Habari za Punde

Nyumba ya Walimu Lumuma Sekondari Kujengwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akikagua ujenzi wa shimo la choo katika sekondari ya Lumuma jimbo la Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.

Na.Mwandishi Wetu.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tamisemi imeahidi kujenga Nyumba ya walimu moja two in one itakayojengwa kwa kupitia mradi wa EP4R katika shule ya sekondari Lumuma iliyojengwa madarasa sita kwa nguvu za wananchi.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo la kibakwe  Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Simbachawene alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, wananchi wa kata Lumuma baada ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa shule  hiyo.`

“gharama za matofali katika ujenzi wa nyumba hiyo ya walimu zitatolewa na nguvu kazi ya wananchi, na tunaweza kujenga nyumba mbili za aina hiyo kama tutakaza msuli vizuri alisema waziri”

Kupitia fedha za mfuko wa jimbo nitasaidia katika kukamilisha ujenzi wa miundo mbinu mingine, ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala.

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri ameelekeza Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kusajili barabara ambazo hazijasajiliwa hasa zinazoenda kwenye maeneo ya huduma za kijamii au maeneo mapya ya utawala ambayo yameongezeka.

Halmashauri inapaswa kuzifungua na kisha kuzisajili kwa mujibu wa mchakato wa kisheria, ambapo lazima kamati ya maendeleo ya kata ikae na kuzibainisha baraba mahali zilipo na urefu wake na kuonesha taasisi inayokwenda ili kupeleka mapendekezo kwenye Halmashauri na baadae kupeleka DCC na baadae kwenye bodi ya barabara ya mkoa ( Road Board).

“Barabara hizi zikisajiliwa  kwa mujibu wa sheria ni rahisi kwa wakala wa barabara vijijini (TARURA) kuzitambua na kuzitengea fedha alisema Waziri”

Awali katika taarifa yake Diwani wa kata ya Lumuma  Mhe. Joktan Chelligah amesema wananchi wa kata ya Lumuma wamejenga shule hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja.

“Wananchi tumechanga fedha kiasi cha million 17, lakini Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa imetuchangia million 20, na mifuko 150 ya saruji pamoja na mabati 250, na chama cha mapinduzi Mkoa wa Dodoma  kimechangia mifuko 130 alisema”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.