Habari za Punde

Wakwere wana msemo. “Mulungu Kibidu.” Muda mwingine Mungu huwa anaingilia kati mambo yakiwa kombo.

Na. Adeladius Makwega-DODOMA

Kwanini nasema haya kwa leo? Mwaka 2009-2016 nilisimuliwa na injini wa sauti(Sound Enginer) mmoja wa RTD hadi TBC. Akasema wakati wakitoka RTD-TVT-TUT-TBC walipitia hatua mbalimbali mpaka siku inazaliwa TBC.

RTD ilikuwa na Watangazaji na Waandishi wa habari wazuri sana kama Eda Sanga (Mtangazaji) na Clement Mshana (Mwandishi wa Chumba cha Habari). Eda Sanga japokuwa alikuwa kiongozi wa RTD lakini pia alikuwa mtangazaji mahiri.

Eda Sanga alikaimishwa nafasi ya ukurugenzi kwa muda mrefu katika kipindi hicho hadi anastaafu. Baadaye nafasi hiyo ikapitia kwa watu wengine wengine kadhaa mwisho wa siku Dastan Mhando akawa Mkurugenzi Mkuu wa TBC.

Msomaji wangu unaweza kujiuliza kwanini mwanakwetu anatoa mfano huo? Jibu lake ni kuwa Mei 21, 2022 niliandika juu ya Tunu Abdallah Kukaimu TSN muda mrefu. Mdau mmoja ambaye pia ni mwanahabari aliandika ujumbe huu kwa utani,

“Tuma Abdallah atakimu hadi atakapostaafu.”

Binafsi nikaikumbuka ile simulizi ya Injini wa RTD ambaye alinisimulia juu ya mama Eda Sanga kukaimu hadi anastaafu. Je ni kweli Tuma Abdallah wa TSN atayapitia yale yale ya Eda Sanga wa RTD?

Binafsi nina imani kuwa suala hilo litafanyiwa kazi tu maana ya wakati ule si ya sasa.

Nakutaka siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.