Waziri wa Nchi (OMKR) Mhe. Harusi Said Sleiman akimsikiliza mwenyekiti wa kikundi cha Hifadhi ya Mazingira Kikobweni HIMAKI wakati akizungumza kuhusu chanzo cha maji kilichopo Kikobweni mara walipotembelewa na kamati ya Baraza la wawakilishi ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa kuangalia miradi ya Mazingira . PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Wajumbe wa Kamati Baraza la wawakilishi ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Kitaifa wakiangalia Chanzo cha Maji kilichopo Kikobweni Kinachotunzwa na kuhifadhiwa na kikundi cha Hifadhi ya Mazingira Kikobweni HIMAKI huko Chaani Wilaya ya Kaskazini "A"Mkoa WA Kaskazini Unguja . PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Mwenyekiti wa kamati ya Baraza la wawakilishi ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa Mhe. Machano Othman Said akizungumza na wanakikundi cha Hifadhi ya mazingira Kikobweni HIMAKI wakati wa Ziara ya Kamati hiyo kutembelea miradi ya mazingira Wilaya ya Kaskazini "A"Mkoa wa Kaskazini Unguja . PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Mkurugenzi Idara ya Mazingira OMKR Farhat Ali Mbarouk akizungumza kuhusiana na miradi ya mazingira wakati wa ziara ya Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa kuangalia miradi hiyo huko Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa Kaskazini Unguja.ziara hiyo iliongozwa na Waziri wa Nchi OMKR Mhe. Harusi Said Sleiman. PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Mdau wa Mazingira na Mbunge wa Jimbo la Chaani Mhe.Juma Usonge Hamad akizungumza wakati wa Ziara ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa kuangalia miradi ya mazingira Wilaya ya Kaskazini "A" Mkoa wa Kaskazini Unguja, kamati hiyo iliambatana na Waziri wa Nchi (OMKR) Mhe.Harusi Said Sleiman PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Makamo Mwenyekiti kamti ya kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa Mhe Mtumwa Pea akipanda mti katika Shamba la kikundi cha Hifadhi ya Mazingira Kikobweni (HIMAKI) wakati walipofanya Ziara kutembelea miradi ya Mazingira huko Chaani Wilaya ya Kaskazini “A”Mkoa wa Kaskazini Unguja .PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na Rahima Mohamed Maelezo 09/8/2022
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia Ofisi za viongozi wakuu wa kitaifa Mhe Machano Othman Said amewataka watendaji wa mazingira kuhakikisha kuwa sheria za mazingira zinafuatwa katika kuwalinda wanavikundi wanaojihusisha na utunzaji wa mazingira.
Akizungumza mara baada ya kutembelea kikundi kinachojishughulisha na kuhifadhi vyanzo vya maji pamoja na utunzaji wa mazingirahuko Chaani Kikobweni (HIMAKI ) amesema ,kuwepo kwa sheria hizo kutawasaidia wanavikundi kufanya kazi zao za kutunza mazingira kwa ufanisi .
Aidha Mwenyekiti huyo ameiomba Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kushirikiana na Wizara ya kilimo Umwagiliaji Mali asli na Mifugo kuwaelimisha wakulima kupanda miti inayofaa katika maeneo yaliyopo karibu na vyanzo vya maji ili kuzuia vyanzo hivyo visiathirike na kukauka.
Mhe. Machano ameisisitiza Ofisi ya Mkoa kuhakikisha kwamba eneo hilo linalindwa, kuhifadhiwa na kupandwa miti yenye kuleta tija ili kuepuka uvamizi na kuongezeka kwa uharibifu katika vyanzo vya maji.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe Harusi Said Suleiman amesema Wizara yake imejipanga kupanda miti katika wilaya zote za Unguja na Pemba, kuviimairisha vitalu vya awali ili kuweza kuhifadhi mazingira na kuepuka athari za na mmong’onyoko wa ardhi nchini.
Waziri huyo amekipongeza kikundi hicho kwa juhudi wanazochukua za kulinda mazingira na kuwataka wasivunjike moyo na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ili kuleta manufaa kwa vizazi vijavyo.
Nae Katibu Tawala wa Mkoa huo Makame Machano Haji amesema atahakikisha wanasimamia vyema kwa kuwapatia elimu na kuwaunga mkono katika masuala ya utunzaji wa mazingira.
Akisoma Risala ya Mjumbe wa kikundi cha Himaki Mwanaisha Makame Abdalla wamesema kikundi hicho kinakabiliwa na changamoto ya kuvamiwa na watu wanaolima katika maeneo ya hifadhi pamoja na matumizi mabaya katika vyanzo vya maji.
Kamati hiyo imetembelea kikundi cha HIMAKI na mradi wa majiko nafuu katika Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja.
No comments:
Post a Comment