Habari za Punde

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKUMBUSHO DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Khamis Juma akifungua kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani huko Ukumbi wa Kasri ya Mwinyi Mkuu  Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mkuu wa makumbusho kutoka Idara ya makumbusho na Mambo ya Kale Bi Kei Mohammed Abdalla akiwasilisha mada ya nguvu ya makumbusho katika Maendeleo endelevu ,wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani  huko Ukumbi wa Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mjumbe kutoka Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Salama mohammed akichangia mada ya nguvu ya makumbusho katika Maendeleo endelevu, wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani huko Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Afisa Elimu Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Zanzibar Ramadhan Ali Machano  akiwasilisha mada ya nafasi ya makumbusho katika elimu, wakati wa maadhimisho ya siku ya makumbusho Duniani ,huko Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mdau wa mambo ya kale Joshi  akichangia mada ya nafasi ya makumbusho katika elimu, wakati wa kongamano la kuadhimisha siku ya makumbusho Duniani, huko Ukumbi wa Kasri ya Mwinyi Mkuu Dunga Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

 

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.