Habari za Punde

Benki ya CRDB yazindua Msimu mwingine wa kampeni ya “Tisha na TemboCard,” wateja 4 kupelekwa Nchini Qatar kushuhudia Kombe la Dunia

  
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (watatu kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Kadi, Farid Seif (wapili kulia), Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya CRDB, Badru Idd (wapili kulia) na Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa Benki hiyo, Erica Mwaipopo, wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya Tisha na TemboCard kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia, uliofanyika leo katika viwanja vya Skaut, Upanga jijini Dar es salaam.
 
 Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul akizungumza wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya Tisha na TemboCard kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia, uliofanyika leo katika viwanja vya Skaut, Upanga jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda akizungumza wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya Tisha na TemboCard kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia, uliofanyika leo katika viwanja vya Skaut, Upanga jijini Dar es salaam.
 
===========   ==========   =========
Benki ya CRDB kwa mara nyingine leo imezindua kampeni maalumu matumizi ya kadi iliyopewa jina la “Tisha na TemboCard” inayolenga kuendelea kuhamasisha wateja kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao za TemboCard huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwamo kushuhudia kombe la la Dunia litakalofanyika nchini Qatar.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika viwanja vya skauti vilivyopo Upanga, Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boniventure Paul alisema, zawadi zitatolewa kwa wateja ambao watafanya miamala mingi zaidi kupitia TemboCard zao katika kipindi chote cha kampeni hiyo ambayo inatarajiwa kuchukua miezi 6 hadi mwishoni mwa mwezi Januari 2023.
“Lengo letu ni kuona wateja na Watanzania wanaendeleza utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya malipo ya manunuzi na kuachana na utaratibu wa kutumia pesa taslimu ambazo sio salama. Katika kipindi hiki cha kampeni tutatoa zawadi kwa washindi zaidi ya 200 ambapo zawadi zenye jumla ya thamnani ya shilingi Milioni 100 zitashindaniwa,” alisema Bonaventure.

Akielezea kuhusu zawadi zitakazotolewa katika kampeni hiyo, Bonaventure alisema wateja watapata zawadi mbalimbali ikiwamo kurudishiwa asilimia 10 ya kiasi walichotumia mara baada ya kufanya  manunuzi. “Kubwa zaidi ni zawadi ya safari ya kwenda Nchini Qatar kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia kwa wateja 4 ambao watakuwa na miamala mingi zaidi katika kipindi chote cha kampeni.” aliongezea.

Bonaventure alitoa rai kwa wateja wa Benki hiyo na Watanzania kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo kwa kutumia kadi zao za TemboCard kwa kufanya malipo huku akiwasihi kuendelea na utamaduni huo hata baada ya kampeni kwani lengo ni kufanya matumizi ya kadi kuwa sehemu ya kawaida ya miamala ya malipo ikiwa ni mkakati wa kujenga jamii yenye matumizi machache ya pesa taslimu “cashless society”.

“Kwa wale ambao hawana akaunti Benki ya CRDB niwashauri wafungue akaunti ili waweze kuunganishwa na TemboCard na kuanza kufurahia huduma huku wakijiwekea nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo ikiwemo fedha taslimu ambapo Benki itatoa kiasi cha shilingi milioni mbili kila mwezi. Kama mnavyojua sasa hivi zoezi la kufungua akaunti tumelirahisisha sana,” alibainisha.

“Kama una simu janja unachotakiwa kufanya ni kupakua SimBanking App na kufuata hatua za kufungua akaunti kwa kutumia namba ya NIDA na kisha utaomba kupata TemboCard yako, kwa wale wa sio na simu janja wanaweza kutembelea kwa CRDB Wakala au tawi la karibu wakiwa na kitambulisho cha NIDA kufungua akaunti na kupata TemboCard kwa urahisi. Tunatamani kuona watu wengi zaidi wakishiriki ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo,” aliongezea.
Awali akielezea namna ya kushiriki katika kampeni hiyo na kuibuka mshindi, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi Benki ya CRDB, Erica Mwaipopo alisema wateja wanatakiwa kutumia kadi zao za TemboCard kulipia manunuzi na huduma katika maduka, supermarkets, migahawa, hoteli na vituo vya mafuta kupitia vifaa vya manunuzi (POS), pamoja na malipo ya mitandaoni ikiwamo kulipia tiketi za ndege au malipo ya kuagiza bidhaa nje ya nchi.

Benki ya CRDB ilikuwa benki ya kwanza kuanzisha huduma za kadi ‘TemboCard’ nchini mwaka 2002, ikilenga kuwapa wateja wake urahisi na unafuu wa upatikanaji wa huduma popote walipo. Mpaka sasa Benki ya CRDB imefanikiwa kutoa zaidi ya TemboCard milioni 3 ikiungana na mifumo ya malipo ya kimataifa ya Visa, MasterCard na Union Pay.  Huduma za Tembocard zimechangia kwa kiasi kikubwa kusaidia jitihada za serikali katika kuimarisha mfumo wa malipo nchini na kuongeza ujumuishi wa kifedha “Financial Inclusion”.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.