Enzi za uhai wake Marehem Baba yetu alitoa eneo hili lililojengwa Madrassa ambayo imekamilika na kuendelea kusomewa masomo ya Dini ya Kiislam hivi sasa,eneo jengine linaloendelea kujengwa madrassa vile vile ni sehemu tulioendeleza kutoa sisi warithi kama sadaka yetu tena.
Ujenzi wa eneo hili hauna mfadhili isipokua wenye kuitengenza Akhera yao hujitoa na kusahau ya Dunia na kuwekeza zaidi kwa Mwenyezimungu.
Nikuombe wewe unaesoma ujumbe huu kutoka ulichonacho ili kuwa sehemu ya waliotoa sadaka zao kukamilisha majengo haya ambayo matumizi makubwa yatakua ni kusomewa dini ya kiislamu na wanafunzi kutoka maeneo mbali mbali ya Pemba na nje ya Zanzibar kuishi hapa ambao hivi sasa wamekodiwa nyumba kama hostel yao.
Madrssa hii ya Fatuma Bint Rasuul ipo kijijini kengeja kitongoji cha mwakunguu na inahitaji mabati ya kawaida,milango saruji na mbao za kuezekea hivyo unaweza kutoa kutokana na uwezo wako ulionao.
Kwa mawasiliano zaidi na maekekezo tafadhali piga namba hizi hapa.
0774848800 0712550666
No comments:
Post a Comment