Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amejumuika na Viongozi Mbalimbali katika Hafla ya Maalum ya Chakula cha Usiku.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi  Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwasili katika viwanja  vya Ikulu Bujumbura wakiongozana na mwenyeji wao Rais Jamhuri ya Burundi Mhe.Evariste Ndayishiniye na Mkewe Mama Angeline Ndayubaha, baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula maalum cha usiku kilichoandaliwa katika viwanja vya Ikulu Bujumbura jana usiku 30-6-2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi  Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi  wamejumuika na Viongozi mbalimbali katika hafla ya chakula cha jioni walichoandaliwa na mwenyeji wao Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye na Mkewe Mama Angeline Ndayubaha Ndayishime, Ikulu Bujumbura.

Rais Dk. Mwinyi yupo nchini Burundi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi zitakazofanyika leo 01 Julai, 2022.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi  Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiagana na mwenyeji wao Rais Jamhuri ya Burundi Mhe.Evariste Ndayishiniye na Mkewe Mama Angeline Ndayubaha, baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula maalum cha usiku kilichoandaliwa katika viwanja vya Ikulu Bujumbura jana usiku 30-6-2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.