyo alishindwa kudhibitisha ubadhirifu wa viongozi waskimu hiyo kwa kuwa hakuwa na na vielelezo vya madai ya ubadhirifu aliowatuhumu viongozi wa skimu hiyo.

Diwani Fundi Mihayo alisema kuwa wananchi wa Kijiji cha Luganga sio wapiga kura wake hivyo kuona wanatoa tuhuma hizo ameshawazoea ndio maana amekuwa hapati kura kipindi cha uchaguzi Kutoka kwa wananchi wa Kijiji hicho

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo alisema kuwa Serikali imesikia kilio na kuwaomba wananchi wawe na utulivu anaunda tume maalumu kushughulikia kero za wananchi pamoja na skimu hiyo ili wananchi waweze kufanya shughuli za kimaendeleo kama walivyokuwa wanafanya awali.

Moyo alimuagiza mtendaji wa kata kutoa maelezo kwanini uchaguzi haufanyiki katika skimu hiyo na nani alitoa idhini ya kusimamisha uchaguzi wa skimu hiyo ili ajue aanzie wapi kutatua changamoto hiyo.

Alisema kuwa viongozi wa kata ya Ilolo mpya wanatakiwa kutumia busara kwenye maamuzi mbalimbali ambayo wanakuwa wanayachukua kwa wananchi waliowachagua na wanaowaongoza ili wote wawe wamoja kuwa wanajenga nyumba moja.

Moyo alimuagiza mtendaji wa kata,mkuu wa kituo cha polisi na afisa tarafa wa pawaga kuwa wakimuweka ndani mwananchi ni lazima wakamfungulie mashtaka mahakamani mwananchi huyo na sio kuwaonea wananchi kwa kuwa wao wamepewa madaraka hayo.

Alimazia kwa kuwaomba wananchi wasiwe na hasira na viongozi hao kwa kuwa ameyasikia yote anayatufutia ufimbuzi na hakuna mwananchi ambaye atanyanyaswa tena na ikitokea kiongozi anamnyanyasa mwananchi wampigie simu kwa kuwa alishawapa namba yake ya simu kumaliza mgogoro mbalimbali ya wananchi hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.