Habari za Punde

Udumisheni umoja na mshikamano uliopo - Mhe Hemed

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akiomba Dua kwenye kaburi la wanazuoni wa Zanzibar, Al-Habib Abdulrahman Bin Abubakar Bin Sumait aliefariki miaka 100 iliyopita 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia waumini wa msikiti mkuu wa Ijumaa Malindi mara baada ibada ya sala ya Ijumaa leo. 

Baadhi ya waumini waliofika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi wakimsikilizaMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ( hayupo pichani) wakati alipokuwa akiwasalimia hivi leo 

Na Ali Mohammed, OMPR

Waislamu na Wananchi kwa ujumla wametakiwa kuimarisha umoja na mshikamano uliopo kwa maslahi ya watanzania .

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo alipojumuika na Waumini katika Msikiti mkuu wa Malindi wakati wa Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Ameeleza kuwa ni wajibu wa kila muislamu na mzanzibari kuimarisha umoja na mshikamano uliopo kwa kila mmoja kwenye nafasi yake kwa maslahi ya wazanzibari na wageni wanaoingia na kutoka nchini.

Alhajj Hemed amewataka waumini na wananchi kwa ujumla kuimarisha umoja na mashikamano kwenye nchi yetu kwa maslahi ya vizazi vya sasa na baadae ndani ya nchi yetu.

Aidha Mhe. Hemed ametoa wito kwa waislamu wenye uwezo kuwasaidia watu  ambao hawana uwezo na wenye mahitaji maalum na sio kusubiri  hadi mwezi mtukufu  wa Ramadhani ndio waweze kuwasaidia watu hao.

Akizungumzia suala la madawa ya kulevya na udhalilishaji Alhaj hemed amesema waislamu na wazanzibar ni vyema kujitathmini  kwa kila hali ili kuweza kuyatokomeza matendo haya maovu hapa nchini.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wazanzibari ambao bado hawaja hesabiwa kwenye zoezi la sensa ya watu na makaazi linalooendelea nchini kuendelea kutoa mashirikiano kwa makarani wa zoezi hilo kwa maslahi ya taifa.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed amesema kuwa Serikali zote mbili zimejipanga kuhakikisha kila mwananchi atahesabiwa ili Serikali iweze kupanga mipango yake ya kimaendeleo.

Kwa upande wake Sheikh Mbarouk Shaaban amewataka Waumini kujiepusha na makundi yasiofaa yakiwemo ya watu wanaofanya vitendo kwa ria na shirki katika maisha yao ya kila siku ili wawe waumini wa kweli na kupata fadhila hapa duniani na kesho akhera.

Amesema ni wajibu kwa Waumini kujipanga na kuutumia wakati kwa kufanya mambo mema kama ulivyoamrisha uislamu kwa kufanya vitu kwa wakati kwani hakuna binadam ambaye anauhakika na wakati ujao hivyo ni lazima kufanya amali njema kwa wakati huu uliopo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.